Mtoto aliyenusurika ajali ya Lucky Vincent asimulia jinsi wenzake 35 walivyokufa

ng'ombo

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
418
619
Screenshot_2017-05-10-09-40-22-1-1.png

KUFELI kwa breki la basi la shule ya msingi ya mchepuo wa Kiingereza ya Lucy Vicent na udereva usio na uzoefu, vinahofiwa kuwa sababu ya ajali ya basi hilo iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa basi hilo.

Akizungumza jana , mmoja kati ya wanafunzi wasiozidi watatu walionusurika kwenye ajali hiyo, Urusula Godfrey, alisema mvua kubwa ilikuwa ikiyesha kabla ya ajali hiyo kutokea.

Kwa mujibu wa Urusula, ghafla aliona gari limeruka ambapo yeye wanafunzi wenzake wakiwemo waliokufa katika ajali hiyo, walibaini si mruko wa kawaida na mara moja walianza kupiga kelele za kuomba msaada.Wakati wakipiga kelele hizo bila msaada, Urusula alisema alishuudia basi hilo likianza kuserereka mpaka mtoni (Mto Marera), ambako lilipinduka na kuanza kuviringika.

Baada ya hapo Urusula alisema hakutambua kilichoendelea zaidi ya kujikuta tu yupo hospitalini, alisema na kushindwa kuendelea kusimulia mkasa huo na kuanza kububujikwa na machozi kwa uchungu.
 
Nilimsikiliza Bonge wa Clouds ambaye aliliona basi lililopata ajali. Anasema kilichomshangaza siti za hilo basi ziling'oka zote na hazikuwa na umadhubuti.
 
Ile Gari haikuviringika ukiitazama baada ya ajali, kwa kutazama Uharibifu wa kwny gari inaonekana iliruka ukaenda kukita kwa mbele na hilo ndilo lilileta Madhara zaid

Kwa Nyuma ya gari Hakuna Madhara yoyote na kwa mbele kumeharibika kabisa na pia kuna Udongo mwingi ambao ulitokana na gari kukita kwa mbele kitu kilichopelekea mpaka siti za gari kuchomoka na Wote kwenda kukita kwa mbele!

Kama Gari ile ingekuwa na Seat belt Basi huenda waliokuwa siti za Nyuma wangesalimika Kama pia Viti visingeng'oka lakin kwa ajali ile mkanda usingesaidia kitu
 
Nilimsikiliza Bonge wa Clouds ambaye aliliona basi lililopata ajali. Anasema kilichomshangaza siti za hilo basi ziling'oka zote na hazikuwa na umadhubuti.
Ni kawaida kung'oka viti kama umewahi kushuhudia ajali za magari yaliyoviringika kwa ajali
 
Ile Gari haikuviringika ukiitazama baada ya ajali, kwa kutazama Uharibifu wa kwny gari inaonekana iliruka ukaenda kukita kwa mbele na hilo ndilo lilileta Madhara zaid

Kwa Nyuma ya gari Hakuna Madhara yoyote na kwa mbele kumeharibika kabisa na pia kuna Udongo mwingi ambao ulitokana na gari kukita kwa mbele kitu kilichopelekea mpaka siti za gari kuchomoka na Wote kwenda kukita kwa mbele!

Kama Gari ile ingekuwa na Seat belt Basi huenda waliokuwa siti za Nyuma wangesalimika Kama pia Viti visingeng'oka lakin kwa ajali ile mkanda usingesaidia kitu
Mkuu ukute hata mtoto hajasimulia kitu, hizi habari za udaku tu.
 
Tukusikilize wewe au aliyekuwepo wakati wa tukio!

Upendavyo, Maneno yangu si Sheria wala kanuni,
Tazama comment no.1 kuna Picha ya gari hapo juu sehemu ya juu ya gari haijaharibika hata kidogo sasa huko kuvingirika ilivingirika vipi kusilete hata michubuko kwny bodi kwa juu?

pia usilazimishe wote tuamini hiyo story ambayo hatujui Kama ni ya Mtoto kweli maana mpaka sasa Watoto wote watatu walionusurika wapo ICU, sasa sijui hayo Mahojiano yalifanyikia hapo ICU au kabla ya kufikishwa ICU?
 
Ni kawaida kung'oka viti kama umewahi kushuhudia ajali za magari yaliyoviringika kwa ajali
Sijawahi kushuhudia ajali bali nimewahi kuwa manusura ya ajali ambayo watu nane walipoteza maisha. Hiyo gari ilibiringika mara nne na kwa bahati ilipozuiwa mti ndipo ilipokoma kubiringita. Na kilichoniokoa ni kuing'angania miguu ya siti za Coaster. Na waliokufa ni wale waliokuwa wanataka kuruka wakati ikibiringita na wengine kutokana na kukanyagana au kusukwasukwa wakati ikibiringita.
Tatizo kubwa watu wengine huwa wanang'oa siti zilizokuja na magari ili kuongeza idadi ya siti au kuongeza eneo la katikati ya basi ili kuongeza wingi wa abria watakao simama. Na hizo siti zinanakuwa imara kwa muda mfupi na baada ya muda utaona zinaanza kuchezacheza na kupoteza umadhubuti katika vishikizo vyake. Zikipata dharuba zinang'oka.
Lakini kusalimika kwenye ajali ni mipango ya mungu, vitu vingine ni ziada na vinaweza kunusuru maisha pindi vitapotumiwa ipasavyo.
 
Back
Top Bottom