Mtihani wa elimu ya msingi leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtihani wa elimu ya msingi leo

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by KiuyaJibu, Sep 9, 2009.

 1. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Darasa la saba kote nchini Tanzania leo wanafanya mtihani wa kumaliza elimu yao ya msingi baada ya kuisotea kwa miaka saba;kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi.

  Naibu Waziri Mwantumu Mahiza alisema,wanaotakiwa kufanya mtihani huo ambao utachukua siku mbili yaani leo na kesho ni wale wote waliosajiliwa kuanzia mwanafunzi aliyelipa ada,ambaye hajalipa ada,mwenye ujauzito(mjamzito) ili mradi tu awe amesajiliwa kwaajili ya mtihani wa mwaka huu.

  Binafsi kilichonisikitisha,ni hili tatizo la wanafunzi wajawazito;kwa mfano katika wilaya ya Tabora imetolewa takwimu inayosema katika kila wanafunzi saba(7) watatu(3) ni wajawazito.

  Kali zaidi ni ile ya iliyotokea kijiji cha Chito kilichopo mkoani Tabora ambapo mabinti watatu wa mheshimiwa mwenyekiti wa kijiji kugundulika wote watatu wanaingia kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi wakiwa wajawazito.

  Kwa mujibu wa sheria namba 27 ya elimu,inamaanisha hawa wote wanaofanyia mtihani wakiwa wajawazito ndiyo wamejitoa kwenda elimu ya sekondari kwa njia moja ama nyingine ila wanaweza kujiendeleza kupitia utaratibu wa MEMKWA.

  Wakati huohuo mkuu wa wilaya ya Tabora amesema amesikitishwa sana na hali hiyo na amesema atahakikisha waliofanyia vitendo hivyo wanafunzi hao wanabainika na kufikishwa katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi za kinidhamu dhidi yao.

  Kwa mtazamo wangu binafsi,bado naamini Fataki ana nguvu kuliko jamii inavyopambana nae.
   
 2. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duu bongpo jamani watoto wadogo twafanya nao penzi wapi na wapi? iwepo sheria ya kumfunga mtu ten years bila faini. Ni noma sasa. Kila jambo baya Africa linaporipotiwa na BBC lazima TZ itajwe au limetokea TZ haya STD 7 are pregnants.
   
Loading...