niachiemimi
JF-Expert Member
- Feb 18, 2015
- 3,579
- 5,241
Habari zenu wakuu.
Mke wangu ana ujauzito wa miezi 7. Juzi tulikwenda kufanya manunuzi ya vitu kama vile vitenge,kanga na baadhi ya vyombo lakini yote ni maandalizi ya kumpokea kijacho.
Tupo kwenye duka la vitenge na kanga wife wakati anachagua alichagua baadhi ya vitenge na kanga zenye rangi ya njano. Muuzaji alikua ni mama mtu mzima(age go) alimwambia wife kua hata mimi ni mama sikushauri mwanangu uchukue hizi nguo zenye rangi ya njano maana utaleta manjano kwa mtoto.
Nilishtuka nikamuuliza mama je hata matunda kama embe nayo yanarangi inayofanana na njano, akasema maembe asile kwa kipindi hiki.
Hapa naomba ushauri na udhoefu wenu juu ya manjano hasa kwenye nguo za njano wakati mama anajifungua na ulaji wa maembe. Maana wife alikua anakula sana maembe ila ameacha juzi baada ya kupewa darasa na huyo mama wa vitenge.