Mtoto wa ajabu azaliwa Dodoma

Mtoto wa ajabu azaliwa Dodoma

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,286

Mkazi wa kijiji cha Chibwechangula Behelo wilaya ya Mpwapwa mkoani hapa, Ruth Stanely Matonya (26), amejifungua mtoto wa ajabu wa jinsia ya kike mwenye kichwa nusu.

Mtoto huyo ambaye alikuwa na sura inayofanana na ya chura huku viungo vingine vya mwili vikiwa vya binadamu, alifariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa.

Tukio hilo limetokea jana katika kituo cha afya cha mtakatifu Luke kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mpwapwa.

Kwa mujibu wa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Dk. Edwin Kihura, mama huyo baada ya kufika kituoni hapo alikuwa na uchungu mkali ambao uliendelea bila kukoma huku akisindwa kujifungua hali iliyosababisha afanyiwe upasuaji.

“Pamoja na uchungu huo mkali lakini hakuweza kijifungua kwa njia ya kawaida ingawa njia ilionyesha ipo wazi mtoto aweze kutoka tuliamua kumfanyia upasuaji ili kuokoa maisha ya mama huyu,” alisema Dk. Kihura.

Dk.Kihura alisema maendeleo ya ujauzito wake alipokuwa akifika kliniki yalikuwa hayaonyeshi mkao wa mtoto huyo na mapigo ya moyo yalikuwa hayapatikani .

“Miezi ya mwisho mama huyu alipokuwa akihudhuria kliniki tulikuwa hatupati mkao wa mtoto na mapigo ya moyo yalikuwa hayapatikani lakini mtoto alikuwa anacheza tumboni kitu ambacho kilikuwa kikiwashangaza sana waganga na wauguzi wa kituo hiki,”alisema Mganga huyo.

Alisema baada ya kufanyiwa upasuaji walitoa mtoto huyo, akiwa na sura isiyoeleweka inayofanana na chura na kichwa nusu.

Akizungumzia tatatizo hilo linasababishwa na nini, Mganga huyo, alisema kuna sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na mama kukosa baadhi ya madini mwilini na hivyo uumbaji wa mtoto kutokamilika.

“Unasababishwa na sababu za kibailogia ambazo ni kushidwa kugawanyika kwa kromozome na tatizo kama hili limewahi kutokea mara chache sana

katika hospitali nyingi lakini vitendo hivi vimekuwa vikiongezeka kwa wingi siku hizi za karibuni na kitaalamu linajulikana kama ANECEPHALY,”alisema Mganga huyo.

Aliitaja sababu nyingine kuwa ni baadhi ya kina mama kutumia dawa za kienyeji ambazo ni kali wakati mimba zikiwa changa zinaweka sumu kwa mtoto tumboni.

Alisema hali ya mama huyo inaendelea vizuri katika kituo cha mtakatifu Luke ambako anaendelea kupatiwa matibabu.

Chanzo: Nipashe
 
mkuu Huna Ata Kapicha?
Samahani Lakin
ahsante
Jigo
 
Haikuwa na picha n gazeti
 
nmesoma aya ya kwanza nikatafta picha nlipokosa basi sijaendelea hata mstari mwingine.. hizi story bila picha hazinogi
 
Stori za uongo hizi.
Hata kama imeandikwa Nipashe ni uongo.
Ilikua rahisi kuzuga watu zamani. Yani siku hizi na ulimwengu wa Whatsapp IG n.k. kusiwe na picha hata yenye chenga? Msimu huu wa Escrow, Bomba la Gesi, tutaskia mengi sana. Kuna stori ya mchawi magomeni. Halafu kumbukeni ya babu wa Loliondo baada tu ya uchaguzi.......
 
acha uongo tena uwe na aibu kudanganya watu wazima wenzako
 
Hawa waandishi makanjanja eti 'kromozome'...

Halafu badala ya anencephaly wao wanaandika anecephaly halafu kwa herufi kubwa...

Hahahah!!!
 
Stori za uongo hizi. Hata kama imeandikwa Nipashe ni uongo.....

acha uongo tena uwe na aibu kudanganya watu wazima wenzako

Mmmmh aingiii akilin.

Wabongo umaamuma wenu ndio unaofanya mtumike kama mtaji na werevu...

Kushindwa kwako kuamini habari au taarifa fulani haina maana kuwa unachokisoma au kuambiwa ni uongo...

Sehemu ya kichwa (fuvu na ubongo) kwa mtoto aliyepo tumboni inaposhindwa kukua vizuri ndipo mtoto anapoweza kupata tatizo kama hili...

Muonekano wa mtoto anayezaliwa huwa ni kama hivyo ilivyoelezwa (muonekano wa chura), na kama ni mzazi umekutwa na kadhia hiyo unaweza kukufuru Mungu...

Sasa kwa muda wenu kama mlivyoweza kuingia JF pia nadhani hamtashindwa kufika google...

So try to google image hili neno anencephaly
 
Mimi naamini mtu kama hutaki kuelewa story flan sio lazima kutoa lawama, kama vp unapotezea tuu.
Kukosea herufi moja tuu katika neno hilo ANECEPHALY instead of anencephaly imekuwa shida!!
Ni mengi matukio tena ya ajabu kuliko hilo na hayapati wa kuyaripoti hapa na kwingineko!
Tusivunje watu Moyo wa kutuletea habari!
 
Tatizo watu humu wamezidi u-shigongo. Na mfululizo wa matukio ya ajabu nchini hutokea nyakati zenye hali tete kisiasa/kiuchumi/kijamii...

Vibwengo, popobawa, babu muongo wa Loliondo, n.k. Kibaya kabisa hata vyombo vikubwa vya habari hutekwa kwenye hizo kanyaboya.......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom