Habari zenu members wa Jf,
Kuna shida inatanitatiza kwa mtoto wangu wa kike mwenye umri wa miaka mitatu, ni kwamba amekuwa na kawaida ya kutokwa na maji meupe kama maziwa sehemu zake za siri kila baada ya muda flani, nimejaribu kumpeleka hospital mbalimbali naambiwa U.T.I anapewa dawa na muda mwingine sindano lakini tatizo linajirudia tatizo linaweza kuwa nini?
Naombeni ushauri, mana najua Jf kuna madaktari bingwa wapo humu, Mara ya mwisho nguo zake zilifuliwa na Dettol ili kuuwa vimelea lakini tatizo limerudi tena, naomba ushauri.
Asanteni!.
Habari!
Pamoja na michango yote, naomba kuongeza au kuweka sawa baadhi ya mambo:
1: Ute mweupe na mchanganyiko kama maziwa ni ishara ya uwepo wa maambukizi ya fangusi/ more suggestive. Ila ni nzuri pia mtaalamu wa afya akiuona au hata kupimwa pia.
2: Si vyema kumpa mtoto wa miaka mitatu dawa za kutumbukiza kwenye uke, utaratibu ni kutoa dawa ya kupaka na ikishindikana ya kunywa.
3: Kulingana na historia ya ugonjwa wa mtoto, huwezi kuliacha tu hili la UTI. Unapopima maambukizi ya njia ya mkojo kwa hali iliyojitokeza kwa mtoto kama huyu ni vyema kuhakikisha anasafishwa vyema kabla ya kutoa sample ya mkojo. Pia, ni muhimu kufanya uoteshaji/culture&sensitivity pale ambapo kipimo cha urine routine/urinalysis ni chanya/positive..
4: Matumizi ya antibiotics mara kwa mara au kwa muda mrefu huweza kulinfanya tatizo kuanza au kuwa zaidi kutokana na kuua bakteria wazuri/balansi (ecosystem) walioko kwenye njia ya uzazi.
5: Ni vizuri kujifunza jinsi mtoto anavyofanyiwa usafi. Matumizi ya sabuni/na hasa medicated kumsafisha mtoto sehemu ya siri yanaweza kuwa ni chanzo cha tatizo.
Matumizi ya baby wipes, hasa zenye uwezo wa kuua bakteria kama zile zenye alcohol/pombe ni shida pia.
Si vyema pia kuingia vidole ndani sana wakati wa kumsafisha/ douching.
NB: Mtoto huyu ni vyema kuangaliwa kwa ukaribu zaidi na upendo kati ya mzazi na daktari bingwa wa magonjwa ya watoto asiye na haraka.
Ni vyema kukusanya ushahidi vyema, na mlolongo wote na kufanya kitu kidogo tu, ambacho chaweza kumsaidia sana mtoto.
Hali hii yaweza kuwa ni complications ya yaliyotajwa hapo juu. Umakini unahitajika ili kutoendelea kumpa madhira mtoto.
Matibabu mema.