Mtikisiko CCM 2012: Mbinu za kumg'oa Lowassa zakamilika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtikisiko CCM 2012: Mbinu za kumg'oa Lowassa zakamilika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jan 1, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jan 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Mwandishi wetu - Mwanahalisi

  MWAKA 2012 tuliouanza leo unabashiriwa kuwa mgumu zaidi katika medani ya kisiasa, hasa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Daima Jumapili limedokezwa.


  Kwa mujibu wa viongozi wa dini, wanasiasa, wananchi na makundi ya kijamii wameweka wazi kuwa vita ya makundi iliyoshika kasi ndani ya chama hicho tawala inatarajiwa kuwa mbaya zaidi mwaka huu ambapo kitakuwa na uchaguzi wa chama.

  Chaguzi za chama zinazotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu zinaelezwa ndizo zitakazotoa mwelekeo wa mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2015.  Tayari baadhi ya makada wa chama hicho wanadaiwa kuanzisha mbinu za siasa za kuwachafua wale wanaoonekana kuwa tishio kwenye nafasi husika.  Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, ni miongoni mwa wanasiasa wanaokabiliana na tishio la kung’olewa kwenye nyadhifa za chama kwa kile kinachodaiwa anahusishwa na tuhuma mbalimbali zinazokiathiri chama.  Hata hivyo baadhi ya makada wa chama hicho akiwamo Katibu Mkuu, Wilson Mukama wameweka wazi kuwa vita ya urais wa mwaka 2015 ndiyo imezidisha mpasuko baina ya makada.  Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kuwa hivi sasa kuna makundi makubwa mawili yanayovutana kutengeneza mtandao wa kufanikisha dhamira ya kukiongoza chama na hatimaye serikali.  Kundi moja linadaiwa kuwahusisha wanasiasa maarufu wakiwamo Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harisson Mwakyembe na wabunge ambao kwa nyakati tofauti walionekana kulivalia njuga suala ufisadi.  Kundi la pili ni lile linalohusishwa na Lowassa, ambaye amekuwa akitajwa mara kwa mara kutaka kuwania urais, kundi hili limekuwa likitaka vigogo wote wanaowahusisha wenzao kwa tuhuma za ufisadi bila kuwapo kwa ushahidi waadhibiwe.  Mnyukano wa makundi hayo pia unadaiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa kulegalega kwa utendaji wa serikali, ambapo baadhi ya watendaji wake wanaingiwa na woga kutekeleza baadhi ya majukumu yao.  Kuathirika kwa utendaji wa serikali ndiko kumewafanya baadhi ya watu kutaka mawaziri na manaibu wao wasiwe wabunge ili kuboresha utendaji wa chama na serikali.


  Sitta na Makinda
  Spika wa Bunge, Anne Makinda, anadaiwa kutokuwa na uhusiano mzuri na Spika aliyemtangulia, Samuel Sitta, kiasi cha kumfanya awahamishe baadhi ya watendaji wa ofisi hiyo kwa madai wanahujumu utendaji wake.


  Hata hivyo Makinda aliwahi kuweka wazi kuwa uhusiano wake na Sitta si mbaya bali kuna watu wanawafitinisha, hasa baada ya Sitta kuenguliwa kuwania kiti hicho mwaka 2010.  Wachambuzi wa masuala ya siasa wameweka wazi kuwa kiongozi huyo wa Bunge anapata wakati mgumu wa kuliongoza Bunge kwakuwa baadhi ya wabunge wanamtuhumu kukiendesha chombo hicho kwa upendeleo.


  Kiongozi huyo hivi sasa anakabiliwa na shinikizo kubwa la kutakiwa kuachia madaraka yake kwa madai kuwa alikiuka utaratibu wa kisheria kwa kuamua kuongeza posho za wabunge kutoka sh 70,000 kwa siku hadi sh 200,000

  Spika Makinda anadaiwa kumpokonya madaraka Rais Kikwete ambaye ndiye mwenye dhamana ya kuridhia ongezeko la posho hizo, kama ilivyowasilishwa kwake na Ofisi ya Bunge.  Kiongozi huyo wa Bunge pia inasemekana hana uhusiano mzuri na Katibu wa chombo hicho, Dk. Thomas Kashililah, ambaye alisema posho za Bunge hazijapanda na baada ya siku mbili Makinda alisema zimepanda na kutaja kuwa zilikwisha kuanza kulipwa katika vikao vya Novemba mwaka jana.


  Kauli ya CCM
  Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema kuwa chama hicho hakitegemei kupata mtikisiko kutokana na chaguzi hizo kama baadhi ya watu wanavyofikiri.


  Nape alisema taratibu na kanuni za chama ndizo zitakazotumika kwenye chaguzi hizo na chama hicho kina uzoefu wa kufanya chaguzi nyingi na kubwa.  “CCM ni chama imara, tunamshukuru Mungu kwa kuingia mwaka 2012, wanaofikiri tutakuwa na wakati mgumu wanajidanganya sisi tuna mfumo mzuri wa kuwajibishana.”

  “Kila jambo linalotokea ndani ya chama chetu tunalimaliza kulingana na taratibu tulizojiwekea, wanaofikiri wao wana nguvu kuliko chama wanajidanganya,” alisema.


  Dk. Slaa
  Juzi Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema kuwa nchi inayumba kutokana na rais kushindwa kutatua matatizo yanayowakabili wananchi likiwemo la umasikini.

  Aliweka wazi kuwa kutofautina kwa mawaziri hadharani ni dalili ya udhaifu na kutokuwapo uwajibikaji ndani ya serikali inayoongozwa na CCM.

  Viongozi wa dini
  Kwa nyakati tofauti mwaka 2011 viongozi wa dini walitoa wakati mgumu kwa utawala wa Rais Kikwete kutokana na msimamo wao wa kukosoa mambo kila walipoona yanakwenda kombo.


  Utaratibu wao huo uliwafanya baadhi ya watu kuwatuhumu kuwa wanauchukia utawala wa Rais Kikwete na kuvipendelea vyama vya upinzani.
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  'UVUAJI GAMBA' NA 'UUNDAJA KATIBA MPYA YA WNANCHI' NDIO MAMBO MAZITO MAWILI KATI YA MENGI YATAKAYOTOAMUA CCM KUZIKWA KIMOJA AU KUENDELEA KUISHI KWA MATUMAINI

  Kati ya mambo mazito katika mwaka huu wa 2012 ambayo CCM kisiposhughulikia kwa haraka na umakini mkubwa basi ndivyo vitakvyokua lango la chama hiki kuelekea kaburini kisiasa ni pamoja na mambo mawili haya; (1) kurudisha swala la uundaji katiba mpya kwa wananchi wenyewe kuisimamia na lile swala la (2) pili la kujivua gamba.

  Endapo CCM itapata viongozi wake wapya tangu sasa BILA KWANZA KUJIVUA GAMBA, kwa wapiga kura tafsiri yake halisi itakua ni kwamba tayari GAMBA JIPYA litakua limezaliwa mgongoni mwake hiyo sfu mpya ya uongozi tayari kwa kuendeleza mradi wao ule ule wa UFISADI mpaka kufa na hivyo kukifanya chama hiki kisiweze KUCHAGULIKA hata kwa kiwango cha kuwa chama kikuu cha upinzani bungeni 2015.

  Na hilo ndilo jambo la msingi zaidi kisiasa nchini ambacho wadadisi wa mambo ya kisiasa nchini hivi sasa wamekodolea macho zaidi.

  Hakika kuna hatari kubwa zaidi kwamba CCM huenda kikakimbiwa na wanachama wengi zaidi kwa kitendo cha kushindwa kujivua gamba kuliko hata ile hatari wanayoihisi kwa kutekeleza jambo hili zito kitaifa kuchagua kujitenga na Gamba au kuendelea kula nayo yamini.
   
 3. M

  Mathewz Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imetulia hiyoo mkuu:A S 465:
   
 4. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nawashauri CCM wasimguse EL hata kidogo.
   
 5. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Halafu mleta mada edit pale juu kwani si mwandishi wa MwanaHalisi bali ni mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima
   
 6. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Naam, kwa wale wenzetu wenye kuchelewa saaaaaana kung'amuaa mambo, nasema kuna kimbunga kizito zaidi ya ile ya Tsunami inakuja CCM kunakoelekea 2015.

  Tahadhari zote tulizitoa tangu mwaka wa juzi lakini hatukusikilizwa; katika hili hakuna njia yoyote ya mkato itakayokua salama na yenye baraka kwa CCM kutafuta kule KUJINASUA!!!!!!!!! Kwa kuwa si mawimbi tu ya bahari la ufisadi na katiba ya watawala zitakazotafuta kukizamisha CCM, upepo wa kutoka Mashariki ya Mbali ukijichanganya vema na ardhi tambalale ya umasikini wa kutupwa nchini kwa hisani ya UFISADI wa kitaasisi, hali ni tete zaidi mwaka huu na kuendelea.

  ... and that is a fact anywa!!
   
 7. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #7
  Jan 2, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  uangalifu mkubwa unahitajika vinginevyo kitakuwa chama chama cha upinzani hata kabla ya uchaguzi mkuu kwa tayari zote zinaonekana
   
 8. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu kwenye nyekundu hapo, tutunziane heshima mkuu.
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kumbe Gamba tayari lilishazaliwa hata hivo? Mkuu heshima mbeeeeele kama tai. Hebu zingatia hayoyanayosemwa hapo juu si matani hata kidogo tena.

   
 10. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Muda utatuambia.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ukiona kujivua gamba ni kugumu sana basi kajaribu kulienzi zaidi na uje uone jinsi gani CCM kitakavyoanza kukimbiwa na Makada pamoja na wanachama wa kawaida kwa makundi yasio na idadi maalum.

  Hoja za Uvuaji gamba na Katiba Mpya ya wananchi kamwe hakuna njia yoyote ya MKATO itakayokua salama na kuleta neema kwa makundi yote pinzani ndani ya CCM.

  Uchaguzi ujao ndani ya CCM na kipindi baada ya hapo mpaka kufikia 2015 ni kimbembe kitupu;
  it will be a Make or Break Election for all presidential aspirants in the party.

  Na hadi hivi sasa ni mambo mazito mno yanaendelea nyuma ya pazia kwa kila kundi. Ajabu ni kwamba Ikulu yetu Magogoni ndio yenye wasi wasi mwingi kuliko kundi lingine lolote ndani ya chama hicho hadi sasa kwa kuwa siri zake zote ziko nje kweupe.
   
 12. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kwa nini wasimguse?
   
 13. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  THE POLITICAL CHASEBOARD TANZANIA 2012 - 2015:
  TAFSIRI YA TAARIFA NYETI NYUMA YA PAZIA NA MWELEKEO KISIASA KWA CCM NCHINI


  Amillion dollar question mjumbe Okada.

  Ukweli wa mambo ni kwamba kwa CCM juu ya jambo hili nyeti mno hakika kote kote kuna gharama tena kubwa mno; kwa upande wa kwanza ni kwamba MAFISADI kuvuliwa gamba ni kwamba siri yooote itatoka rasmi nje hasa juu ya biashara kichaa ya Richmond / Dowans na ukwapwaji wa fedha zetu kule benki kuu.

  Kwa upande wa pili ni kwamba endapo hii nadharia ya 'FULANI USIMGUSE' kweli utazingatiwa basi sura halisi ni kwamba CCM itabaki a minority political party madarakani tangu mwaka huu kwa kuona wabunge kibao wakijiuzulu nyadhifa zao kwa kupinga hatua hiyo na kujaribu kusalimisha ubunge wao kwa njia ya kujiweka mbali na Chama cha Kifisadi.

  Kitendo hiki kitafuatwa kwa karibu sana na wanachama wa kawaida CCM nao kusema yametosha (kwamba CCM si mama zao wala baba zao) na kutimkia vyama vingine kwa wingi.

  Hata hivyo, wabunge watakaojiuzulu nyadhifa zao watajitokeza tena kuomba nyadhifa hivo kwa mafanikio makubwa chini ya udhamini wa vyama tofauti na CCM.

  Na kama hilo halitoshi, ni mara baada ya uchaguzi ndani ya CCM mapema mwaka huu ambapo tutashuhudia vyama vipya kusajiliwa na vile vingine vidogo vidogo vilivyozoeleka kuwika tu ndani ya brief-case za wamiliki wao binafsi safari hii vitapata uhai mpya kabisaaa!!


   
 14. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  CCM doomsday is more than imminent at the backdrops of a shake-off from mega-corruption scandles and the dilemma of mainstreaming the ordinary citizens as the determining architects of the new constitution.

  It gonna be a do or die for the once formidable independence but now frail political party embroiled in its own undoing in pursuit of inconsistent decision streams that are deeply contradictory to her very founding policies in the early '60s.

  Yes, a do or die ...!!!!!!!!!
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,779
  Trophy Points: 280
  hawa wanataka kuuza magazeti tu hawa .
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Tunajua vizuri sana kwamba Lowassa kisha wanunua viongozi wengi wa dini kwa hiyo kila yanayofanyika nchini yamepangwa sii bure.
   
 17. A

  Ame JF-Expert Member

  #17
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Say it again......

  Acha sisi tuingie katika nchi ya ahadi bwana hatuwezi kukaa jangwani maisha yetu yote hata kama miguu yetu inakuwa pamoja na viatu; nguo hazichaniki na wala hatuna haja ya kuwa na magala maana mana kila siku asubuhi inadondoka tunataka maziwa, asali sasa na divai fresh kutoka katika mashamba ambayo wenye nchi wametulimia kwa nguvu zao; sisi ni kuvuna tu na kula raha Mungu atupe nini?

  Wengi wanaona bahari ya Shamu mbele wanajitahidi kupiga kelele kuomba msaada hawajui wokovu wao ni karibu sasa kuliko wakati mwingine wowote. Adui naye kwa upande wa pili anashangilia kuwa ndiyo anatukamata vizuri lakini kuna ishara moja adui ameiona yakuwa magurudumu ya magari ya vita haya kimbii kwa speed zake madereva wanakanyaga moto mpaka mwisho lakini ni sauti tu ndo zinakuwa kubwa lakini speed ndiyo kwanza 4okm/hr........
   
 18. t

  thatha JF-Expert Member

  #18
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  wakubwa acheni ndoto za mchana fanyeni kazi kujipatia rizki.ivi who is lowasa,mbona mnamuabudu ivo? kwanini msimpe nafasi huko chadema kama mnamuhitaji?inaonekana munamuogopa kweli kweli.kwa taarifa yenu ccm haitayumba kwa haya majungu yenu sana sana itaimarika na ndio itakuwa aibu kwenu...........

  chadema ndio itasambaratika kwa kukosa sera baada ya kuonekana ni chama maslahi na ndumila kuwili wa hoja,hakina msimamo thabiti.mfano suala la posho.
   
 19. t

  thatha JF-Expert Member

  #19
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  hakuna chama cha upinzani kilicho imara hapa tanzania,vyote vina matatizo yanayokaribiana,ukabila na udini mfano chadema,kukandamiza demokrasia mf nccr na cuf,kufukuza wanachama na viongozi wake mf chadema,NCCR na TLP.Watanzania hawadanganyiki na vyama uchwara vya kaskazini
   
 20. FREDRICK KIMARO

  FREDRICK KIMARO Member

  #20
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kukumbatia mafisadi ndiko kumewaponza na bado watakiona.
   
Loading...