Mtikila akamatwa kwa uchochezi

Namkubali Mtikila, ukitaka kujua umuhumu wake kwa jamii nenda pale Rugakingira kituo cha sheria Kijitonyama. uone wanavy omsifia kuwa ni mtu aliyeleta mageuzi ya kisheria nchi hii japo yeye si mwanasheria.
Kwa wale wanaofuatilia siasa zake Mtikila alikuwa sumu hata utawala wa Mwinyi na swala la OIC.ndo alilipinga vikali, na kwake ikulu ilikuwa kama sebuleni.

Ndo huyu aliyeingiza misamiati mipay katika lugha yetu, neno kama "MLALA HOI" tungelipata wapi kama siyo Mtikila, neno kama "Gabachori" japo halikuvuma sana, mwanzilishai ni yeye aliwa ana nadi sera zake za "SAA YA UKOMBOZI NI SASA".

Mtikila akiibua kitu anakuwa amefanya research na anajua mwanzo na mwisho wake, na ndo maana kesi zake nyingi hushinda.

Tatizo la huyu mtu ni kushindwa kujimeneji mwenyewe, angekuwa mkombozi wa kweli ktkt nchi hii.
Mkuu, kama sikosei, saa ya ukombozi ni sasa ilikua katika kitabu cha kuli tulichotumia kwenye fasihi O-level starring akiwa Rashid Majaliwa... yeye alikopi na kupesti
 
Kama utaniamsha usingizini na kuniuliza mpinzani wa kweli Tanzania basi bila hata kufikiri nitakujibu Mtikila,yeye alitakiwa kuukubali muungano ili chama alichokianzisha kisajiliwe lakini alikataa kwani anaamini huu muungano unamapungufu sehemu fulani.Hivyo kama angekuwa ni mtu wa kutaka madaraka naamini angekubali tuu suala la muungano ili chama alichokianzisha kisajiliwe na bila shaka angekuwa kiongozi mwanzilishi.NAMPA HONGERA TUNATAKA WAPINZANI WA AINA HII.
 
Mimi kwa upande mwingine, Mtikila huwa anaongea facts. Achilia mbali swala la yeye kuwa na kesi nyingi. Serikali ya JK imekuwa ikituyeyusha sana. Nchi inayumba, jamaaa anacheka cheka tu, nothing is done, mafisadi wanasamehewa, udini nao unaongezeka kwa kasi, usalama wa raia hakuna tena, watu wanakabwa mchana peupe tena hadi mbele ya vituo vya polisi, kiwango cha elimu kimeshuka sana hali population inaongezeka, huduma za hospitali hakuna huku Rais anatembelea expensive cars everyday (kila siku msafara wake unaenda kwa fashion, leo ni motorcade ya BMWs tu, kesho ni Benz tupu, kesho kutwa ni VX/V8 tupu). We need people like Mtikila ambao wana comfo la kuibana mbavu serikali.

Ila Mtikila sasa akomae na facts tupu, apunguze kesi za kizushi.
 
KUNA taarifa ambazo tunazifanyia kazi kwamba Mtikila yuko mikononi mwa polisi Central amekutwa na vipeperushi vinavyodaiwa kumshughulikia KIKWETE lakini kwa kutumia udini. Amekatwa leo asubuhi. Inabidi apekuliwe.

Kwa taarifa za magazeti asubuhi ya leo ni kwmba polisi walienda nyumbani kwake kutafuta (search) waraka ambao inasemekana Mch Mtikila ameusambaza kwa waumini/wananchi. Hata hivyo hawakufanikiwa kupata nakala ya waraka huo. Katika waraka huo (mimi sijauona!) inadaiwa kuwa Mch Mtikila pamoja na mambo mengine 'anawachochea' wananchi kutomchagua JK tena kwa sababu ni 'mdini'!
 
Do we not have freedom of expression in Tanzania? It is not against the law to have pamphlets. It is also not against the law to express an opinion against anyone.

It is political brutality for Kikwete to arrest Mtikila for being in possession of pamphlets.

Kama Mtikila ana maoni kwamba Kikwete ni mdini, kwa nini aogope kusema hivyo?

Mtikila ni Mwanasiasa jasiri. Hizo porojo kwamba alihongwa na Rostam Aziz ni za kupuuza.

Not yet UHURU.
 
Hizo habari za kukamatwa mchungaji Mtikila ni za ukweli, lakini taarifa zisizo rasimi ni kwamba aliwaambia polisi kuwa huo waraka ameishausambaza kwa wananchi na kwa bahati mbaya nakala zilishaisha vinginevyo angewapatia polisi na wao nakala.

Wana JF tunawaomba yule aliyebahatika kuuona atuwekee kwenye JF blog tuusome,asante in advance
 
Kosa la "uchochezi" likoje hasa? Nini definition ya "uchochezi"? Kama wakoloni wangetumia definition yetu ya uchochezi tungejinyakulia uhuru kweli?

Ni lini viongozi wa CCM wataacha kuwakamatakamata hovyo wananchi?

How do we protect ourselves from the whims of our leaders?
 
Mtikila na Mrema wanabaki kuwa watu pekee katika upinzani ambao matunda ya kazi yao yanaonekana.....!

VITUO VYA POLISI, ZANZIBAR KWA PASPOTI, MGOMBEA BINAFSI, MISAMIATI MIPYA, KUBADILISHWA KATIBA na mengineyo mengi tu.....!
 
Do we not have freedom of expression in Tanzania? It is not against the law to have pamphlets. It is also not against the law to express an opinion against anyone.

It is political brutality for Kikwete to arrest Mtikila for being in possession of pamphlets.

Kama Mtikila ana maoni kwamba Kikwete ni mdini, kwa nini aogope kusema hivyo?

Mtikila ni Mwanasiasa jasiri. Hizo porojo kwamba alihongwa na Rostam Aziz ni za kupuuza.

Not yet UHURU.

Kama kawaida polisi Tanzania ndiyo inavyoperate, na make no mistake unaweza kufikiri wametumwa I doubt ila ni kujipendekeza tu,............kukurupuka na sometimes kuweweseka.

Well said mkuu, nadhani humu watu wamesahau au they were too young or negligent kutambua vuguvugu la demokrasia lililoanzishwa na Mtikila in late 80's na early 90's. Mtikila anakamata credits karibu zoote za kusensitize watanzania kuhusu nini maana ya vyama vingi, kutambua kwamba serikali yao inafisadi left, right and centre. Hoja ya mgombea binafsi ni kipimo tosha kuonyesha huyu jamaa ni mtu wa namna gani. Ni one of the few Tanzanians if not alone kuishinda serikali ktk kesi ya kikatiba.

Kama watu mna kumbukumbu vizuri in 1995 Mtikila alipoulizwa kuhusu umaarufu na possibility ya Mrema kuwa rais alitamka bayana kwamba haiwezekani mpaka katiba ibadilishwe na kuwe na tume huru ya uchaguzi something wapinzania wengine wameanza kuizungumzia in 2008.

Mtikila pia aliwahi kufukuzwa shule kwa kukataa kuwa mwanachama wa TANU in the so called youth league pale Malangali sec. school.

Funny enaf na kama kawaida tutazisikia sifa kem kem za mtikila , God forbid let's say akiwa RIP.

Anywayz mwisho wa siku wataumbuka tu!!!!!!
 
In tanzania tuna hali mbaya sana ya kutopenda kuambiwa tunachotaka.... this has lead to hii tabia ya kubana freedom of expression kwa watu wenye haki hiyo.. Mtikila ni mtu wa pekee kwa kuweza kuweka hoja zake na kuchukua muda ku-challenge vile anavyoamini

Mapolisi watashindwa, na haki na usawa vitashinda.. mtikila is just a vehicle
 
Mimi namkubali sana Mtikila, na wadanganyika wengi wameshindwa kumwelewa kwa kuwa si waelewa wa mapinduzi ya kweli ya nchi. Mwanasiasa yeyote mahiri wa upinzani ni lazima aandamwe kwa kesi nyingi za kubambikizwa, kwani watawala kama ccm kamwe hawawezi kuvumilia kuvuliwa nguo. Natamani kuuona huo waraka kwani najua Mtikila sio mtu wa kukurupuka kama wengi wanavyodhani, ni mtu wa facts. Inawezekana kweli mahali fulani kama binadamu akavutwa na vipesa vya ccm, lakini kwa ujumla wake yeye ndiye anayeinyima serikali ya Kikwete usingizi.

BRAVO MTIKILA SAA YA UKOMBOZI NI SASA.
 
Mkuu, kama sikosei, saa ya ukombozi ni sasa ilikua katika kitabu cha kuli tulichotumia kwenye fasihi O-level starring akiwa Rashid Majaliwa... yeye alikopi na kupesti

Katika riwaya ya KULI mstari maarufu ni 'yana mwisho haya' hiyo saa ya ukombozi ni sasa ni kwenye vitabu vya Will Gamba.
 
Hizo habari za kukamatwa mchungaji Mtikila ni za ukweli, lakini taarifa zisizo rasimi ni kwamba aliwaambia polisi kuwa huo waraka ameishausambaza kwa wananchi na kwa bahati mbaya nakala zilishaisha vinginevyo angewapatia polisi na wao nakala.

Wana JF tunawaomba yule aliyebahatika kuuona atuwekee kwenye JF blog tuusome,asante in advance

i like this,the guy(rev. mtikila) is very smart and strong
very few people can stand up and face this corrupt government .
 
Kwa taarifa za magazeti asubuhi ya leo ni kwmba polisi walienda nyumbani kwake kutafuta (search) waraka ambao inasemekana Mch Mtikila ameusambaza kwa waumini/wananchi. Hata hivyo hawakufanikiwa kupata nakala ya waraka huo. Katika waraka huo (mimi sijauona!) inadaiwa kuwa Mch Mtikila pamoja na mambo mengine 'anawachochea' wananchi kutomchagua JK tena kwa sababu ni 'mdini'!

mh haya makosa mengine!kwani kuwaambia watu wasimchague kikwete nalo kosa?udini, what is udini?mbona watu wengi tu wameitwa wadini,au one law for kikwete then the other for mtikila and the likes
i wish watu kama mtikila wangekuwa 10 tu tanzania hii ccm na vibaraka wake wangenyooka.
 
Kwa taarifa za magazeti asubuhi ya leo ni kwmba polisi walienda nyumbani kwake kutafuta (search) waraka ambao inasemekana Mch Mtikila ameusambaza kwa waumini/wananchi. Hata hivyo hawakufanikiwa kupata nakala ya waraka huo. Katika waraka huo (mimi sijauona!) inadaiwa kuwa Mch Mtikila pamoja na mambo mengine 'anawachochea' wananchi kutomchagua JK tena kwa sababu ni 'mdini'!


hata mie ningekuwa na muda ningesaidiana nae kushinikiza wananchi kutokumchagua Kikwete kwa sababu sijaona alichofanya mpaka sasa
 
Kwa Mtikila kujihusisha na mambo ambayo wengine tunaamini ni mwiko kwake si ajabu. Kama kukamatwa mara nyingi, kufikishwa kwa Pilato mara kadhaa na wala hivyo vyote havijamfanya aache kueleza kila ambacho mwenyewe anaamini ni ukweli. Nadhani angefaa kuwa mwana jamiiforums aliyetukuka maana amethubutu kwa muda mrefu kujieleza peupe bila kificho - where we dare to talk openly!. Siku zilizopita aliwahi kueleza mazito zaidi kama nilivyowahi kuonjeshwa hapa chini:
=============================================================================
IJUE CCM MAFIA​
Mzalendo Stan Katabalo amepoteza uhai katika kumtetea mama yetu Tanganyika, alipolipua uchi wa CCM‑MAFIA wa "ACCOR" na "TAHI", kashfa za kutisha zilizopelekea mpaka kuuawa kwa shirika la WALALAHOI la UTALII kwa ajili ya mlo wa wazee wa MAFIA. Katabalo alilikalia rohoni tena genge hili, katika kuliacha uchi katika LOLIONDOGATE, mpaka akapewa onyo la kuuawa, kwa simu, eti
asiguse machafu hayo ya CCM‑MAFIA!
Katabalo amepata pigo la mauti akiwa na bomu la INDOL mkononi, ambalo limewapa "wazee" wa CCM‑MAFIA mpaka na majumba ya fahari huko Afrika Kusini! Dhambi ina nguvu kuliko haki ya Mwenyezi Mungu? La hasha! Genge la CCM‑MAFIA ni binadamu wa damu, nyama na mifupa. Damu ya Mpendwa wa Mungu Stan Katabalo inawalilia mbinguni, na Mungu asema wazi kwamba kipimo kile kile walichompimia hayati Katabalo ndicho watakachopimiwa na wao, saa wasioijua wao. Wapendwa wetu Charles Kabeho na Wilfred Mwabulambo sasa hawapo kazini kwa sababu ya maradhi yatokayo mikononi mwa CCM‑MAFIA, kwa utekelezaji wake wa MAAZIMIO YA ABUJA. Itawalazimu hawa kupata kinga na tiba ya Nguvu za Mungu kwa neema kwa njia ya imani.
Kifo cha Mheshimiwa Mbano, Mbunge wa Kigoma ni jibu la herufi kubwa la CCM‑MAFIA kwa kufunuliwa machafu ya "mzee" wa ndani wa Genge hili, ambaye nafasi yake katika "mafia" alijipatia kwa kuwa tegemeo la genge hilo kwa upande wa nguvu za giza. Mzindakaya amefikia cheo cha juu cha KUTOKOSEA katika CCM‑MAFIA, ndiyo maana hata baada ya uchafu wake kumwagwa bungeni, alizungumzia kukubali kuhamishwa, la kufukuzwa halipo. Huyu ndiye aliyehusika na yale "mauaji ya shappervile" ya Kilombero, lakini alihamishwa tu. Ndugu yetu Mbano hakuwa peke yake, hivyo wazalendo wenzake pia wanakabiliwa na kiu ya damu ya genge la CCM‑MAFIA. Ulinzi wa Mungu uwe juu yao, Amina.
Madhambi ya genge la CCM‑MAFIA ni ya kutisha na ni mengi. Taarifa za ndani zinathibitisha kuwa idara ya " Maazimio ya Abuja" inao mlolongo wa wakubwa ambao wametakiwa kuondolewa duniani, pamoja na wale wanaothubutu kuleta pingamizi katika uporaji wa "wazee" na sindiketi zao za Madawa ya Kulevya. Lakini kwa wale wote wenye wito wa kuikomboa Tanganyika na kuwaokoa WALALAHOI na vizazi vyetu vyote vijavyo, nawatia moyo kuwa mwisho wa CCM‑ MAFIA umewadia, na Mkono wa Mungu umenyooshwa juu yao.
Sasa kuliko wote walio katika orodha ya kupoteza uhai, kila mtu ameelekeza jicho lake kwa Mchungaji Christopher Mtikila, mkombozi wa WALALAHOI na jemedari mkuu wa Operasheni "OKOA MAMA TANGANYIKA". Huyu ndiye adui mkuu wa genge la CCM‑MAFIA. Mchungaji Mtikila ni mwiba wa moto mkali sana katika roho za genge hili, hasa kwa vile kutokana na ahadi ya Mwenyezi Mungu, kila silaha itakayofanyika juu yake haitafanikiwa, hata akinywa kitu cha kufisha hakitamdhuru kabisa, na kwamba kila ulimi utakaoinuka juu yake katika hukumu atahukumiwa kuwa mkosa.
Seif Shariff Hamad ni mmoja katika wale ambao kufuatana na mwana "mafia" Salmini Amour, anacho kitanzi cha CCM‑MAFIA shingoni tayari. Safari zake zote za nje na ndani zina mitego ya kila aina. Kunatafutwa uwezekano wa kupewa watumishi na hata "wafuasi" watakaothamini kiasi chochote cha fedha kuliko damu ya Hamad ili utaratibu wa kumshusha kimyani ufanikiwe. Hii ndiyo CCM‑MAFIA!
Licha ya ubeberu wote aliofanyiwa Mchungaji Mtikila na CCM‑ MAFIA, ikiwa ni pamoja na kufungwa jela, kutupwa mara kwa mara katika Magereza ya mahabusu, kutiwa mbaroni na polisi bila sababu, na mikiki mingine mingi, nguvu yake ya ukombozi iko pale pale na huzidi siku kwa siku. Mikakati yote ya rushwa, vitisho na mauaji imeshindwa kupata nafasi kwa Mchungaji Mtikila. Lakini mwaka 1988 kulikuwapo mpango kabambe wa kumwua, lakini Mungu akawa ngao yake. Mzalendo Abdalla Salum Yolero, kada wetu wa Dodoma alikataa hongo la CCM‑MAFIA la shilingi milioni 50 ili amwekee sumu "spesheli" inayoua polepole, ambayo bila shaka ndiyo iliyowamaliza wapendwa wetu Rutihinda, Kibona na wengine.
WALALAHOI karibu watashinda na Mungu yuko upande wao. CCM‑ MAFIA ni wanadamu wa damu, nyama na mifupa tu. Wamateketeza wenzao mpaka wameloa damu inayowalilia hata mbele za Mungu usiku na mchana. Kufuatana na Neno la Mungu na hata historia, huu ndio mwisho wa genge la CCM‑MAFIA. Watanganyika wamejifunza kwa uchungu sana ushetani wa CCM, na kwamba Tanganyika yao mpya inahitaji fikra mpya zisizo hata na harufu ya damu ya CCM‑MAFIA.

SAA YA UKOMBOZI NI SASA!
=========================================================================


Dawa ya mjinga ni kuumia
 
Huyu mtumishi mwenzangu wa Mungu hivi hadi kurudi kwa baba atakuwa amekamatwa mara ngapi? But the guy is in most cases not only right but also objective. Sema tu anaonakana kama mpiganaji asiyekuwa na silaha a sole fighter!
 
Back
Top Bottom