KATIKA KILA KUNDI LA WANA-CCM 10 UTAKAOKUTANA NAO 08 NI WEZI WA MALI YA UMMA
Mtendaji wa nini huko Iringa, au wa CCM kasikia Nguvu ya Umma tunakwenda kuwashika wakarejeshe walichokipora???
Gamba walilolichokoza ilikuwa ni hoja-mtego itakayokimaliza kabisa CCM. Maana yake ni kwamba endapo mnyama mkubwa kama tembo mwili wake wote ni magamba sasa akianza kujivua gamba moja baada ya nyingine basi matokeo yake ni kwamba hata atakapofikia saizi ya mwili sawa na dawa ya piritoni bado haja ya kujivua gamba zaidi itakua inaendelea tu.
CCM katika hii dhana ya 'Kujivua Gamba' hapo ndipo kunasa kwenu jumla kwenye ndoano rahiiiiiiisi mno!!! Vueni hiyo migamba enyi wana-CCM mnaoelemewa na mizigo ya kutupora kila kitu nchini.
Katika hili nadhani Watanzania tuchange ili tukajenge Mi-jela zaidi ya kuwafungia wana-CCM endapo kweli kutakwepo na haja mioyoni mwao kujirudi na kweli kila mmoja wao 'Kujivua Magamba' sugu ya miaka nenda rudi kwa kuwaibia Watanzania.
Hili ni kutokana na ukweli kwamba katika kila kundi la Wana-CCM 10 utakaokutana nao 8 ni wezi wa mali ya umma ama kuendelea kufaidika nazo bila ustahili wowote.