Mti mrefu duniani wagundulika

Mti mrefu duniani wagundulika

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,608
Wanasayansi nchini Uingereza na Malaysia wanasema kuwa wamegundua mti mrefu zaidi duniani wenye urefu wa zaidi ya mita 100. Mti huo wa kitropiki aina ya meranti ulipatikana katika msitu wa Borneo na kundi moja kutoka chuo kikuu cha Nottingham mwaka uliopita.

66b8dab7e695cabe4e46e6630adc779e

Kwa mujibu wa BBC. Watafiti kutoka katika chuo kikuu cha Oxford walifanya utafiti huo kwa kutumia kamera zisizokuwa na rubani kuthibitisha rekodi hio.

Mti huo uliopatikana katika eneo la uhifadhi la Danum Valley huko Sabah umepewa jina Menara ambalo linamaanisha jumba refu.

66b8dab7e695cabe4e46e6630adc779e-1

Mkweaji miti kutoka eneo hilo, jami ambaye aliupima mti huo kwa kutumia kamba alisema alliogopa kuupanda mti huo

”Lakini kwa kweli picha kutoka juu ilikuwa nzuri mno. Sijui cha kusema isipokuwa tu ulikuwa uzoefu mzuri sana”, liongezea.

Inadaiwa kuwa mti huo unaweza kuwa mti mrefu wenye maua duniani.


Inadaiwa kuwa mti huo unaweza kuwa mti mrefu wenye maua duniani.
Daktari Doreen Boyd, kutoka chuo kikuu cha Nottingham, alisema kuwa ugunduzi huo ulikuwa muhimu kwa kuwa ni sayansi inayosema miti kama hii inapatikana , ni mirefu hali ya kwamba hatukuwahi kudhania na huenda kuna miti mirefu zaidi ambayo haijagunduliwa.

”Inatuambia kwamba tunahitaji kuilinda miti”, alisema. Daktari Alexander Shenkin , kutoka chuo kikuu cha Oxford , alisema baada ya kusikia ugunduzi huo walitembea kwa muda wa saa tatu hadi Menara.

Alisema: Nimeona kile ambacho wanasema ni miti mingi , lakini nilipotembea hadi katika mti huu, kichwa changu kilizidi kuangalia juu unapokaribia kileleni.Sijawahi kuona mti mrefu kama huu.
 
Vile ule wa Kilimanjaro ushapitwa urefu ghafla hata mwaka haujaisha
 
Maajabu kwa kweli
Hapo inaonekana ni msitu mkubwa na mti unazidi kurefuka kutafuta mwanga.
Sijui mti huu unakunywa maji kiasi gani?


Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Back
Top Bottom