Mtoto HAWA MOHAMMED wa Kenya ameokotwa

Mtoto HAWA MOHAMMED wa Kenya ameokotwa

jaffari yogo

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2014
Posts
685
Reaction score
148
Kuna mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 13 hapa wilayani Bunda mkoa wa Mara Tanzania ambaye alipotea kutoka kwao Sehemu ya MIGORI KENYA. Alikuwa anasoma darasa la 7 katika HASARY JOHAN PRIMARY SCHOOL ilioko Migori.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo anaitwa mwalimu BEN, mwalimu wa English na kiswahili anaitwa MKUNE na mwalimu wa Hesabu ni MBUSIRO. Huyu mtoto anaitwa HAWA MOHAMMED jina analotumia shuleni na nyumbani au Boke. Baba wa mtoto anaitwa MOHAMMED au DEO.

Amedai pale Migori anaishi karibu na kituo cha mafuta yaani Petrol station (TOTAL) karibu na centre ya Migori. Tafadhali anayeweza kumfahamu huyu mtoto tuwasiliane kwa namba +255788043177.

Utani tuache ni suala muhimu sana hili tafadhali. Let us be serious on this please!.
 
Mkuu katoe taarifa kituo cha polisi ni rahisi sana kwa wao kuwasiliana na watu wa uhamiaji pale Musoma na akarudishwa kwao kwa gharama za serikali kwa kuwa details zake zinajulikana..

Ila kibongo bongo lazima Polisi wakuzingue kidogo uwaachie chochote maana dah, hili li-nchi lishajiozea liko kwenye auto-pilot
 
Hutaki utani wakati wewe mwenyewe umeleta utani..!?
 
Vp nikupe namba mh. Kenyatta au fuata taratibu balozi wa kenya nchini tz kwani swala ilo ni la kimataifa au mh Six S
 
Mkuu katoe taarifa kituo cha polisi ni rahisi sana kwa wao kuwasiliana na watu wa uhamiaji pale Musoma na akarudishwa kwao kwa gharama za serikali kwa kuwa details zake zinajulikana..

Ila kibongo bongo lazima Polisi wakuzingue kidogo uwaachie chochote maana dah, hili li-nchi lishajiozea liko kwenye auto-pilot

Taarifa ziko polisi mkuu
 
Back
Top Bottom