Mtoto wa ajabu India

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
May 9, 2007
3,836
2,792
Kwa kweli haya ni maajabu hivi karibuni tuliona kama si kusikia katika vyombo vya habari kuhusu watoto toka Lindi ambao pamoja na umri wao kuwa mkubwa maumbile yao ni madogo sana, katika hali ya kustajabisha huko India amezaliwa mtoto mwenye vichwa viwili vilivyoungana na katika hali ambayo wazazi wa mtoto huyo hawakutarajia imekuwa ni kama ule usemi wa wahenga usemayo "mgeni njoo, mwenyeji apone" au ule usemao "Kila mtoto huja na riziki yake"
ZAIDI SOMA HAPA CHINI

Kilomita 50 Kasikazini mwa jiji la Delhi katika kijiji cha Noida kazaliwa mtoto wa kike mwenye maumbile yasiyo ya kawaida.Mtoto huyo mwenye umri wa wiki tatu ana Sura (nyuso)mbili na Mafuvu mawili ambayo kwa mujibu wa Madaktari wanaomhudumia yameungana pamoja na hayawezi kutenganishwa.
Habari za kuzaliwa kwa mtoto huyo zimeenea haraka sana na zinasemwa kila mahali.Watu toka India yote na nchi za nje wazidi kumiminika katika kijiji hicho kumwona mtoto huyo.Wanaamini kuwa mtoto huyo ni Mungu wa wahindu aitwae Ganesh mwenye kichwa cha Tembo ambae bila yeye hakuna kitendekacho wala hakuna Ibaada yoyote itakayofanyika. Watu wanakuja katika Familia hiyo ili kupata mibaraka,wanafanya hivyo kwa kupapasa nyao(miguu) ya mtoto huyo,wanaendesha Ibaada inayoambatana na kucheza ngoma wengine wanawazawadia fedha wazazi wa mtoto huyo .
Picha.
1- Mtoto ana afya nzuri na hana matatizo yoyote- kwa mujibu wa Dk
2- Baba wa mtoto-„nilishikwa na woga mara baada ya mtoto kuzaliwa"
Habari zote nimezipata na kuzitafsiri toka MNS.de(Germany)
Alex magere
Rhein str.78
D-76532 Baden-baden
GERMANY.


Mtoto vichwa viwili Mungu wa Wahindu.jpg


Soma taarifa hii toka Haki-hakingowi. http://www.haki-hakingowi.blogspot.com/
 
Back
Top Bottom