Mtoto amua mwenzake kwa bunduki

Mtoto amua mwenzake kwa bunduki

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,775
Reaction score
37,960
Mtoto amua mwenzake kwa bundukiNa Hussein Semdoe, Handeni

MTOTO Hashiruna Hassan (5) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Awali ya Suwa iliyopo katika Kijiji cha Suwa Kata ya Mazingara wilayani Handeni , amekufa baada ya kupigwa risasi na dada yake Mwanaidi Hassani (8).

Mwanaidi alimpiga Hashiruna risasi hiyo kichwani sehemu ya jicho kwa kutumia bunduki ya baba yao aina ya gobore wakati walipokuwa wakiichezea nyumbani kwao.

Akizungumzia suala hilo Afisa Mtendaji wa kata hiyo, Hassani Lugundi alisema tukio hilo lilitokea saa 4:00 usiku wa kuamikia jana. Mgundi alisema wakati tukio hilo likitokea baba yao hakuwepo nyumbani kwake. Alisema kuwa tayari polisi wilaya ya Handeni walifika jana katika eneo la tukio.
 
Wanasheria, hivi huyu mtoto atawekwa ndani?, ama mwenye silaha ambaye ndio naona ni mzembe kwa kiasi fulani.

Pole kwa wafiwa. Na ulale pema Peponi Malaika.
 
Back
Top Bottom