Godwin M Mroso
Member
- May 25, 2013
- 90
- 32
Huyu jamaa watu wengi ambao sio makini wanamchukulia kama mtu ambaye hayupo sawa hususani kwa
jinsi anavyoongazo kanisa lake, jinsi anvyofanya siasa zake, na hata maisha yake binafsi kwa ujumla.
Hata serikali inamchukulia kama mtu mkorofi na ambaye anapenda sana kesi.
Mchungaji huyu alishawahi kufungwa jela mwaka mmoja kwa kumkashifu baba wa taifa.
Napenda kumpongeza mchungaji mtilkila kwa ujasiri wake na uwazi wake, mchungaji mtikila alikuwa anaipigania Serikali ya Tanganyika kwa muda mrefu sana, Tumemshuhudia mara nyingi kwenye maazimisho ya uhuru wa Tanzani dec 9 kila mwaka jinsi anavyokorofishana na watu wa usalama pale alipokuwa anataka kuingia uwanja wa Taifa na bendera ya Tanganyika ambao wao walikuwa wanamzuia, vijana wengi hata wazee ambao walikuwa hawaijui bendera ya tanganyika walikuwa wanaionea nyumbani kwake ikipepea.
Mchungaji Mtikila ameshaipeleka Mahakamani Serikali kuhusiana na suala la mgombea binafsi ambapo Mahakama Kuu ilimpa ushindi dhidi ya Serikali lakini Serikali ikakata refaa Mahakama ya Rufani na kushinda.
Tume ya Katiba imetupatia Rasimu ya Katiba ambayo pamoja na masuala mengine imetuletea hoja ya kuundwa kwa Taifa la Tanganyika na pia kuwa na wagombea binafsi. Madai ambayo Mchungaji Mtikila alikuwa anayapigania sana na kwa uwazi hadi kugombana na dola.
Safi sana mchungaji Mtikila , wewe ni mfano wa kuigwa.