GE2025 Mtia nia Udiwani aliyetoweka siku 7 kupigiwa kura leo. Polisi kufanya uchunguzi

GE2025 Mtia nia Udiwani aliyetoweka siku 7 kupigiwa kura leo. Polisi kufanya uchunguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
844
Reaction score
1,604
Wakati wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata wakijiandaa kupiga kura kwa watiania wa ubunge na udiwani leo Jumatatu, Agosti 4, 2025, hali ni tofauti kwa Siza Mwita, mtiania wa udiwani wa Ganyange mkoani Mara, ambaye zimepita siku saba hajulikani alipo.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi mkoani Tabora ambako limekutwa gari la mtiania huyo, limesema linafuatilia taarifa hiyo. Kutokana na hali hiyo, Mwita hakuwa sehemu ya watiania wa udiwani waliofanya ziara katika kata na matawi ya CCM kwa wajumbe kujitambulisha na kuomba kura za maoni, kuelekea mchakato unaofanyika leo.

1754294514475.png

Hata hivyo, chama chake cha CCM, kimesema jina lake litakuwa miongoni mwa ya watiania yatakayokuwepo kwenye karatasi za kupigiwa kura na kuchaguliwa au kutochaguliwa, litakuwa jukumu la wajumbe.

Siza alipotea pamoja na rafiki yake, Antony Gabriel, walipokuwa safarini, huku gari yao ikitelekezwa wilayani Nzega mkoani Tabora.

Akizungumza na Mwananchi, leo Jumatatu Agosti 4, 2025, Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Hamza Kyeibanga amesema jina la Siza ni miongoni mwa yatakayokuwepo kwenye karatasi za kupigia kura.

Wakizungumzia kutoweka kwa wawili hao, ndugu zao wamesema Siza na Gabriel waliondoka nyumbani Julai 29, 2025 kwenda kwenye shughuli zao za kibiashara kama ambavyo wamekuwa wakifanya siku zote.

Soma zaidi www.mwananchi.co.tz (Imeandikwa na Beldina Nyakeke).
 
Naumia sana chama ambacho Nina kadi yake kinatia aibu kiasi hiki!!

Mungu tusaidie!
 
Back
Top Bottom