Mtihani wa hisabati la saba wa kuchagua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtihani wa hisabati la saba wa kuchagua

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kimboka one, Sep 8, 2011.

 1. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  jamani mnisaidie hapa hivi watoto wanapopewa mtihani wa hisabati wa majibu ya kuchagua wanapima nini?,wadau wa elimu tuna domain 3 na vipengele vya katika table of specification,hawa wamewapima nini?,jamani siasa mpaka elimu?,kunasiku zitaingia kwenye afya.
   
 2. Big One

  Big One JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 759
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  wanatakiwa wakokotoe wenyewe mpk kieleweke kuchagua c wanaweza kuibiana
   
 3. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  kwani wewe hujui serikali yetu? wanasubiri watoto wafeli form four then wapeane ulaji kwa
  kuunda tume ya uchunguzi. cha ajabu wakati huohuo wanasisitiza watoto wasome sayans.
  mi nasubiri watakapoanzisha multiple choice hata kwenye practicals za sayansi wanazopigia debe
  kwa sasa.wao wanathubutu hawawezi lakini wanasonga mbele
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Yani huo ni zaidi ya ujinga na uzembe wa hiyo tume ya elimu ya kizushi!!

  Sijui wanategemea kufaidika vipi kwa kuwalemaza vijana ambao ndo wanaotakiwa kuendesha nchi siku zijazo!!
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  kwani kuna tatizo gani hapo mkuu??
  kwani mitiani ya zamani ilikuwaje? mitihani ya hisabati huwa wanatakiwa kuandika jibu tu, sio kuonyesha jinsi jibu lilivyopatikana kama kwenye higher levels.

  Of course, siifagilii njia hiyo ya kuandika jibu tu, lakini thats just a fraction of our education system.
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  nawaambia wana jf darasa la 4 la mkoloni ni sawa na mtoto wa kidato cha 6 wa tanzania ya leo!bora watoto wetu wajiandikishe kufanya mitihani ya cambridge
   
 7. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Iko poa, NIMEIKUBALI
   
 8. c

  conversant Member

  #8
  Sep 9, 2011
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  mmh! Mi naona iko sawa tu cuz kama hajui kufanya hayo mahesabu hawezi pata jibu sahihi sema kuwe na usimamizi madhubuti kusiwe na kuegelezeana
  kwa nchi kama turkey hiyo ipo hata university entrace exams zinaitwa Yoss na pia USA kuna SAT mambo ni multiple choice na kama hujui utaona nyota tu kama hiyo yoss hata form six PCM inamtoa nishai
  wakuu msiwe watu wakulalamika waliofanya hivyo wanaelewa ndio maana wabongo kwenye interview za kimataifa tunashindwa cuz tunaona kusoma ni kurelease tulivyokariri hata kama ni hesabu watoto wanataka kujua formular tu bt logic hamna duh! Tubadilike so we can b great thinkers
   
 9. nachid

  nachid JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  <br />
  <br />
  Mtihani wa mwaka huu wa std 7 wametaka uonyeshe njia uliotumia kupata jibu
   
 10. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Ni maswali yote ya kuchagua au ni mchanganyiko?

  Halafu si kweli kwamba maswali ya kuchagua ni rahisi ki hivyo (kama mtunzi yupo makini). Binafsi nimefanya mitihani (ya hesabu/mahesabu/numbers) yenye 'multiple choice' hata katika level za juu na kwa kweli parts za multiple choice ndio watu walikuwa wanaboronga zaidi au kutumia muda mrefu hasa kama hujui/huna uhakika na unachofanya!
   
 11. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  According to NECTA, all exams are in multiple choice format to enable the use of electronic mark recognize machine. Mashine hii karatasi ya majibu inapita na yenyewe inatambua kama jibu la swali husika ni right au wrong. Hii itasaidia 1. Kupunguza upendeleo au makosa ya kiusahishaji. 2. Kupunguza muda wa kusaisha. 3. Kuokoa manpower.
   
 12. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Kwani huduma zinazotolewa katika sekta ya afya (hospitali, vituo vya afya na zahanati) huoni kuwa ni dhihaka tosha??Duka la madawa nako unakutana na dawa feki achia mbali kuuziwa hata madawa yaliyokwisha muda wake ufaao kwa matumizi.
  Eee Mungu endelea kufanya OVERTIME kuilinda Tanzania na watu wake maana serikali kama imeamua kutuacha tujihangaikie hata kwa yale ambayo tunailipa kodi kuiwezesha iyafanye kwa ajili yetu kama wananchi tuliyoiajiri itutumikie
   
 13. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Sipati picha pale mwanafunzi asiyejua kabisa hisabati kwa kupitapita huko nyuma,akafanikiwa kupata alama za juu kwenye mtihani wa mwisho kisa tu alibahatika kuchagua majibu sahihi baada ya kufanya "ana ana do" !.....Hii ndo mizigo wanayotupiwa walimu wa sekondari za kata...lol.
   
 14. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2011
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  jamani nimefanya utafiti kunashule moja mwka jana imepokea watoto sita hawajui kbsa kusoma na Tsm9 imesama mtoto huyu hana uwezo wa kusoma sekondari,cha ajabu yupo darasani f1,sasa hili la hisabati ni moja ya maandalizi ya kuongeza wngn
   
 15. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,057
  Likes Received: 3,084
  Trophy Points: 280
  Aaahaa!nilicheka sana watoto wengi wanasema mtihani wa mwaka huu ni mwepesi sana,tena kengine kakasema kwa wepesi huu hata walioko drs la5 leo wanaweza kuujibu mtihani huu....sasa kama hii ndivyo ilivyo yangu ni macho!!ila nahisi wanapunguza uwezo wa watoto baadae kufanya solving.
   
 16. s

  siwalaze Senior Member

  #16
  Sep 10, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 124
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Si bora hata kukokotoa mwenyewe,kuliko kuandika A,B,C,D daah!!
   
 17. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  hio ndo elimu ya bongo bana halafu 2nalalama watoto we2 hawapend mats!? Shame..whr z foundation?
   
 18. The Pen

  The Pen JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 764
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Elimu ya ki-twishen twishen. Ni shortcuts kwenda mbele.
   
 19. N

  NIMIMI Senior Member

  #19
  Sep 13, 2011
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jana usiku katika dkk 45 Dr. Kawambwa alikumbusha kuwa mitihani hiyo ya maswali kuchagua kwenye Hisabati ilikuwepo hata enzi zao hivyo serikali inaonesha kwenda na mifumo ya kikoloni katika Elimu ya karne 21.
   
 20. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #20
  Sep 13, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Umesoma wapi mkuu? Nakumbuka pepa ilikuwa na column za Swali, kazi, jibu.
  <br />
  <br />
   
Loading...