Mtoto nje ya ndoa naomba ushauri

Mtoto nje ya ndoa naomba ushauri

Mitihani

Senior Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
158
Reaction score
46
Hbr wana JF.
Upo na mumeo au mkeo kwa zaidi ya miaka 10 mkiishi kwa amani na furaha na mmebarikiwa kupata watoto 2. Siku mmeo/mkeo anakwambia ooh! Blaa blaaa blaaa unajua nilikuwaga na mtoto kabla hatujaoana sasa moyo unaniuma kuweka siri hii leo nimeona nikwambie. Kama ni wewe unafanyaje na kweli ukifwatilia unajua yupo na ni mkubwa kulingana na mlipofunga ndoa na kuna baadhi ya ndugu zake wanajua hili.

Ushauri jamani kama ni wewe unafanyaje?
 
Chukua mtoto changanya na nduguze lea unataka nini tena akiwa mdogo zaidi jua ulikua unasalitiwa
ni mtoto tu kama uliozaa wewe na hana hatia yoyote .
hata wewe unaweza tangulia mbele za haki watoto wako wanakua na jina la watoto wa kambo na mambo
yanakwenda maisha ni nouma.....
 
kwaiyo wewe ulitaka ufanye nini? kwa huo muda mliokaa na mumeo? wewe lea tu huyo mtoto sidhani hata kama ulikuwa unahitaji ushauri hapo................ na ungeambiwa kamzaa hivi karibuni ungeachika?
 
chukua toto yako lea, hataki aondoke....
 
je unajuaje kama na wewe si mtoto wa nje ya ndoa LAKINI UKACHUKULIWA NA KULELEWA KAMA WATOTO WENGINE NDANI YA NDOA YA BABA YAKO NA MAMA YAKO
 
Hbr wana JF.
Upo na mumeo au mkeo kwa zaidi ya miaka 10 mkiishi kwa amani na furaha na mmebarikiwa kupata watoto 2. Siku mmeo/mkeo anakwambia ooh! Blaa blaaa blaaa unajua nilikuwaga na mtoto kabla hatujaoana sasa moyo unaniuma kuweka siri hii leo nimeona nikwambie. Kama ni wewe unafanyaje na kweli ukifwatilia unajua yupo na ni mkubwa kulingana na mlipofunga ndoa na kuna baadhi ya ndugu zake wanajua hili.

Ushauri jamani kama ni wewe unafanyaje?
mtoto ambaye humfuti mavi,humwogeshi ,utamtuma dukani hahahah beba mama tena mlee kwa upole na ustaarabu atakuja kukufaa kuliko hao uliokunya mwenyewe
 
Kulea mtoto si shida, tatizo ni kwanini siri muda wote huoo? Na nilipojaribu kuuliza nikagundua kwamba ni watu waliokuwa wakiwasiliana muda wote huo na isitoshe alijaribu mbinu za kumtenganisha na mimi huyo mzazi mwenzake hadi yeye alipopata mpenzi mwingine na kwenda mbali ya nchi, ndo akaamua kusema. Kwanini asiseme mwanzoni kama tatizo ni kumlea tu. Kwa ufupi ni watu waliokuwa na mahusiano muda wote huo hadi yeye kwenda mbali.
 
Hakuna cha ajabu hapo lea mtoto huyo tena mpende kuliko wako.......ulitaka aseme ili akukose?
 
Kulea mtoto si shida, tatizo ni kwanini siri muda wote huoo? Na nilipojaribu kuuliza nikagundua kwamba ni watu waliokuwa wakiwasiliana muda wote huo na isitoshe alijaribu mbinu za kumtenganisha na mimi huyo mzazi mwenzake hadi yeye alipopata mpenzi mwingine na kwenda mbali ya nchi, ndo akaamua kusema. Kwanini asiseme mwanzoni kama tatizo ni kumlea tu. Kwa ufupi ni watu waliokuwa na mahusiano muda wote huo hadi yeye kwenda mbali.
Jina lako mwenyewe Mthihani solve sasa kamtihani kadogo hako
 
Hbr wana JF. Upo na mumeo au mkeo kwa zaidi ya miaka 10 mkiishi kwa amani na furaha na mmebarikiwa kupata watoto 2. Siku mmeo/mkeo anakwambia ooh! Blaa blaaa blaaa unajua nilikuwaga na mtoto kabla hatujaoana sasa moyo unaniuma kuweka siri hii leo nimeona nikwambie. Kama ni wewe unafanyaje na kweli ukifwatilia unajua yupo na ni mkubwa kulingana na mlipofunga ndoa na kuna baadhi ya ndugu zake wanajua hili. Ushauri jamani kama ni wewe unafanyaje?

swala dogo sana hilo, samehe maisha yaendelee!! na sidhani kama kuna kosa hapo maana huyo mtoto alimpata kabla hajakuwa na wewe' alifanya siri maana hakutaka kukupoteza!!
 
Hbr wana JF.
Upo na mumeo au mkeo kwa zaidi ya miaka 10 mkiishi kwa amani na furaha na mmebarikiwa kupata watoto 2. Siku mmeo/mkeo anakwambia ooh! Blaa blaaa blaaa unajua nilikuwaga na mtoto kabla hatujaoana sasa moyo unaniuma kuweka siri hii leo nimeona nikwambie.

Ndani ya huo muda wote je huyo mtoto alikuwa analelewa wapi na nani aliyekuwa akimlea?
 
mtoto ambaye humfuti mavi,humwogeshi ,utamtuma dukani hahahah beba mama tena mlee kwa upole na ustaarabu atakuja kukufaa kuliko hao uliokunya mwenyewe

We dada una maneno makali
 
Kulea mtoto si shida, tatizo ni kwanini siri muda wote huoo? Na nilipojaribu kuuliza nikagundua kwamba ni watu waliokuwa wakiwasiliana muda wote huo na isitoshe alijaribu mbinu za kumtenganisha na mimi huyo mzazi mwenzake hadi yeye alipopata mpenzi mwingine na kwenda mbali ya nchi, ndo akaamua kusema. Kwanini asiseme mwanzoni kama tatizo ni kumlea tu. Kwa ufupi ni watu waliokuwa na mahusiano muda wote huo hadi yeye kwenda mbali.

Hii dunia kila mtu ana matatizo, VUMILIA
 
Kubali tu matokeo hakuna chakufanya ili kubaadili uhalisia wa yalotokea naelewa unaumia kwasababu unahisi umesalitiwa na umedanganywa lakini ukumbuke huyo ni mumeo na amekosea msamehe tu maisha yasonge mbele...MAJI YAKISHAMWAGIKA HAYAZOLEKI...
 
Mtoto alikuwa akilelewa na mamake na huyo mama huko alikokwenda hatakiwi kwenda na mtoto ni peke yake. Na mtoto kamwacha kwa mamake hadi leo hii.
 
Nipe huyo mtoto nimlee mimi. Na yeyote asiyependa watoto wa kambo nipeni. Watoto ni baraka hawajalishi walipatikanaje mradi wako duniani, ni watoto.
 
...watoto wa nje ya ndoa huwa wanakuwa na mafanikio sana na utajiri
 
Huna jinsi inabidi umpokee huyo mtoto kwa sababu yeye hana makosa. Kumbuka unapompokea mtoto huyo lazima ujiandae na changamoto nyingi zitokanazo na watoto waliolelewa kwingine. Naamini mtoto huyo ni mkubwa hivyo aweza kuwa na vitabia ambavyo hutavipenda yakupasa uvumilie ndio cost ya kufichwa mambo muhimu kama hayo. Tena yakubidi uwe mwangalifu mno aweza leta tafrani hapo home. Baba/Mama hakuna faida ya kuweka siri za namna hii kwa muda mrefu kama mmeamua kuishi pamoja ni vizuri kuwa wawazi tangu mwanzo hata kama uwazi huo utapelekea kuvunja mahusiano yenu ni bora kuliko kuumizana mbele ya safari. Sasa kwenye ndoa ya aina hii tayari imeshaingia kasoro, hapo kuna atakaeitwa mama/baba wa kambo na watu hawa hata wafanye jema kwa jamii ni vibaya tu.
 
Kwanini alificha muda wote huo?uwa nategemea kabla hamjafunga ndoa hivyo vitu vinatakiwa kujulikana..mimi kutoka moyoni sitalea mtu..aendelee kukaa na mama yake tu,au apelekwe kwa bibi mzaa baba si walijua na wakaficha.maana haya mambo ya kusamehe tumesamehee mengi sana.
 
Back
Top Bottom