G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,704
- 36,457
Tangia Mtela Mwampamba amalize degree yake ya kwanza pale chuo cha ualimu-DUCE na kupangiwa kituo cha kazi na serikali huko Mwanza hajawahi hata kuripoti kituoni hapo.
Mtela Mwampamba aliukana ualimu na degree aliyosomea aliitumia kama daraja kufanikisha harakati zake za kisiasa akauvaa ukada kwa kuanzia Chadema na alipoona kule hakuna maslahi kwake akaingia CCM.
Toka aingie CCM amekuwa ni msaka vyeo na ubunge bila mafanikio. Aliunda kikundi hewa ili kujisogeza karibu na macho ya viongozi aonekane.
Leo Mtela Mwampamba anateuliwa kwenda kuwa mtumishi wa umma na mbaya zaidi kwenda kuwasimamia hao waalimu ambao mbali na yeye kuwa na degree katika fani hiyo bado aliuona kama ajira ya hovyo.
Mtela Mwampamba kuteuliwa kuwa mtumishi wa umma kada aliyoikana hapo kabla siyo sahihi hata kidogo. Narudia tena siyo sahihi hata kidogo na huku ni kuwafedhehesha watumishi ambao wamejitolea kuutumikia utumishi wa umma kwa moyo mmoja. Hawa watumishi ndiyo walipaswa kuwa promoted na siyo kuteua makada walioukana Utumishi wa Umma.
Mimi nikiwa kama mwana Ubungo anatangaza rasmi kutokumpa ushirikiano Mtela Mwampamba kutokana na kutokuridhishwa na uteuzi wake.
Naomba nieleweke kuwa sina nia mbaya yoyote ile ila pale taratibu zinapokiukwa na pale wazalendo wanapopuuzwa ni lazima tuwasemee.
Rais kumteua Mtela Mwampamba kwenye utumishi wa umma ameenda kinyume na kauli mbiu yake na anaweza kupoteza imani yake kwa jamii. Hili siyo sahihi hata kidogo!