Mtibwa hii sijui kama itakuja kutokea

Twamo

JF-Expert Member
May 27, 2017
2,881
4,993
Mtibwa sugar sports club ni moja ya timu zilizodumu katika ligi kuu kwa muda mrefu! Ilipanda daraja enzi hizo ikiitwa daraja la kwanza mwaka 1996. Katika kipindi chote hicho wachezaji wengi wamepita katika timu hiyo. Kati ya vizazi vya wachezaji vilivyopita kizazi hiki kamwe hakitasahaulika!
Sudi Slim
Meck Mexme
Kassim Issa
Geoffrey Magori
Salum Mayanga
Patrick Batwel
Mussa Hassan Mgosi
Kamba luffo
Abubakar Mkangwa
John Thomas Masamaki
Zuberi Shaban Katwila

Hapo sijataja watu kama kina Manyika Pitta, Saidi Mhando, Victor Costa, Nicco Nyagawa, Godifrey Kikumbizi, Salhina Mjengwa n.k! Kwa ujumla ni wengi sana waliopita Mtibwa sugar sports club! Sitaki kutaja kizazi hiki cha kina Juma Abdul, Kichuya, Dante na wengineo!

Katika miaka ya karibuni timu hii imeonekana kutofanya vizuri na sababu kubwa ni uongozi wa kiwanda kupunguza bajeti yake kwa timu! Nikiwa mdau mkubwa wa soka naomba wafadhili waitazame timu hii kwa jicho la ziada kwani ndio pekee inayoweza kuleta upinzani kwa hizi timu za Kariakoo.
 
mtwamo pale juu kabisa hukupaswa kumsahau salihina mjengwa pia omari kapilima mimi mtu ambaye angerudi hata leo ni kasimu issa namba tatu bora kabisa.Mkuu hebu lete na wale prison anza na NSEKA BUGOYA
 
Sawa wamekusikia...!

Hii si ile Mtibwa iliyokosa pesa za kusafiri kwenye muchuano ya Africa!?
Haikukosa pesa, sema kina Jamal baada ya kuona wameshatolewa wakaona haina haja ya kupeleka timu kucheza mechi ya away!
 
Monja Liseki
Monja ni miongoni mwa wakongwe walioenda kuisapoti timu! Wengine ni kina Alphonce Modest, Mao Mkami, Saidi Mrisho ziko wa kilosa, Stephen Names, Juma Buruhan na wengineo! Hawa hawakujengwa na Mtibwa walienda tu kumalizia vipaji vyao
 
Back
Top Bottom