Mtoto Aangua Kilio Wakati wa Kuingizwa Kaburini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtoto Aangua Kilio Wakati wa Kuingizwa Kaburini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Aug 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]Mtoto mchanga wa kike wa nchini Brazili aliyetangazwa amefariki punde baada ya kuzaliwa aliangua kilio wakati anatumbukizwa ndani ya kaburi lakini alifariki baada ya kuokolewa na kufikishwa hospitali.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikuwa na ujauzito wa miezi saba alijifungua mapema hospitalini kabla ya muda wake.

  Lakini madaktari wa hospitali ya Santa Casa de Misericord katika mji wa Araxa walitoa taarifa muda mfupi baadae wakimwambia kuwa mtoto wa kike aliyejifungua alikuwa amefariki.

  Taarifa ya madaktari ilionyesha kuwa mtoto huyo alifariki wakati wa kuzaliwa.

  Wakati maandalizi ya mazishi yalipokamilika na maiti ya mtoto ilipokuwa ikiingizwa kaburini, mtoto huyo aliangua kilio hali iliyowashtua watu na kugundua kuwa mtoto huyo kumbe alikuwa hajafariki.

  Kichanga hicho kiliwahishwa kwenye hospitali nyingine tofauti na kulazwa kwenye chumba cha watu mahututi.

  Haukupita muda mrefu taarifa ilitolewa kwamba mtoto huyo amefariki dunia.

  "Amefariki dunia baada ya ogani zake muhimu kushindwa kufanya kazi kutokana na ukosefu wa oxygen kwenye damu", alisema msemaji wa hospitali aliyokuwa amelazwa mtoto huyo.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,056
  Likes Received: 6,504
  Trophy Points: 280
  huyo malaika alikosa hewa, kumbe na madaktari wa huko juu wapo vilaza pia.
   
 3. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ina maana kuwa mtoto alizaa mtoto?
   
 4. COMPLICATOR2011

  COMPLICATOR2011 JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Hao madakaktari wanafanya mambo kama serikali ya ccm hapa tz, plz wachukuliwe hatua mara moja.
   
 5. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tujadiliane yanayojiri tz umeme, mafuta, njaa nk ya majuu baadae
   
Loading...