Mtego wa TAKUKURU wamnasa Mhadhiri NIT akiomba rushwa ya ngono

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Mhadhiri Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Samson Mahimbo (66yrs) akamatwa na TAKUKURU Wilaya ya Kinondoni baada ya kunaswa katika mtego wa rushwa ya ngono kwa mwanafunzi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, Denis Manumbu ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kuwekewa mtego kutokana na taarifa iliyotolewa na mwanafunzi aliyeombwa rushwa hiyo ili aweze kumpatia matokeo mazuri ya mtihani wake wa marudio (Supplementary Exams).

“Bwana Mahimbo alimtaka mtoa taarifa (Mwanafunzi) kufika katika Bar ya Shani iliyoko maeneo ya Sinza jirani na Bar ya Meeda na alitii agizo hilo ambapo walikutana na akapewa majibu ya mtihani wa somo la Road Transport, na kuyaandika ili arekebishe mtihani wake alioufanya Janury 5, 2017”.
 
mi nataka kujua huo mtego huwa unakuwaje hasa, maana ile ya pesa huwa wanakupa unazipokea, baadae wanakusachi ndio wanakukamata nazo, sasa hii ya ngono inakuwaje kuwaje unapiga bao kwanza au?:)

Duh! ingekuwa hivi china wangejikamatisha wengi sana tuu !!!!

Na washawasha!
 
Mlalamikaji akitoa maelezo atataja namba. Watafuatilia mazungumzo ya hawa wawili ikiwa ni pamoja na kurekodi mazungumzo. Sauti zao ndzo ushahidi kuwa uliomba rushwa ya ngono. Lkn mjanja hapa anapozungumza na msichana hapaswi kuhusisha msingi wa KUBETI na ombi la ngono. Kwa kufanya hivi hata warekodi kesi haipo kwani kutongoza so dhambi, bali dhambi ni kuhusisha kutongoza na KUBETI.
 
Back
Top Bottom