Mto Zigi ni moja ya mito mashuhuri katika bonde la Pangani. Umuhimu wa mto huu pamoja na huduma ya kimazingira mto huu ndio chanzo pekee cha maji kwa Jiji la Tanga na vitongoji vyake.
Kwa sasa mto huu umeathirika kwa kiasi kikubwa sana. Kutokana na shughuli za kibinaadamu mto huu upo katika hali mbaya inayotishia uwepo wake. Uchimbaji haramu wa madini umetamalaki tena kwenye maeneo muhimu ya vyanzo vyake.
Ukienda kwa mfano Sakale, Nelusanga na hata Kihara mkuu unaweza kutoa machozi kwa kile utakacho kishuhudia. Kiufupi licha ya juhudi kubwa zinazofanywa na mhifadhi wa msitu wa asili Amani bado uharibifu umetamalaki.