nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
Na Mwandishi wetu - Mwanahalisi
MWAKA 2012 tuliouanza leo unabashiriwa kuwa mgumu zaidi katika medani ya kisiasa, hasa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.
Kwa mujibu wa viongozi wa dini, wanasiasa, wananchi na makundi ya kijamii wameweka wazi kuwa vita ya makundi iliyoshika kasi ndani ya chama hicho tawala inatarajiwa kuwa mbaya zaidi mwaka huu ambapo kitakuwa na uchaguzi wa chama.
Chaguzi za chama zinazotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu zinaelezwa ndizo zitakazotoa mwelekeo wa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2015.
Tayari baadhi ya makada wa chama hicho wanadaiwa kuanzisha mbinu za siasa za kuwachafua wale wanaoonekana kuwa tishio kwenye nafasi husika.
Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ni miongoni mwa wanasiasa wanaokabiliana na tishio la kungolewa kwenye nyadhifa za chama kwa kile kinachodaiwa anahusishwa na tuhuma mbalimbali zinazokiathiri chama.
Hata hivyo baadhi ya makada wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu, Wilson Mukama wameweka wazi kuwa vita ya urais wa mwaka 2015 ndiyo imezidisha mpasuko baina ya makada.
Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa hivi sasa kuna makundi makubwa mawili yanayovutana kutengeneza mtandao wa kufanikisha dhamira ya kukiongoza chama na hatimaye serikali.
Kundi moja linadaiwa kuwahusisha wanasiasa maarufu wakiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harisson Mwakyembe na wabunge ambao kwa nyakati tofauti walionekana kulivalia njuga suala ufisadi.
Kundi la pili ni lile linalohusishwa na Lowassa, ambaye amekuwa akitajwa mara kwa mara kutaka kuwania urais, kundi hili limekuwa likitaka vigogo wote wanaowahusisha wenzao kwa tuhuma za ufisadi bila kuwapo kwa ushahidi waadhibiwe.
Mnyukano wa makundi hayo pia unadaiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kulegalega kwa utendaji wa serikali, ambapo baadhi ya watendaji wake wanaingiwa na woga kutekeleza baadhi ya majukumu yao.
Kuathirika kwa utendaji wa serikali ndiko kumewafanya baadhi ya watu kutaka mawaziri na manaibu wao wasiwe wabunge ili kuboresha utendaji wa chama na serikali.
Sitta na Makinda
Spika wa Bunge, Anne Makinda, anadaiwa kutokuwa na uhusiano mzuri na Spika aliyemtangulia, Samuel Sitta, kiasi cha kumfanya awahamishe baadhi ya watendaji wa ofisi hiyo kwa madai wanahujumu utendaji wake.
Hata hivyo Makinda aliwahi kuweka wazi kuwa uhusiano wake na Sitta si mbaya bali kuna watu wanawafitinisha, hasa baada ya Sitta kuenguliwa kuwania kiti hicho mwaka 2010.
Wachambuzi wa masuala ya siasa wameweka wazi kuwa kiongozi huyo wa Bunge anapata wakati mgumu wa kuliongoza Bunge kwakuwa baadhi ya wabunge wanamtuhumu kukiendesha chombo hicho kwa upendeleo.
Kiongozi huyo hivi sasa anakabiliwa na shinikizo kubwa la kutakiwa kuachia madaraka yake kwa madai kuwa alikiuka utaratibu wa kisheria kwa kuamua kuongeza posho za wabunge kutoka sh 70,000 kwa siku hadi sh 200,000
Spika Makinda anadaiwa kumpokonya madaraka Rais Kikwete ambaye ndiye mwenye dhamana ya kuridhia ongezeko la posho hizo, kama ilivyowasilishwa kwake na Ofisi ya Bunge.
Kiongozi huyo wa Bunge pia inasemekana hana uhusiano mzuri na Katibu wa chombo hicho, Dk. Thomas Kashililah, ambaye alisema posho za Bunge hazijapanda na baada ya siku mbili Makinda alisema zimepanda na kutaja kuwa zilikwisha kuanza kulipwa katika vikao vya Novemba mwaka jana.
Kauli ya CCM
Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kuwa chama hicho hakitegemei kupata mtikisiko kutokana na chaguzi hizo kama baadhi ya watu wanavyofikiri.
Nape alisema taratibu na kanuni za chama ndizo zitakazotumika kwenye chaguzi hizo na chama hicho kina uzoefu wa kufanya chaguzi nyingi na kubwa.
CCM ni chama imara, tunamshukuru Mungu kwa kuingia mwaka 2012, wanaofikiri tutakuwa na wakati mgumu wanajidanganya sisi tuna mfumo mzuri wa kuwajibishana.
Kila jambo linalotokea ndani ya chama chetu tunalimaliza kulingana na taratibu tulizojiwekea, wanaofikiri wao wana nguvu kuliko chama wanajidanganya, alisema.
Dk. Slaa
Juzi Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema kuwa nchi inayumba kutokana na rais kushindwa kutatua matatizo yanayowakabili wananchi likiwemo la umasikini.
Aliweka wazi kuwa kutofautina kwa mawaziri hadharani ni dalili ya udhaifu na kutokuwapo uwajibikaji ndani ya serikali inayoongozwa na CCM.
Viongozi wa dini
Kwa nyakati tofauti mwaka 2011 viongozi wa dini walitoa wakati mgumu kwa utawala wa Rais Kikwete kutokana na msimamo wao wa kukosoa mambo kila walipoona yanakwenda kombo.
Utaratibu wao huo uliwafanya baadhi ya watu kuwatuhumu kuwa wanauchukia utawala wa Rais Kikwete na kuvipendelea vyama vya upinzani.