Sheria zetu zimeweka wazi kuwa mtt chini ya miaka 12 hawezi kuhukumiwa kwa kosa la jinai isipokua na endapo tu itathibitika kua wakati akifanya kosa hilo alikua akitambua fika kua anachofanya ni kosa.(yn alikua akielewa kua hakupaswa kufanya hilo jambo)
Lakini mtt chini ya miaka 7 hawezi kuhukumiwa kwa kosa la jinai la aina yoyote...hii ni kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (Penal Code) kf 15
Sambamba na hilo wtt wanamahakama zao maalumu, juvenile courts na adhabu hutolewa kwa hekima za majaji, kwa kuzingatia uzito wa kosa husika, madhara na sababu nyinginezo km wataona inavyofaa...
Vilevile adhabu mara nyingi huwa ni nyepesi na zile za kulenga kuwabadilisha wtt kitabia mfano viboko, kazi nyepesi nk