Mtoto amkataa mama yake na kutaka kuishi na mama wa kambo

jr.kiyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
787
4,863
Kuna habari hapa kuna dogo huko Tunduru mkoa wa Ruvuma umri miaka 11 amemkataa mama yake mzazi kwa madai ya kwamba ana mshurutisha sana, dogo alipopewa nafasi ya kujieleza mbele ya kikao rasmi cha kijiji,alisema kuwa mama yake huyo anamlazimisha kufua nguo zake kitendo ambacho yeye hakubaliani nacho.

Na la kustajabisha ni pale dogo alipodai anataka kwenda kuishi kwa mama yake wa kambo kitu ambacho kilichowashangaza watu wengi na pia alitoa tahadhari kama atalazimishwa kuishi na mama yake mzazi basi atafanya jambo lolote baya ikiwemo kujiua.

Dah...........
 
huyo anatakiwa mboko tu wala si vinginevyo, wakimlea jinsi anavyotaka eti kisa atajiua wajue kuwa wanamharibu. kwani mama yake kumwambia afue nguo zake ni kosa!!! yaani hakataki kufundishwa kazi. %^%$#@!@#$ wamlete kwangu kama wiki moja then arudi huko Tunduru angenyooka nyambafu zake mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Katika hali ya kusikitisha kama siyo kustajabisha imetokea huko Tunduru mkoa wa Ruvuma,mtoto mwenye umri wa miaka 11 amemkataa mama yake mzazi kwa madai ya kuwa anamshurutisha sana,alipopewa kuongea dogo amedai kuwa mama yake amukuwa anamlazimsha sana kufua jambo ambalo hakulipenda.
Dogo huyo ameomba akakae kwa mama yake wa kambo kuliko kuishi na mama yake mzazi. Na amedai atafanya jambo lolote baya ikiwemo na kujiua iwapo atalazmishwa kuish na mama yake mzazi.
 
Ruvuma kule kwa yule jamaa aliyekuwa anaDO na mama yake.
Usikute dogo hajui habari za wet dreams. Kila 'tone' linatua kwa maza wa kambo.
 
upuuzi kisa anafua...sasa asipoaznaa kufua umri hu huko mbele si atakuwa anataka afuliwe na kila mtu....pambafu dogo huyo akora zinahusika...
 
Hapo ni malezi inaonekana mama yake wa kambo ana mlea vizuri kwa kumdekeza lakini asihukumiwa kwa jambo maana kupiga siyo kufundisha.
 
Kuna habari hapa kuna dogo huko Tunduru mkoa wa Ruvuma umri miaka 11 amemkataa mama yake mzazi kwa madai ya kwamba ana mshurutisha sana, dogo alipopewa nafasi ya kujieleza mbele ya kikao rasmi cha kijiji,alisema kuwa mama yake huyo anamlazimisha kufua nguo zake kitendo ambacho yeye hakubaliani nacho.

Na la kustajabisha ni pale dogo alipodai anataka kwenda kuishi kwa mama yake wa kambo kitu ambacho kilichowashangaza watu wengi na pia alitoa tahadhari kama atalazimishwa kuishi na mama yake mzazi basi atafanya jambo lolote baya ikiwemo kujiua.

Dah...........
BONGO FLAVOUR AKA KIZAZI KIPYA
 
Unajua utandawaz sasa iv unaharibu sana watoto yan hawatak kabisa kujifunza kaz za mikono. Mi nakumbuka nikiwa na miaka hyo tena nililelewa na mama wa kambo kaz mtindo mmoja. Ila mama ake anajaribu kumjenga nakumtengenezea msing wa maisha yake ya badae aweze kuja kuish na kila MTU.
 
Mtoto wa miaka 11 kufua nguo zake kuna shida gani, hawa watoto wa siku hizi ni wa ajabu sana. Mama yake anamjenga kuwa mwanadamu bora, mwanadamu anayefaa kwenye jamii yeye analeta figusifigusi za kutishia watu wazima.
Nguo za Mama yake!
 
Kuna habari hapa kuna dogo huko Tunduru mkoa wa Ruvuma umri miaka 11 amemkataa mama yake mzazi kwa madai ya kwamba ana mshurutisha sana, dogo alipopewa nafasi ya kujieleza mbele ya kikao rasmi cha kijiji,alisema kuwa mama yake huyo anamlazimisha kufua nguo zake kitendo ambacho yeye hakubaliani nacho.

Na la kustajabisha ni pale dogo alipodai anataka kwenda kuishi kwa mama yake wa kambo kitu ambacho kilichowashangaza watu wengi na pia alitoa tahadhari kama atalazimishwa kuishi na mama yake mzazi basi atafanya jambo lolote baya ikiwemo kujiua.

Dah...........
Tatizo ni malezi kwani alichofanya mama mzazi kitu kinachofanya na wazazi wengi. Umri aliofikia huyo kijana anapaswa afanye hivyo na kama mama yake wa kambo hafanyi hivyo kutokana na kutaka kukubalika kwake kwa huyo mtoto basi iweleweke kuwa anamharibu mtoto huyo 'SAMAKI HUKUNJWA AKIWA MBICHI'
 
Itakuwa mama wa kambo anapika vizuri kwa sababu ni mpya kwa baba yake na ile unafiki wa mwanzo wamwache aende huko akakae hata mwaka ndo atajua alieingia labor na anayemkimbilia yupi bora, watoto wanadanganywa na tabasamu la usoni na chakula lkn hajui moyo huficha mengi mwache aende akaione dunia, mama ni mama ipo siku atakumbuka
 
Usipozaa fibroids ukizaa ndo haya jamani watoto muwe na huruma,sasa huyo mama yake wa kambo ataishi milele kumfulia?
 
Back
Top Bottom