CPA
JF-Expert Member
- Mar 1, 2011
- 809
- 354
Utaratibu mpya uliotangazwa unatoa nafasi kwa wabunge wa EALA kwa mwaka 2017 kulingana na idadi ya wabunge wa kila chama kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Kwa mujibu wa Mwongozo huo, kutokana na idadi ya wabunge wa vyama kwa kila chama, CCM imepata nafasi za wabunge sita kwenda EALA, Chadema mbili, CUF moja, huku ACT Wazalendo pamoja na NCCR Mageuzi, vikiwa havina nafasi hata moja kwenye Bunge hilo la Afrika Mashariki, kutokana na kuwa na mbunge mmoja kila kimoja, hivyo kutokidhi
Kutokana na hali hiyo, Zitto ameliandikia Bunge barua kutaka Kamati ya Kanuni za Bunge ikutane kujadili uchaguzi wa wajumbe wa Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki.
Barua hiyo, ambayo baadhi ya wachambuzi wa siasa wanadai inalenga kutaka utaratibu wa awali ubadilishwe ili chama cha Zitto (ACT Wazalendo), kimwingize mwanachama wake, Profesa Kitila Mkumbo kugombea ubunge huo, inasema mwongozo uliotolewa na Bunge umekwenda kinyume cha Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wanasema endapo hoja ya Zitto ikikubaliwa, ni rahisi zaidi wagombea wa Chadema wakakosa nafasi hizo na badala yake nafasi za upinzani kuiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki zikachukuliwa na wagombea wa ACT na wale wa CUF.
Hali hiyo inaelezwa kuchangiwa na wabunge wengi kwenye Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuwa ni wa CCM, hivyo ni rahisi kuweka msimamo wa kuwapigia kura wale wagombea wa ACT Wazalendo na wale wa CUF, badala ya wale wa Chadema kutokana na hali ya kisiasa iliyopo nchini kwa sasa.
Barua ya Zitto ya Machi 28 iliyoandikwa kutokana na Tangazo la Bunge kwenye gazeti namba 11 la Machi 17, lililotangaza uchaguzi huo na masharti yake, ilisema mwongozo wa uchaguzi huo unavunja kanuni mbalimbali na kwamba kitakachofanyika sasa kitakuwa ni uteuzi na siyo uchaguzi.
Source: www.mitandaoni.co.tz, Mtifuano wa CHADEMA vs ACT ubunge wa EALA, Lissu awaambia ACT wasitumiwe na CCM – Mitandaoni: Blog ya jamii