Mtoto amshitaki babake akimdai urithi wa babu yake

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,983
11,400
Jamaa yangu kapata mkasa anashitakiwa na mtoto wa mdogo wake akitaka urithi wa nyumba iliyojengwa na baba yake hiyo imekaaje kisheria?

Kisa ni kuwa mzee mmoja alikuwa na watoto wawili alivyofariki mjane aliachwa kwenye nyumba na wanae wawili, badae ajuza nae akafariki, wakabaki watoto nae mtoto mmoja akafariki. Akabaki kaka mtu.

Sasa mtoto wa ndogo mtu anamshitaki babake mkubwa akitaka urithi wa ngumba ya babu yake, hiyo imekaaje kisheria?
 
Wapi hiyo imetokea,

Hiyo ntoto hana adabu, ni mvivu na mpuuzi hataki kutafuta vyake ataka vya bure,
 
Ni haki yake, kama jamaa yako anafaidika yeye na kusahau watoto wa mdogo wake, kijana afanyeje?, au babu aliandika wosia jamaa yako ndiye mrithi pekee?,kama jibu siyo mrithi pekee, dogo ana haki ya jasho la babake..
 
Babu yake hakuacha wosia na watoto waliishi poa tu na mama yao, sasa dogo anamkomalia babake mkubwa,
 
Habari ya hapa, hii kesi nimekutana nayo hapa Mwanza, ila kaka mtu anadai yule ni mtoto wa nje ya ndoa, wapo inakuwaje?
 
Kama no mtoto nje ya ndoa kwa imani ya kiislam hana chake labda baba yake mkubwa amfanyie wema tu ampe chochote tu kwa kuwa ni damu yao!
 
Utajuaje kama ni wa nje ya ndoa wakati babake na mamake walishafariki, kabaki babake mkubwa tu.
 
Kwa islamic law ana haki maan alivyokufa babu baba ake alirithi so anapokufa baba yey ambaye ni km mjukuu ana haki kupitia urithi wa baba ake ambaye pia alishafariki,ila inategemea vipo vilikaa vip yaan mpangilio but kam alikufa babu akafa baba mjukuu ana haki ya baba ake kwa babu kiislam,ila km baba ake huyo mjukuu ndo alianza kufarik afu ndo babu hapo ndo mjukuu atakua hana haki ya urithi pia km huyo mjukuu ni wa nje ya ndoa pia kiislam hawez kurith but km alizaliwa ndani ya ndoa ana haki.
 
Kama babu aliishi maisha ya kiislam, kikristo au kijamii, niwazi kuwa huyo mtoto ana haki ya huo urithi wa sehemu ya nyumba.
Kama babu alikufa bila wosia basi sehemu ya haki "by way of transmission" ilirithishwa kwa baba mtu, then baba mtu alipokufa kama hakuacha wosia ile sehemu ya haki "by way of transmission", ilienda kwa mtoto ambaye ndiyo mlalamikaji.
Mtoto anachotakiwa kuprove kuwa yeye ni mtoto halali wa huyo baba aliyekufa.
 
Back
Top Bottom