Mtoto 'Kibonge' Mwenye Uzito wa Kilo 8.7 Azaliwa Indonesia

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Mama mmoja wa nchini Indonesia alipata tabu sana kujifungua mtoto mnene kuliko kawaida mwenye uzito wa kilo 8.7 ambaye taarifa zinasema hata jinsi anavyolia ni tofauti na watoto wenzake kwani anatoa sauti kali kuliko kawaida.</SPAN>

Mwanamke mmoja wa nchini Indonesia amejifungua mtoto mwenye mwili mkubwa kuliko watoto wote waliozaliwa nchini humo akiwa na uzito wa kilo 8.7.

Mtoto huyo wa kiume ambaye wazazi wake bado hawajampa jina ana urefu wa sentimeta 62 na alizaliwa jumatatu kwa njia ya operesheni kwenye hospitali moja iliyopo kwenye mji wa Sumatra uliopo kaskazini mwa Indonesia.

"Mtoto huyu kutokana na unene wake aliifanya operesheni iwe ngumu sana hasa hasa wakati wa kumtoa kwenye tumbo la uzazi la mama yake, miguu yake ni mikubwa sana", alisema daktari mmoja katika hospitali hiyo.

Mtoto huyo alizaliwa akiwa na afya njema ingawa awali iliwabidi madaktari wamwekee mirija ya oxygen kutokana na kuwa na matatizo ya kupumua.

"Kila baada ya dakika chache anasikia njaa na kuanza kulia, inabidi kumnyonyesha kila baada ya dakika chache".

"Mbali na unene wake usio wa kawaida, hata jinsi anavyolia ni tofauti na watoto wenzake, ana sauti kali sana", alisema daktari huyo.

Unene wa mtoto huyo unasemekana kuwa umesababishwa na mama yake kuwa na ugonjwa wa kisukari.

Mama wa mtoto huyo ana watoto wengine watatu ambao aliwazaa kwa njia ya asili.

Wataalamu wa mambo ya uzazi walisema kwamba wakati kiwango cha sukari cha mama mjamzito kinapokuwa juu, mtoto aliye tumboni naye hupokea kiwango kikubwa cha sukari ambacho humfanya awe mnene zaidi.



Source: AFP

 
Du licha ya unene wote huo lakini bado mtoto anakula msosi kwa sana, baada ya muda mfupi huo uzito utaongeza mara mbili. Hivi hakuna namna ya kupunguza unene kwa huyo mtoto, kama vile mazoezi n.k
 
Ndy tatizo ya kuzaa watoto wanene! Naskia kawaida wanatakiwa wanyonye sana
 
Back
Top Bottom