Peter Madukwa
JF-Expert Member
- Sep 20, 2012
- 3,139
- 2,485
Wakuu salaam! Mara ya mwisho mwaka jana huyu mtoto wa pili wa marehemu Col. Muamar Gadaffi nilisikia amefutiwa hukumu yake ya kifo kule Libya, baadaye ikasemekana alitolewa gerezani lakini bado ikawa haina uhakika mahali aliko.
Mwanzoni mwa mwezi Mei, 2017 ikasemekana alishambuliwa na wana mgambo wa Libya lakini akanusurika kuuawa.
Inasemekana bado yuko Libya lakini haijulikani yuko libya maeneo gani hasa.
Kuna wengine wanadai bado yupo gereza la Zintan alikofichwa kwa ajili ya usalama wake.
Kama mnavyojua, Seif al Islam ndye mtoto wa pekee wa Ghadafi mwenye elimu kubwa maana ana Phd. Aliyoipata pale London School of Economics mwaka 2007.
Aidha, seif el Islam ni mtoto wa pekee wa Gadafi mwenye ushawishi mkubwa katika 'legacy' ya marehemu Gadafi.
Je, Seif al Islam anaishi wapi hasa?
Je, Seif al Islam atarejea kuiunganisha Libya kurudi katika mstari?