Mtera wanaweweseka nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtera wanaweweseka nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Mar 12, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Anayemvaa Malecela ashambuliwa Dodoma
  Na Mwandishi wetu  12th March 2010


  [​IMG]
  B-pepe  [​IMG]
  Chapa  [​IMG]
  Maoni

  [​IMG] CCM wilaya wajitokeza kumpinga
  [​IMG] Wamlaumu kudai amerithishwa jimbo  [​IMG]
  Mbunge wa sasa, John Malecela.  Wenyeviti na makatibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Mtera, mkoani Dodoma, wameibuka na kupinga madai yaliyotolewa na Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Livingston Lusinde, kuwa aliahidiwa kuachiwa jimbo hilo na Mbunge wa sasa, John Malecela, katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
  Akisoma tamko la kupinga kauli ya Lusinde kwa waandishi wa habari mjini hapa jana kwa niaba ya viongozi wa CCM jimbo la Mtera, Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Chamwino, Patrick Nyambuya, alisema wanashangazwa na madai hayo yaliyotolewa hivi karibuni na kusema kuwa ni ya uongo.
  Mkutano huo ulifanyika katika baa ya Kibarua mjini hapa na kuhudhuriwa na wenyeviti na makatibu zaidi ya 20 wa kata za jimbo la Mtera waliokuwa wamevalia sare ya CCM.
  Nyambuya alisema kuwa madai hayo aliyoyatoa Lusinde wakati akitangaza kugombea katika jimbo hilo katika uchaguzi wa Oktoba sio ya kweli na kuonyeza kuwa nia yake ni kumpaka matope Malecela.
  Mwenyekiti huyo adai kuwa kauli za Lusinde zimewashangaza viongozi kwani ubunge si ufalme wa kuachiana na kwamba jimbo ni mali ya wananchi, sio la mbunge.
  Nyambuya alisema kauli ya Katibu huyo inalenga kumpaka matope Malecela ambaye mpaka sasa nia yake ya kugombea katika uchaguzi ujao haijabadilika.
  Alisema ingawa ni haki ya kila mwana-CCM kugombea katika jimbo hilo, lakini ni vyema kauli za wanachama kupakana matope zikaepukwa.
  Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, wao kama viongozi wa CCM jimboni humo hawana taarifa yoyote kuhusiana na suala la Malecela na Lusinde kuachiana jimbo hilo.
  Aidha, Nyambuya alisema madai ya Lusinde kwamba Malecela aliwaaga wananchi wa jimbo lake ni ya uongo kwani hakuna siku ambayo mbunge huyo alitamka kuwaaga wananchi wake kwamba anastaafu ubunge mwaka huu.
  “Tunashangazwa na kauli za Livingstone, sisi tunachojua kwa mujibu wa katiba ya chama chetu, kila mwenye nia ya kutaka kugombea nafasi yoyote huchukua fomu na kuomba ridhaa ya chama chake na wanachama kumpendekeza kuwa mgombea kwa nafasi anayogombea, sio anavyodai kuwa aliahidiwa ataachiwa jimbo,” alisema Nyambuya.
  Hata hivyo, Nyambuya alisema chama kinakemea vikali vitendo vya wana-CCM kupaka wenzao matope kwa nia ya kutaka uongozi na kuonya kuwa watakaoendeleza vitendo hivyo hawatavumiliwa katika chama.
  Nyambuya alisema viongozi wa CCM katika jimbo hilo wamewaomba wenye nia ya kugombea wawe waadilifu na waseme ukweli ndani ya chama badala ya kuzua uongo ambao unaweza kuwafarakanisha wanachama wa CCM hasa katika Jimbo la Mtera.
  Malecela hajatangaza rasmi nia yake ya kugombea tena kiti hicho ingawa kumekuwepo na taarifa kuwa atagombea kwa mara nyingine.
  Hata hivyo, miezi kadhaa iliyopita, uongozi wa CCM Wilaya ya Chamwino ulijtoa tamko la kusifia utendaji wake hususan utekelezaji wa Ilani ya CCM.
  Pia, uongozi wa CCM wa Wilaya ya Chamwino ulimsifia Mbunge wa Chilonwa, Ezekiah Chibulunje, kwa utekelezaji wa Ilani ya CCM.
  Majimbo ya Mtera na Chilonwa yako katika wilayani Chamiwno.
  Malecela amekuwa mbunge wa Mtera kuanzia mwaka 1995 hadi sasa. Mwanasiasa huyo mkongwe nchini alishika nafasi nyingi za utumishi wa umma, ukiwemo uwaziri katika awamu ya kwanza na ya uwaziri mkuu awamu ya pili.
  Aidha, alishika wadhifa wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara katika awamu ya pili, ya tatu na ya nne hadi alipostaafu rasmi mwaka 2007.
  Lusinda bado ni mchanga katika siasa. Alijiunga na CCM miaka kadhaa iliyopita akitokea katika Chama cha National Leaque for Democracy (NLD).
  Baadaye aliteuliwa kuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma kabla ya kuhamishiwa Tarime.
  Source: Nipashe 12.03.2010
  MAONI YANGU: katika demokrasia ya kweli kila mtu anayo niya ya kusema kile kilichoujaza moyo wake. La sivyo hakuna haja ya uchaguzi.
   
 2. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nadhani kuna mtu anataka kuwa mbunge wa maisha jimboni humo. Wito kwa vijana competent, shime mjitokezeni kugombea ubunge kwenye jimbo hili na mengine.
   
Loading...