Mkuu huyu nishatumiwa sana picha zake akitaka msaada kuwa anaishi Burkina faso na alitoweka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Congo ya Kinshasa, hii picha inatumika sana kutapelia watu kwenye mitandao na kama wewe ni mfuatiliaji sana wa inshu za net utakubaliana na mimi.
Mara ya kwanza nilipotumia hii picha udenda ulinitoka ila nilipoambiwa nitoe Dollar 300 ili aje Bongo ndo akiri ikastuka kumbe naibiwa, Kiukweli huyu huko aliko ni balaa, na sio mbongo huyu. Heshima kwake anaekula mzigo huu ila kaeni chonjo msije ingizwa chaka kwa kutumia hiyo picha.