Mtoto afariki baada ya kukeketwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto afariki baada ya kukeketwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Dec 29, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Ngariba wa miaka 70, mkazi wa kijiji cha Irienyi Kinesi, wilayani Rorya, mkoa wa Mara, Nyaisanga Marwa, amekamatwa na Polisi na anatarajia kufikishwa mahakamni kujibu mashitaka ya kumkeketa mwanafunzi wa darasa la pili wa Shule ya Msingi Irienyi (jina tunalihifadhi) na kumsababishia kifo, baada ya kutokwa na damu nyingi kwenye sehemu aliyokatwa.

  Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Tarime/Rorya, Justus Kamugisha, jana alisema kuwa, tukio hilo lilitokea Desemba 19, mwaka huu, katika kijiji cha Irienyi Kinesi, wilaya ya Rorya na kwamba baada ya mtoto huyo kukeketwa, alitokwa damu nyingi iliyoendelea kutoka bila msaada wowote kwa matumaini kuwa atapona kwa miti shamba.

  Kamanda huyo alisema, Desemba 23, mwaka huu, mtoto huyo (9) alipoteza maisha na kwamba Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na ndugu wa marehemu walimkamata ngariba huyo kabla hajatoroka na hadi sasa yupo mikononi mwa Polisi na wanatarajia kumfikisha mahakamani wakati wowote kujibu shitaka la kukeketa na kusababisha kifo.

  MTOTO ANUSURIKA KUOZWA

  Katika tukio lingine, mtoto wa darasa la nne katika shule moja ya msingi jijini Dar es Salaam ambaye ni yatima, amenusurika kuozwa kwa nguvu na baba zake wakubwa, ili zipatikane ng’ombe za kumwezesha kaka yake kuoa.
  Tukio hilo llitokea hivi karibuni baada ya mwanafunzi huyo kwenda na mlezi wake kwenye msiba wa mama yake katika kitongoji cha

  Nyamoko, kijiji cha Mahanga, kata Mihingo, Tarafa ya Chamriho, wilayani Bunda, mkoa wa Mara.
  Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Francis Isack, amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) alinusurika kuozwa na baba zake wakubwa baada ya mlezi wake kutoa taarifa kwake kuhusiana na mpango huo.

  Isack alisema kuwa, mama mzazi wa mtoto huyo alifariki Desemba 10, mwaka huu na kufanyiwa mazishi kijijini hapo na kuongeza kuwa mtoto huyo alifuatana na mlezi wake, Noela Haruni Chacha, mkazi wa jijini Dar es Salaam.
  Mkuu huyo wa wilaya alifafanua kuwa mtoto huyo alinusurika kuozwa kwa nguvu, baada ya mlezi wake kutoa taarifa ofisini kwake.

  Alisema baba zake wakubwa wanataka kumuoza kwa mwanaume kijijini hapo ili zipatikane ng’ombe za kumwezesha kaka yake kuoa, kwani hadi sasa hajaoa kutokana kukosekana kwa ng’ombe.

  Aliongeza: “Kufuatia hali hiyo, nilimwagiza Kaimu Katibu Tarafa wa tarafa hiyo kufuatilia tukio hilo.”
  Hata hivyo, Isack, alisema kwa sasa hawezi kuchukua hatua dhidi ya watu hao, kwa sababu hakuna ushahidi wa kutosha wa kuwapeleka mahakamani, lakini alisema lazima wafike ofisini kwake ili waohojiwe kutoa maelezo.

  Kwa upande wake, Kaimu Afisa Tarafa ya Chamriho, Juma Mkami, alisema baada ya kufuatilia aligundua kilichoelezwa ni kweli, kwani baba zake wakubwa walimkatalia asirejee jijini Dar es Salaam kuendelea na masomo yake.
  Alisema wazazi hao walisema kuwa, wameshamwandalia mwanaume wa kumuoa kwa lengo la kupata mahari ili imwezeshe kaka yake kuoa.

  “Watuhumiwa walitaka kumkatalia mtoto huyo asirudi Dar es Salaam, nilitumia sauti ya serikali ya ukali kidogo ndipo wakanipatia na leo hii (jana) nimempeleka kwa DC ambaye amesema kesho asubuhi mlezi wake aende akamchukue,” alisema.

  Mkami aliongeza: “Na nimewaita hao baba zake wakubwa nao waje ili watoe maelezo kwa DC.”
  Alisema kuwa tayari jana alimkabidhi mtoto huyo kwa DC na kwamba mlezi wa mtoto huyo leo asubuhi ataitwa kukabidhiwa mtoto huyo ili arejee naye Dar es Salaam kuendelea na masomo.

  Aliongeza kuwa watuhumiwa hao pia wametakiwa leo asubuhi wafike ofisini kwa mkuu wa wilaya.
  Kwa mjibu wa Mkami, wakati wakimhoji mtoto huyo, alisema anataka shule na si kuolewa kama ndugu zake wanavyotaka na kwamba kwenye darasa lao lenye watoto zaidi ya 100, amekuwa akishika nafasi ya kwanza, ya pili na ya tatu kwenye mitihani.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Why, why, why?

  Why mutilate poor little innocent girls? Have you no heart?

  SMH in disgust.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tuna kazi ya ziada kuwanusuru watoto kutokana na mwendelezo wa mila zinazoendeleza biashara ya binadamu hata bila kujali umri wao. Huyo mwanaume wanayetaka kumwoza bila ridhaa yake na kabisa wakati huu angali mdogo hajui nini maana ya maisha ya mume na mke, inanishangaza kidogo, ingawa ndivyo mambo yanavyoendelea sehemu nyingi nchini kwenye mila na makabila mbalimbali ya jamii za wakulima na wafugaji.

  Nimeshuhudia watu wengi huwakimbizia na kuwaficha watoto wao mijini wakifanya kazi za nyumbani, na kisha huwaita waende kuwasalimia ikiwa ni hadaa ya kuwaita wakabidhiwe mabwana wakati mahari zilishalipwa. Watoto hawa hawana nyuma wala mbele, na nchi yetu haina sheria na mfumo wa kuwafunda watoto wapatwapo na mikasa kama hiyo kuwajulisha polisi na vyombo vingine vya kutetea haki zao. Kwa vyo vyote tunahitaji kujenga dhamira ya kuwafunza watoto hazi zao za msingi hadi wanapofikia umri wa ukubwa kisheria kuamua wanavyopenda badala ya kuamuliwa mume au mke wa kuishi naye wakati wangali wadogo na hawajakomaa kuweza kuhimili maisha ya ndoa.
   
 4. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Nimemuona yule bibi wa miaka 70 akisindikizwa na polisi hata kiswahili hafahamu..
   
 5. Jeji

  Jeji JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  inasikitisha sana kwa kweli. bibi apewe adhabu kali iwe fundisho kwa wengine.
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa!.

  Ungemwekea mdhamana jamani Bibi wa miaka 70.
   
 7. s

  sugi JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  wakeketaji wa siku hizi bwana..!hawana utaalamu wa kutosha,wanatakiwa waende shule
   
 8. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  hii ishu ya ukeketaji bado inatokea sana...too sad katoto ka watu kanapoteza maisha for a choice tat is not hers.....bibi itakuwa alikutana na mtoto mwenye haemophilia,hata huku hospital tukikutana nazo ni mbinde kustop hiyo bleeding
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mambo mengine hayaingii akilini. Ni ukatili uliopitiliza...
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  huyo bibi na hao ndugu waliompa idhini ya kumkeketa huyo mtoto wote wafungwe kifungo cha maisha.
   
 11. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0

  Kama wanamfunga watakuwa wanamwonea tu. Hizi mila zipo tangu wakoloni hawajaja na baadhi walikuwa wanakufa na wengine wanasalimika. Waelewane nae aache hiyo kazi then wamwachie.
   
Loading...