Mtoto anashtuka mara kwa mara

Nyleptha

Member
Jun 19, 2012
69
47
Habari madaktari wa JF?

Naomba msaada wenu, nina mtoto wa kiume ana miezi 7 sasa, tatizo tangu amezaliwa anashtuka sana na mara kwa mara, yaani mshtuko wa mtu anayeogopa kitu ukidondosha hata kijiko tu anashtuka sana hadi anatafuta sehemu ya kujishikilia, kama umembeba anakudaka nguo haraka, akiwa amelala anadaka shuka mradi kutafuta salama yake!

Tumemzoesha katika mazingira ya kutokuwa kimya sana, redio, tv tunawasha kama kawa na analala vizuri, pia tunaangusha vitu vyenye kelele ili azoee lakini wapi.

Akiwa macho ndio kasheshe, ikipigwa honi atashtuka karibu adondoke huku macho yamemtoka kwa hofu. Sijui ni tatizo gani na tiba yake ni nini?
 
Polen sana mzazi. Nashauri mumuone Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto naye atakushauri accordingly...
 
nasikia watoto wadogo wanaona vitu ambavyo havionekani kwa macho ya kiutu uzima sijui kuna ukweli.?
 
Mkuu ikishindikana Hospitali Dawa ya kutibu mtoto kustuka stuka jaribu Dawa yangu hii ya Tiba Mbadala:>

Chukua dawa inayoitwa Mvuje, halititi na kibiriti upele zitwange kisha roweka katika maji kwa muda wa saa kisha muogeshe mtoto kwa maji ya dawa hizo asubuhi, mchana, na jioni. Inshaallah ataacha kushtuka. Tumia kisha unipe Feedback. mkuu.@Nyleptha Source. Phd.MziziMkavu.
 
Poleni sana ni kawaida kuwa mtoto anakuwa na hisia kali ila la kushtuka nawashauri mumpeleke hospitali kwani kuna umuhimu wa ushauri wa daktari,japo wanagoma hawamadaktari mjitahidi kwani magonjwa mengine huanzia udogoni na kukomaa matokeo yake hayana dawa, kama hawa wanao jambishwa na kustuka wangewahiwa wasingekuwa hivyo.
 
Mkuu ikishindikana Hospitali Dawa ya kutibu mtoto kustuka stuka jaribu Dawa yangu hii ya Tiba Mbadala:>

Chukua dawa inayoitwa Mvuje, halititi na kibiriti upele zitwange kisha roweka katika maji kwa muda wa saa kisha muogeshe mtoto kwa maji ya dawa hizo asubuhi, mchana, na jioni.Inshaallah ataacha kushtuka. Tumia kisha unipe Feedback. mkuu.@Nyleptha Ph.D.MziziMkavu.

duh, hizo dawa ulizotaja zinapatikana wapi? manake sijawahi kuzisikia doctor MziziMkavu, naomba unielekeze nizisake haraka. halafu niliwahi kusikia eti kama mama mjamzito aliwahi kuanguka akiwa mjamzito mtoto anazaliwa na woga pia, sijui ni kweli, wenye uzoefu nijulisheni
 
Tafuta mhaya kama unamjua yeyote mwambie unataka dawa inaitwa "ekitatela nte"inapatikana sehemu zote za nchi hii ukipata chemsha majani yake kisha ikipoa mpe mtoto 5mil asubuhi Mchana na jioni kwa siku tatu.Na baada ya hapo acha na uwe unampa mara moja kwa mwezi yaani tarehe sawa na ya kuzaliwa kwake.

Ila usisahau kumuona Daktari kwa uchunguzi zaidi kuona kama kuna tatizo zaidi ya hofu kwa mtoto.

MITISHAMBA INA VIRUTUBISHO NA NI DAWA YA MARADHI YETU.
 
Pole sana, mpeleke hospitali kwa daktari wa watoto huenda akawa ana malaria au UTI, pili kama una belive in jesus, nakushauri mpeke kanisani akaombewe.wakwangu alikuwa analia sana usingizini mpaka nachanganyikiwa, nilipo mpeleka kuombewa tatizo limeisha, Jaribu akiwa amelala mlaze kwa ubavu. Pole sana mungu atamsaidia
 
Tafuta jirani wa Kihaya mwambie tatizo lako. Wahaya wanachukulia hilo tatizo very seriously. Mama yangu alikuwa anampa mwanangu dawa inaitwa kitatela nte, huku akinambia kushtuka shtuka ni dalili mbaya sana; sikuwa naelewa ila nilikuwa nawapa watoto wangu hizo dawa. Anasema mtoto anayeshtuka anaweza kupata degedege akipata homa kali.

Na ukitaka kujua kuwa hizi dawa zina work; mama alikuwa ananambia ni very rare kukuta uhayani mtu ameathirika na degedege au mama mjamzito amepata kifafa cha uzazi

Hii dawa wahaya wengi wameipanda dar kama maua majumbani kwao kwani wanaamini they can't without it.
 
duh, hizo dawa ulizotaja zinapatikana wapi? manake sijawahi kuzisikia doctor MziziMkavu, naomba unielekeze nizisake haraka. halafu niliwahi kusikia eti kama mama mjamzito aliwahi kuanguka akiwa mjamzito mtoto anazaliwa na woga pia, sijui ni kweli, wenye uzoefu nijulisheni
Mkuu Nyleptha inaonyesha wewe ni mtu

wa bara Dawa hizo zinapatikana Sokoni Kariakoo Mtaa wa pemba kwenye Maduka ya Wapemba wanaouza Dawa za

kiarabu ukifika mtaa wa nyamwezi na Pemba uliza Wenyeji wa hapo Maduka ya Wauza Dawa za kiarabu maduka ya

wapemba watakuonyesha Kama upo Dar. La kama haupo Dar Waulize waarabu wowote walio karibu na wewe yaani majirani zako watakufahamisha hizo dawa wapi waweza kuzipata.
 
Last edited by a moderator:
Kwa msaada wangu maana hayo nilishayapitia ,kwa sasa nina watoto wa3,,tafuta jani la roseflower alafu ulisage liwe kama unga then chukua maji kidogo kama kijiko kimoja mdondoshe puani kidogo kidogo ukae kama dk 3.

Ataanza kupiga chafya umuache apige chafya mpaka atakapoacha mwenyewe uhakikishe unampa asubuhi kabla jua halijachomoza na jion mda wa saa 2 na kuhakikishia atapona na umpe kila mwezi mpaka atakapo fikisha umri wa miaka 4.
 
Chango hilo(huwa kali zaid kwa watoto wa kiume)likikomaa itakua degedege,tafuta wahaya wakusaidie ni hatari sana! ...
Pia uwe na mazoea ya kumrusharusha mara tu amalizapo kuoga kabla hujamkausha maji itampunguzia uoga!
 
Sauti hzo ni kali sn kwa mtoto zinamuumiza masikio kwani ngoma ya ckio bdo laini sana tofaut na m2 mzm. Jitahd kumuepusha mtoto na hzo sauti kwani kumzoesha haisadii zaid ya kumumiza.
 
Mkuu ikishindikana Hospitali Dawa ya kutibu mtoto kustuka stuka jaribu Dawa yangu hii ya Tiba Mbadala:>

Chukua dawa inayoitwa Mvuje, halititi na kibiriti upele zitwange kisha roweka katika maji kwa muda wa saa kisha muogeshe mtoto kwa maji ya dawa hizo asubuhi, mchana, na jioni.Inshaallah ataacha kushtuka. Tumia kisha unipe Feedback. mkuu.@Nyleptha Source. Phd.MziziMkavu.
Halititi ni nini naomba msaada
 
Pole sana mkuu, ila naamini si ugojwa maana hali kama iyo alikua nayo kijana wangu wa kwanza, ilifika kipindi nikahisi yuko na magojwa ya moyo lakini wapi, alivyozidi kukua iyo hali ilikuja kuisha yenyewe.

Wakati nina ujauzito wa pili nilijikuta nikipenda sana kusoma kuhusu ukuaji wa mtoto tumboni na ndipo niligundua shida aliyokua nayo kijana wangu wa kwanza, mtoto hua anaanza kusikia tangu akiwa tumboni, hivyo kipindi cha mimba kama mama atakua anakaa katika maeneo tulivu mtoto atakayezaliwa atakua na shida kama ya mtoto wako ila hali hiyo itakuja kuisha kwa kadri atakavyoendelea kukua.
Nakuhakikishia hana ugojwa wowote, wakwangu mpaka anafikisha mwaka tulikua ata ukiwasha blender analia vibaya sana maana alikua akiogopa sauti.

Mimba ya kijana wangu wa pili imelelewa uswahilini full kurupushani na kelele za kila aina, sijaona iyo shida ata upige kelele gani haimpi shida yeyote.

Kunaweza kukawa na tiba mbadala maana jadi haishidwi jambo ila hana shida yeyote kiafya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom