Mti wa Ajabu

Mti wa Ajabu

Hii miti ipo sana bukoba nikawaolida sana! ila kama kuna haja yakufanya reseach mkuu endelea natafuta msaada chuo cho chote cha mistu.
 
imani ya kishirikina umeiona wapi katika maelezo yake? wewe mwenyewe ndo mshirikina. sikio lako umeliandaa kusikia ushirikina tu wala sio maajabu ya sayansi ya uumbaji wa mwenyezi Mungu.
Imani za kishirikina zimetawala UBONGO wako
 
imani ya kishirikina umeiona wapi katika maelezo yake? wewe mwenyewe ndo mshirikina. sikio lako umeliandaa kusikia ushirikina tu wala sio maajabu ya sayansi ya uumbaji wa mwenyezi Mungu.

Mbona unajihami baada ya kutaja ushirikina. Huwa unaushiriki au umeshawahi kuushiriki? Sio kosa lako. Tatizo shallow mind. Duniani hakuna mti wa namna hiyo. Nimesoma miti ya aina mbalimbali, hakuna mti wa aina hiyo. Kama unathibitisha naomba unitajie jina la mti huo kwa lugha ya kitaalamu au hata kwa lugha ya kabila lako.
 
inawezekana ni transpiration inafanyika yaani kitendo cha mmea kupoteza maji yakiwa katika hali ya mvuke kupitia stomata ambazo zipo kwenye majani .pia hujatuambia upo wapi wapi kulingana na hali ya hewa hawa maji yakatoka katika hali ya kuwa yamepoa gutation.lakini pia ningependa mzizimkavu unisaidie scientific name ya huo mti au mtoa mada
Ni kawaida baadhi ya miti wakati wa jua kali kutoa maji maji lakini haipendezi kukaa chini ya mti saa 7 mchana wakati wa jua kali unawezwa kukumbwa Shetani mbaya kwani mashetani huwa wanakimbilia kwenye miti wakati wa jua kali. Huo ndio ushauri wangu.
 
Uku kwetu mingi sana hata mimi cku ya kwanza nilishanga kidogo sio kwama ulivyo shangaa wewe. ukanda wa baridi unatoa maji kwa wingi na chini panakuwa kama mvua
 
Hao ni wadudu fulani ambao hukaa vikundi vidogovidogo juu miti mbalimbali, fanya uchunguzi wa kina utagundua hilo, hakuna maajabu yoyote hapo. Kwa sisi tuliokulia vijijini wadudu hao wanaishi hata kwenye miti ya mihogo wakati wa jua kali.
 
Muulize kapuya,c utani ni mtaalamu wa mimea aliyebobea,hawa wengine wanahisi tu,ktk hali isiyo ya kawaida nami pia nimewahi kushuhudia mmea mmoja mdogo ambao ukiunyoshea kidole tu unasinyaa wenyewe,mmea huo ni ngumu sana kuuona,na kwa taarifa nilizopewa na yule mzee mwenyeji wangu ktk lile pori la kutisha,(nahifadhi jina) ni kwamba mmea huo hutumiwa sana na wachawi pamoja na waganga hatari wa kienyeji.

Mkuu nadhani huo mmea kitaalamu ndiyo ule unaoitwa mimosa pudica unasifa ya kuitikia kichocheo cha mguso (THIGMOTROPHIC PLANT) yaani hata mdudu akitua kwenye jani lake hilo jani linajifunga na kutoa kemikali zinazomuua huo mdudu na kumfyonza ndani. Ni mmea wa kipekee ambao hautegemei miziz pekee kujipatia chakula chake. Ukiandika jina hilo youtube au ukasearch google utapata taarifa zake zaidi.

BACK TO THE MAIN TOPIC: Ni kweli kuwa mmea unafanya evapotranspiration kama njia moja wapo ya kusafirisha virutubisho mbalimbali kwenye sehemu mbalimbali za mmea husika, lakini kwa mujibu wa mleta mada nadhani kuna kitu cha kutilia maanani.Anasema mmea huo mara zote anapopita hapo anaona unafanya tabia hiyo kitu ambacho siyo cha kawaida.Transpiration huwa ni ya vipindi tu na hasa huwa inakuwa maximum kipindi cha jua kali. Namshauri mleta hoja ajaribu kuwaona wataalamu wa miti (BOTANISTS) vyuo vikuu au kwenye taasisi za utafiti, who knows may be ni new discovery na wewe unakuwa second after Mr. Erasto Mpemba with MPEMBA EFFECT.
 
yanadondoka kimoyomoyo
attachment.php

...mbona siyaoni hayo matone yakidondoka...?
 
Si mnasemaga Kapuya hamnazo, mwiteni hapa uone atakavyowafafanulia. Botany woyeeeee
 
Mbona unajihami baada ya kutaja ushirikina. Huwa unaushiriki au umeshawahi kuushiriki? Sio kosa lako. Tatizo shallow mind. Duniani hakuna mti wa namna hiyo. Nimesoma miti ya aina mbalimbali, hakuna mti wa aina hiyo. Kama unathibitisha naomba unitajie jina la mti huo kwa lugha ya kitaalamu au hata kwa lugha ya kabila lako.

usijifanye msomi kumbe kanjanja. Ungekuwa umesoma aina ya miti duniani ungeujua na huo kwa jina lake picha yake iko hapo juu.
 
Hao ni wadudu fulani ambao hukaa vikundi vidogovidogo juu miti mbalimbali, fanya uchunguzi wa kina utagundua hilo, hakuna maajabu yoyote hapo. Kwa sisi tuliokulia vijijini wadudu hao wanaishi hata kwenye miti ya mihogo wakati wa jua kali.

Maelezo yako ni sahihi kabisa,nipo maeneo ya Mkoa wa Pwani miti hiyo ni mingi sana na wenyeji wanaiita miombo.Asili ya maji hayo ni mikojo ya hao wadudu na atawaona akichunguza kwa makini .
 
inawezekana ni transpiration inafanyika yaani kitendo cha mmea kupoteza maji yakiwa katika hali ya mvuke kupitia stomata ambazo zipo kwenye majani .pia hujatuambia upo wapi wapi kulingana na hali ya hewa hawa maji yakatoka katika hali ya kuwa yamepoa gutation.lakini pia ningependa mzizimkavu unisaidie scientific name ya huo mti au mtoa mada

Nipo kati ya mkoa wa Pwani na Morogoro.
 
Maelezo yako ni sahihi kabisa,nipo maeneo ya Mkoa wa Pwani miti hiyo ni mingi sana na wenyeji wanaiita miombo.Asili ya maji hayo ni mikojo ya hao wadudu na atawaona akichunguza kwa makini .

Nimechunguza ila sijapata kuwaona hao wadudu kwakweli,nisingekuwa na haja ya kuitoa hii ishu endapo ningehakiki km kuna wadudu wa aina hiyo.
 
Sio mtaalamu wa masuala ya misitu ila kwakuwa ninautimamu wa akili ninaweza nikagundua vitu mbalimbali katika mazingira ninayoishi,mfano ni huo mti hapo.

Huo mti upo maeneo ambayo ninapita pindi ninapoelekea katika shughuli zangu za kila siku sio mbali sana na nyumbani ninapoishi.
Mara nyingi ninapopita chini ya mti huo huo ninahisi kuna vitone vinanidondokea,siku ya kwanza nilidhani labda itakuwa ni dalili za mvua kwa maana kulikuwa na wingu la mvua ingawa haikunyesha siku hiyo.

Siku ya pili nilipita jua lilipokuwa kali mno majira ya saa saba,nikadondokewa tena na vitone mithili ya vinyunyu vya mvua ila hakukuwa na wingu pindi nilipoangalia angani,nikashtuka nikajua labda itakuwa ni nyoka anajaribu kunishambulia kwa mate.
Nilipokagua katika matawi na kutupa mawe kadhaa juu ya mti sikufanikiwa kuona kile nilichokuwa ninahisi (Nyoka).

Ila yale matone yaliendelea kudondoka kwa nyakati tofauti tofauti kutoka katika kila tawi,mmh nikaona bora nisepe labda kuna wadudu wanakojoa.

Siku ya tatu ndipo nikaona hapana leo lazima nitoke na jibu kamili ni kitu gani hasa kinaendelea katika mti huo??,

Nikaenda mida ileile ya saa saba kisha nikaukagua sana ule mti sijaona ndege wala aina ya ndege na kama kawaida nikaona matone yakitoka katika kila tawi la huu mti,ilikuwa ni ajabu sana kwangu nadhani hata kwako pia kama endapo hujawahi kuona ama kushuhudia kitu kama hicho.

Na mpaka leo ukifika mida ya jua kali chini ya mti huo utashuhudia mfululizo wa vitonetoka katika majani machanga ya mti huo,kama wewe ulishawahi kuona haya!!,ila kwangu ni maajabu tosha.

uwe unafanya uchungunzi kabla ya kupost hii miti mbona ipo sana
 
Back
Top Bottom