Mtihani wa kwanza Somalia katika miaka 25

Mtihani wa kwanza Somalia katika miaka 25

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,569
Reaction score
53,583
150616132047_mtihani_wa_kwanza_somalia_katika_miaka_25_624x351_bbc_nocredit.jpg

Zaidi ya wanafunzi elfu 70 walifanya mitihani ya kidato cha nne katika maeneo ya kusini na kati mwa Somalia, ikiwa ni mitihani ya kwanza ya kitaifa katika kipindi cha miaka 25.
Mitihani hiyo itaendelea kwa muda wa siku tano zijazo.

Katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, vituo 11 vilianzishwa kuwawezesha watahiniwa kufanya mitihani.

Elimu ni mojawapo ya sekta zilizoathirika vibaya na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza nchini Somalia mwaka wa 1991.
Tangu kusambaratika kwa serikali kuu nchini Somalia, mitaala mbali mbali imetumika katika shule na kufunzwa katika lugha tofauti tofauti.
Sasa wizara ya elimu inasema imechukuwa hatua za kuunganisha mitaala hiyo na kuhakikisha kuwa wanafunzi kote nchini wanafanya mtihani mmoja wa kitaifa.

150616131710_mtihani_wa_kwanza_somalia_katika_miaka_25_624x351_bbc_nocredit.jpg

Licha ya pingamizi kutoka kwa makundi mbali mbali yaliyoyounda mitala hiyo katika shule za kibinafsi nchini Somalia, serikali iliidhinisha kufanyika kwa mitihani huu.
Waziri wa elimu wa Somalia Khatra Bashir Ali ambaye alikuwa miongoni mwa maafisa waliosimamia mitihani hiyo, alisema nchi hiyo ina mengi ya kufanya katika ulimwengu wa sasa unaoegemea mfumo wa digitali.
Wengi wa wanafunzi waliofanya mitihani hiyo walikuwa na furaha.

150616131602_mtihani_wa_kwanza_somalia_katika_miaka_25_624x351_bbc_nocredit.jpg

Walisema wamefurahishwa na hatua ya kufanya mitihani iliyopangwa na kuandaliwa na serikali kinyume na hapo awali ambapo wasimamizi wa shule kibinafsi ndio waliochukuwa jukumu hilo.
Ulinzi umeimarishwa huku wasimamizi wakiwapekua wanafunzi ilikuhakikisha hakuna udanganyifu.
Kwa wasomali hii bila shaka ni hatua muhimu ya kihistoria katika juhudi za kujaribu kujenga upya taifa ambalo limezongwa na miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/06/150616_somalia_national_exams?ocid=socialflow_facebook

Jameni hongera kwa serikali zote ambazo zimekomaa humo humo hadi mafanikio yameanza kuonekana, wakati wengine walifyata mkia na kila siku wapo kazi ni kubeza waliojitolea. Juzi nimeiona video fulani kuhusu Somalia ya kisasa, matumaini yanaendelea kuonekana baada ya safari ya miaka 25, vijana wameanza kupata elimu ya kweli isiyo na chuki ndani ya nchi.

Alshabaab juzi wameiba vyakula kutoka kwa wanavijiji, ni ishara nzuri sana ya kuonyesha wameishiwa, na hadi wamechanganyikiwa, bangi zimewatuma kuvamia kambi ya jeshi, duh!!

FaizaFoxy na MOTOCHINI mujiandae kutalii Somalia. Wana hoteli nzuri sasa na usalama unaendelea kuimarishwa.
 
Last edited by a moderator:
MK254 Kwanini somalia wakenya mnaifanya kama koloni lenu! halafu kilajambo jema la somalia mnalipigia upatu na kulihusisha na nguvu zenu!
 
Last edited by a moderator:
Elimu kwanza si sera ya Lowassa tu, NI DIRA YA ULIMWENGU MZIMA.
 
MK254 Kwanini somalia wakenya mnaifanya kama koloni lenu! halafu kilajambo jema la somalia mnalipigia upatu na kulihusisha na nguvu zenu!

MOTOCHINI Kwa sababu wengi walijaribu wakatoroka, hadi hata Marekani na nguvu zao, ila sisi tumeenda na kukomaa nao hadi tukaiweka sawa. Na bado, tutatangaza kila mafanikio huko, halafu kwa taarifa yako, sasa hivi wagombezi wa urais wanaosifika na kusikika wote wana asilia ya Kenya. Mtahangaika sana na huo wivu wenu.
 
Last edited by a moderator:
Jameni hongera kwa serikali zote ambazo zimekomaa humo humo hadi mafanikio yameanza kuonekana, wakati wengine walifyata mkia na kila siku wapo kazi ni kubeza waliojitolea. Juzi nimeiona video fulani kuhusu Somalia ya kisasa, matumaini yanaendelea kuonekana baada ya safari ya miaka 25, vijana wameanza kupata elimu ya kweli isiyo na chuki ndani ya nchi. Alshabaab juzi wameiba vyakula kutoka kwa wanavijiji, ni ishara nzuri sana ya kuonyesha wameishiwa, na hadi wamechanganyikiwa, bangi zimewatuma kuvamia kambi ya jeshi, duh!! FaizaFoxy na MOTOCHINI mujiandae kutalii Somalia. Wana hoteli nzuri sasa na usalama unaendelea kuimarishwa.
Msiba umeisha au Standard Digital News - KTN : Kenya News, Nairobi News, World News, KTN Videos polen sana
 
Last edited by a moderator:
MOTOCHINI Kwa sababu wengi walijaribu wakatoroka, hadi hata Marekani na nguvu zao, ila sisi tumeenda na kukomaa nao hadi tukaiweka sawa. Na bado, tutatangaza kila mafanikio huko, halafu kwa taarifa yako, sasa hivi wagombezi wa urais wanaosifika na kusikika wote wana asilia ya Kenya. Mtahangaika sana na huo wivu wenu.
Wagombezi wa nchigan wenye asili ya kenya, wacheni kujidanganya kuwa nyie pekee mmewezesha hayo somalia ajabu kila day marekani hushambulia mara kwa mara kwa ndege kule, Warundi wapokule,Uganda wapo kule,Ethiopia wao kule.
 
Last edited by a moderator:
Wagombezi wa nchigan wenye asili ya kenya, wacheni kujidanganya kuwa nyie pekee mmewezesha hayo somalia ajabu kila day marekani hushambulia mara kwa mara kwa ndege kule, Warundi wapokule,Uganda wapo kule,Ethiopia wao kule.

Kati ya nchi hizo unazoziataja ni ni majeshi ya nchi gani waliojaribu kutuliza nje ya mji mkuu wa mogadishu?
 
Wagombezi wa nchigan wenye asili ya kenya, wacheni kujidanganya kuwa nyie pekee mmewezesha hayo somalia ajabu kila day marekani hushambulia mara kwa mara kwa ndege kule, Warundi wapokule,Uganda wapo kule,Ethiopia wao kule.

Hao wote uliowataja ni mashujaa, ila ni baada tu ya baba yao KDF kufika pale ndio issue ikakaa sawa, la sivyo ingekua mziki wa kila siku. Hilo la wagombezi sina haja ya kupoteza muda wangu maana hutawajua, wala kuwaelewa.
 
Ukipenda acha kupoteza muda kwani kama uongo itafahamika kwani kipindi hiki si chakumbumbereza dume mwenzie kuhusu habari kilajambo ukipenda kulifaham utalifahamu tena kwa ufasaha kuliko mropokaji asie jitambua na kujiamini, Hakuna KDF baba la yeyote wapuzi tu jeshi linakwenda kwenye shuguri pevu wana salia kuiba juice na mikate leo useme jeshi !!
 
Hehehe!! naona nimeguza penyewe, jamaa umetokwa na povu balaa... huwa nacheka sana nikiwafikisha katika hali hii.
 
Jameni hongera kwa serikali zote ambazo zimekomaa humo humo hadi mafanikio yameanza kuonekana, wakati wengine walifyata mkia na kila siku wapo kazi ni kubeza waliojitolea. Juzi nimeiona video fulani kuhusu Somalia ya kisasa, matumaini yanaendelea kuonekana baada ya safari ya miaka 25, vijana wameanza kupata elimu ya kweli isiyo na chuki ndani ya nchi.

Alshabaab juzi wameiba vyakula kutoka kwa wanavijiji, ni ishara nzuri sana ya kuonyesha wameishiwa, na hadi wamechanganyikiwa, bangi zimewatuma kuvamia kambi ya jeshi, duh!!

FaizaFoxy na MOTOCHINI mujiandae kutalii Somalia. Wana hoteli nzuri sasa na usalama unaendelea kuimarishwa.

Hongera sana kwa hilo.
 
Back
Top Bottom