dasenior
Senior Member
- Jul 24, 2012
- 138
- 57
Sio mtaalamu wa masuala ya misitu ila kwakuwa ninautimamu wa akili ninaweza nikagundua vitu mbalimbali katika mazingira ninayoishi,mfano ni huo mti hapo.
Huo mti upo maeneo ambayo ninapita pindi ninapoelekea katika shughuli zangu za kila siku sio mbali sana na nyumbani ninapoishi.
Mara nyingi ninapopita chini ya mti huo huo ninahisi kuna vitone vinanidondokea,siku ya kwanza nilidhani labda itakuwa ni dalili za mvua kwa maana kulikuwa na wingu la mvua ingawa haikunyesha siku hiyo.
Siku ya pili nilipita jua lilipokuwa kali mno majira ya saa saba,nikadondokewa tena na vitone mithili ya vinyunyu vya mvua ila hakukuwa na wingu pindi nilipoangalia angani,nikashtuka nikajua labda itakuwa ni nyoka anajaribu kunishambulia kwa mate.
Nilipokagua katika matawi na kutupa mawe kadhaa juu ya mti sikufanikiwa kuona kile nilichokuwa ninahisi (Nyoka).
Ila yale matone yaliendelea kudondoka kwa nyakati tofauti tofauti kutoka katika kila tawi,mmh nikaona bora nisepe labda kuna wadudu wanakojoa.
Siku ya tatu ndipo nikaona hapana leo lazima nitoke na jibu kamili ni kitu gani hasa kinaendelea katika mti huo??,
Nikaenda mida ileile ya saa saba kisha nikaukagua sana ule mti sijaona ndege wala aina ya ndege na kama kawaida nikaona matone yakitoka katika kila tawi la huu mti,ilikuwa ni ajabu sana kwangu nadhani hata kwako pia kama endapo hujawahi kuona ama kushuhudia kitu kama hicho.
Na mpaka leo ukifika mida ya jua kali chini ya mti huo utashuhudia mfululizo wa vitonetoka katika majani machanga ya mti huo,kama wewe ulishawahi kuona haya!!,ila kwangu ni maajabu tosha.