Mtoto Mtanzania wa miaka 16 alivyoongea kwa kujiamini mbele ya viongozi wa dunia umoja wa mataifa

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,377
8,075
ImageUploadedByJamiiForums1461398732.660065.jpg

Mtoto Mtanzania mwenye umri wa miaka 16 Getrude Clement kutokea Mwanza amehutubia mbele ya viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa umoja wa mataifa akiwa mwenye kujiamini na kutoonekana kuwa na hofu japo anaongea kwenye jukwaa ambalo linatazamwa na viongozi mbalimbali.

Mataifa zaidi ya 150 yalitia saini makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Marekani ambapo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon ndio alimkaribisha Getrude kuongea kwa kusema ‘ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana‘

Getrude alianza kwa kuwasalimia waalikwa huku ikiripotiwa Maraisi 60 walihudhuria na kisha akaeleza kuwawakilisha vijana na watoto ambapo alizungumzia mabadiliko ya tabia nchi, hatari yake na kwamba wamekua wakifikisha ujumbe kwa Wananchi juu ya mabadiliko hayo kama anavyoonekana kwenye hii video hapa chini.
MWANZA MWANZA MWANZA katika ubora wetu.
ImageUploadedByJamiiForums1461398784.877674.jpg

tazama video
 
Nimeipenda sana hii! Msingi mkubwa wa maendeleo yetu pia unategemea jinsi tunavowaandaa watoto wetu, kuwajengea kujiamini na kuwapenda! Mtoto akipendwa akapewa fursa na kusimamiwa vzr atajiamini! Taifa au nchi pia inabidi ionyeshe upendo kwa wananchi wake kwa kiasi kikubwa! Hii inaleta kujiamini! Angalia wamarekani wanavyowalinda raia wao na kuonesha upendo wanapokutana na changamoto mbalimbali as a result mmarekani yyt akisimama kuongea anajiamini sana akijua fika behind me a nation is with me! Hongereni wazazi wa Gertrude!!!
 
huyu mtoto kashaanza kuwa wa kimataifa bado mdogo hivi, je hii inaonyesha ishara gani akishakua?
 
kwenye mada kunasehemu labda imeandikwa kwamba ni binti wa kwanza tz kufanya hivyo?!
ndio maana nimesema pongezi kwake sisi tulienda na faraja akiwa anasoma form two st francis mbeya kwa hiyo alikuwa na umri huo huo
 
Hata viongozi wetu wangekuwa wanatoka miongoni mwa walioandaliwa ingekuwa jambo jema . Haya mambo ya kupata kiongozi kama ngekewa tuu, au zali kumwangukia kwa vile kundi Fulani na Fulani yamekinzana ni hatari. Ndio yanafikisha nchi kuendeshwa bila mwongozo kama getto
 
ndio maana nimesema pongezi kwake sisi tulienda na faraja akiwa anasoma form two st francis mbeya kwa hiyo alikuwa na umri huo huo
kumbe nia yako ni kutueleza ulienda UN new york city!! hapo sasa nimekupata mdada, hongera kwa hilo
 
Back
Top Bottom