Hii bei kwa sasa hamna nchi nzimaGunia la debe nane
bei ya shambani ni tsh 90000
shukran kaka umenifungua macho...Daaaah wewe mkulima wa mpunga zikabili changamoto kwa kuwa mbunifu. Mimi pia ni mkulima wa mpunga ila nilikuja kubadili maamuzi kutikana na bei ya soko. Kwasasa nilishaacha kuuza mpunga kila napohitaji kuuza naukoboa na kuuza mchele wa jumla.
Waweza kuwa huna fedha ya kukoborea ila nenda kakoboe gunia moja kwa Tsh 5,000 kisha unauza hapo hapo na fedha utayopata yanajikoboa yenyewe. Mfano kuanzia mwezi wa tano hadi mwez wa tisa gunia la debe 7 huwa 50,000 hadi 70,000. Lakini ukikoboa mchele kwa gunia hilo hilo la debe 7 hutoa kilo 60 hadi 67 kwa mwezi wa 5 hadi wa 9 bei ya mchele kwa jumla huwa kuanzia 1,200 hadi 1,400 kwa mimi huwa natoa kilo 65 na kupata kuanzia 78,000 hadi 91,000. Mwezi wa 10 hadi 11 bei ya mchele huwa 1,400 hadi 1,600 hivyo kwa mpunga huwa 80,000 lkn mchele unapata kuanzia 91,000 hadi 104,000, mwezi wa 12 na kuendelea mwez wa 3 biashara ni neema tuuu.
Naimani kuna zile mashine kubwa za kukobolea mpunga zinazotenganisha mchele, chenga, na taka taka nyingine.
Pia uwe unajaribu kuzungukia mashine nyingi ha hapo karibia na ulipo kuulizia bei tofauti tofauti ili upate itayojuridhisha. Mwisho tengeneza kamtandao cha kuwa na wateja maalumu kwa kuuza mchele kuanzia wanaonunua mchele wa jumla mashineni, na wanaopika migahawani.
We uko wapi huko mkuu ambako bei ni tamu?niliko sasa gunia la debe saba ni 55,000 na mchele kilo 1,300
Nashukuru sana kwa ushauri mzuriDaaaah wewe mkulima wa mpunga zikabili changamoto kwa kuwa mbunifu. Mimi pia ni mkulima wa mpunga ila nilikuja kubadili maamuzi kutikana na bei ya soko. Kwasasa nilishaacha kuuza mpunga kila napohitaji kuuza naukoboa na kuuza mchele wa jumla.