Mtendee hivi mpenzi asieonesha kukujali/kukuthamini

Singasinga

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2011
Posts
2,741
Reaction score
3,316
AMANI katika uhusiano ni hitaji la kila mmoja. Kila mtu akiwa na mtu ampendaye, kumjali na kumpa kipaumbele ni kitu cha kawaida katika maisha yake. Ila vipi ukiwa na mtu unayempenda sana ila yeye haonyeshi kukujali na kukuthamini? Mtu wa aina hii, unahitajika pia kuendelea kumwonyesha kumjali na kumpa hadhi kamili katika mahusiano yako?

Kama uko na mtu ambaye haonyeshi thamani na hadhi katika maisha yako japo huwa anasema anakupenda sana, unatakiwa kufanya yafuatayo.

Onyesha kumpenda na kumjali. Onyesha ni kwa namna gani ana thamani na umuhimu katika maisha yako. Japo itakuwa inauma kuonyesha upendo na thamani kwa mtu asiyefanya vile unavyotaka ila kumbuka upendo ni tiba.

Kuonyesha kumpenda na kumjali mtu ni mbegu inayoweza kuota ua la upendo katika nafsi yake. Binadamu kaumbiwa upendo. Hufarijika, hujisikia amani sana pale anapoonyeshwa kupendwa na kuhitajika.

Hivyo kumwonyesha upendo mtu asiyeonyesha kujali ni njia ya kuathiri akili na hisia zake ili uweze kufanikiwa kukuza thamani na hadhi yako katika maisha yake. Tathmini zinaonyesha kila mtu hupenda kuona akipendwa na kuthaminika hata kama haonyeshi kufurahi au kuheshimu suala hilo.

Baada ya kuonyesha kumjali kwa muda mrefu kiasi huku yeye akijifanya hana habari, mpotezee kiaina. Punguza kuonyesha ni kwa kiwango gani unampenda. Punguza kuongea naye juu ya thamani na hadhi aliyo nayo katika nafsi yako. Acha kabisa kulalamika juu ya tabia zake ambazo zimekuwa zikikukera.

Dhamira ya kufanya hivyo ni kumfanya akumbuke hadhi yako katika maisha. Kama nilivyosema mwanzo, kila mtu anapenda kuambiwa maneno matamu na mtu anayempenda, kila mtu hupenda kuona akipendwa na kubabaikiwa, hivyo kuacha mambo hayo kutamfanya aanze kufikiri juu ya tabia yako mpya.

Atajiuliuza ni kwanini sasa umebadilika? Nani anakufanya usimwone wa hadhi na thamani kama ilivyokuwa mwanzo? Maswali hayo, yatampeleka kujiuliza juu ya tabia zake pia.

Ataanza kujitathimini kama alivyokuwa anakutendea ilikuwa haki. Mawazo hayo huweza kumpeleka haraka katika wivu wa kuamini tabia zake za kijinga alizokuwa akikufanyia zimekufanya uwe na mtu mwingine anayekupa unachotaka ndiyo maana sasa hivi huna tena habari naye.

Kwa woga wa kukupoteza anaweza kuanza kukujali na kukufanyia mengi ambayo anahisi alikuwa hakufanyii ili akudhibiti usiende kwa mwingine.

Kosa la wengi katika mahusiano pale wanapoona wenzao hawawajali na kuwapa thamani inayotakiwa ni kuanza kulalamika sana ama kuwalilia na kudhani kwa kufanya hivyo itakuwa njia ya kupendwa na kupewa wanachotaka, kitu ambacho sio kweli hata kidogo.

Mapenzi ni mbinu na mikakati. Unatakiwa kujua kucheza na akili pamoja na hisia za mwenzako ili uweze kutawala maisha yake.

Ukiwa unamlilia sana mwenzako usidhani atabadilika tabia zake za ovyo. Mwenzako ili akupe thamani na hadhi stahili anatakiwa kuhisi wewe ni wa thamani na bora na unatakiwa kutendewa mengi makubwa na siyo hayo anayokutendea. Na njia bora ya kumfanya ahisi wewe ni wa thamani na bora zaidi ni kucheza na hisia pamoja na akili yake.

Ili upendwe sana auhitaji kumfanya mwenzako akuonee huruma. Jenga mazingira ya kumfanya muhusika ajue kabahatika kuwa na wewe ndipo atakupa hadhi na heshima stahili. Siyo kwa kulia wala kutoa lawama kila siku ila kwa kuonyesha wewe ni bora na unaweza kuwa na amani na utulivu hata bila yeye.

Copied from orijino
 
Hamna kitu,mtu kama hakupendi mwache aende zake no need ya kujichosha, me naamini mapenzi sio kutumia nguvu au technique kama za prison breaker, kama hakuelewi sepa wanawake au wanaume wamejaa wenye uhitaji wa mapenzi ya dhati but unapoendelea kuforce king ndo kutwa kucha unaumia
 
Kama ni mwanamke fanya haya;
1. Mnyime hela
2.usimpe fedha
3.Kaka acha kumpa pesa
4.Usimsaidie shilingi yoyote.
5.Nimesema usitoe yale makaratasi yenye picha ya Nyerere kwa mtu asiyekupenda.
Ukifanya hivi ndani ya siku saba ataandika barua kutubu na kuungama makosa yake kama wahujumu uchumi.
 
Haha atapewa kwingine
Hapa tunasemea ile really love
 
Eh zama hizi hakuna muda wa kupoteza, mtu ambae hakuthamini hata umfanyie nini haoni wala hajali....dawa ni moja tu kuondoka umwache peke yake ni heri kuwa pekee kuliko kuwa na mtu aliye kama mfu au kupoteza mda kuthibitisha thamani yako kwa kipofu
 
Hii nmeichukua aiseee
AMANI katika uhusiano ni hitaji la kila mmoja. Kila mtu akiwa na mtu ampendaye, kumjali na kumpa kipaumbele ni kitu cha kawaida katika maisha yake. Ila vipi ukiwa na mtu unayempenda sana ila yeye haonyeshi kukujali na kukuthamini? Mtu wa aina hii, unahitajika pia kuendelea kumwonyesha kumjali na kumpa hadhi kamili katika mahusiano yako?

Kama uko na mtu ambaye haonyeshi thamani na hadhi katika maisha yako japo huwa anasema anakupenda sana, unatakiwa kufanya yafuatayo.

Onyesha kumpenda na kumjali. Onyesha ni kwa namna gani ana thamani na umuhimu katika maisha yako. Japo itakuwa inauma kuonyesha upendo na thamani kwa mtu asiyefanya vile unavyotaka ila kumbuka upendo ni tiba.

Kuonyesha kumpenda na kumjali mtu ni mbegu inayoweza kuota ua la upendo katika nafsi yake. Binadamu kaumbiwa upendo. Hufarijika, hujisikia amani sana pale anapoonyeshwa kupendwa na kuhitajika.

Hivyo kumwonyesha upendo mtu asiyeonyesha kujali ni njia ya kuathiri akili na hisia zake ili uweze kufanikiwa kukuza thamani na hadhi yako katika maisha yake. Tathmini zinaonyesha kila mtu hupenda kuona akipendwa na kuthaminika hata kama haonyeshi kufurahi au kuheshimu suala hilo.

Baada ya kuonyesha kumjali kwa muda mrefu kiasi huku yeye akijifanya hana habari, mpotezee kiaina. Punguza kuonyesha ni kwa kiwango gani unampenda. Punguza kuongea naye juu ya thamani na hadhi aliyo nayo katika nafsi yako. Acha kabisa kulalamika juu ya tabia zake ambazo zimekuwa zikikukera.

Dhamira ya kufanya hivyo ni kumfanya akumbuke hadhi yako katika maisha. Kama nilivyosema mwanzo, kila mtu anapenda kuambiwa maneno matamu na mtu anayempenda, kila mtu hupenda kuona akipendwa na kubabaikiwa, hivyo kuacha mambo hayo kutamfanya aanze kufikiri juu ya tabia yako mpya.

Atajiuliuza ni kwanini sasa umebadilika? Nani anakufanya usimwone wa hadhi na thamani kama ilivyokuwa mwanzo? Maswali hayo, yatampeleka kujiuliza juu ya tabia zake pia.

Ataanza kujitathimini kama alivyokuwa anakutendea ilikuwa haki. Mawazo hayo huweza kumpeleka haraka katika wivu wa kuamini tabia zake za kijinga alizokuwa akikufanyia zimekufanya uwe na mtu mwingine anayekupa unachotaka ndiyo maana sasa hivi huna tena habari naye.

Kwa woga wa kukupoteza anaweza kuanza kukujali na kukufanyia mengi ambayo anahisi alikuwa hakufanyii ili akudhibiti usiende kwa mwingine.

Kosa la wengi katika mahusiano pale wanapoona wenzao hawawajali na kuwapa thamani inayotakiwa ni kuanza kulalamika sana ama kuwalilia na kudhani kwa kufanya hivyo itakuwa njia ya kupendwa na kupewa wanachotaka, kitu ambacho sio kweli hata kidogo.

Mapenzi ni mbinu na mikakati. Unatakiwa kujua kucheza na akili pamoja na hisia za mwenzako ili uweze kutawala maisha yake.

Ukiwa unamlilia sana mwenzako usidhani atabadilika tabia zake za ovyo. Mwenzako ili akupe thamani na hadhi stahili anatakiwa kuhisi wewe ni wa thamani na bora na unatakiwa kutendewa mengi makubwa na siyo hayo anayokutendea. Na njia bora ya kumfanya ahisi wewe ni wa thamani na bora zaidi ni kucheza na hisia pamoja na akili yake.

Ili upendwe sana auhitaji kumfanya mwenzako akuonee huruma. Jenga mazingira ya kumfanya muhusika ajue kabahatika kuwa na wewe ndipo atakupa hadhi na heshima stahili. Siyo kwa kulia wala kutoa lawama kila siku ila kwa kuonyesha wewe ni bora na unaweza kuwa na amani na utulivu hata bila yeye.

Copied from orijino
 
Hujui to love is to suffer?.
That is not love, love means the understanding and agreement of two people with the same feelings"

Love ni kujaliana, kupendana, kuheshimiana, kutumia muda mwingi pamoja (mawasiliano) haijalishi distance ... But ukishaona hivyo vitu havipo jua hayo sio mapenzi, kuna kitu kinaitwa one side relationship yani wewe peke yako ndio unajali, una heshimu, una call au una text first usipofanya hivyo ndio basi imetoka mwenzako hakutafuti wala nini, sasa hayo sio mapenzi huo ni uboya one side relationship sio sacrifice za mahusiano love is cheap kama mapenzi yapo yata flow yenyewe tu automatically hakutakua na haja ya kutumia nguvu kubwa wala ku suffer.

"The more you love kiboya the more you suffer
 
Eh zama hizi hakuna muda wa kupoteza, mtu ambae hakuthamini hata umfanyie nini haoni wala hajali....dawa ni moja tu kuondoka umwache peke yake ni heri kuwa pekee kuliko kuwa na mtu aliye kama mfu au kupoteza mda kuthibitisha thamani yako kwa kipofu
Kabisa na mtu akishaona unampenda anakufanyia makusudi bado unaendelea kumtaka basi ndo atakuumiza na kuku take for granted .. Unajikuta unapoteza muda bure, unang'ang'ania mtu miaka mitatu wakati ungekua umemuacha hio miaka mitatu ungekua umepona tayari na ushamsahau kitambo
 
Back
Top Bottom