Mtego wa CCM Kujilipa Kupitia Dowans na Tafsiri ya Wapiga-Kura 'TALAKA TOKOMEA'!!

Waacheni walipe..maisha yawe magumu mara kumi zaidi kwa watanzania na ndipo Dr Slaa atakapopenya kiurahisi ingawa itakuwa kama Ivory Cost

Ni nani anayejidanganya CCM kutoweka baada ya kuilipa kampuni ya kimahayawani Dowans? Kwa maoni yangu hapo ndipo watakapojiimarisha zaidi na hizo hizo fedha watakazochota.

Nyinyi laleni tu usingizi hapo na kuhesabu mikono ya binadamu kudondoka chini sawasawa na yalivyo mawazo ya mnyama fisi.
 
CCM endeleeni tu kuilipa Dowans bila ridhaa yetu na kwa mkono wa pili mpokee yenu talaka tokomea.
 
Ni nani anayejidanganya CCM kutoweka baada ya kuilipa kampuni ya kimahayawani Dowans? Kwa maoni yangu hapo ndipo watakapojiimarisha zaidi na hizo hizo fedha watakazochota.

Nyinyi laleni tu usingizi hapo na kuhesabu mikono ya binadamu kudondoka chini sawasawa na yalivyo mawazo ya mnyama fisi.

Leo hii ndio watakua wamekata kauli huko kwenye kikao chao Dodoma wakifanya kosa tu juu ya Dowans. Hakuna kujiimarisha wala nini.
 
Hivi huyu werema sheria alisoma mashambani kwao, na huyu mwanasheria wa serikali ambaye kesi inasomwa na yeye hakuwepo mpaka anaomba apewe mda apitie hukumu ndo atoe maelezo sasa anaisimamia serikali wapi? Chooni kwake?
 
Hivi huyu werema sheria alisoma mashambani kwao, na huyu mwanasheria wa serikali ambaye kesi inasomwa na yeye hakuwepo mpaka anaomba apewe mda apitie hukumu ndo atoe maelezo sasa anaisimamia serikali wapi? Chooni kwake?

Muda mwingi anayo kazi ya kufuatili malipo ya mikataba feki kuliko kutoa ushauri wa kisheria kwa serikali kutulinda na hasara mijanga kama hii ya Dowans.

Na maamuzi yao huko Dodoma tunayasubiri kwa hamu kweli kweli.
 
Kuna mwenye tetesi zozote kilichojiri kwenye kikao cha CCM Dodoma kuhusiana na malipo ya Dowans atujuze hapa?????????????
 
Serikali inapowaibia wananchi wake mpaka hapo hawana kabisa uhalali wowote kuendelea kuongoza!!
 
Tatizo kuna watu wamebaka fani wanafikiri fedha za serikali ni za bibi zao.
Wanashindwa kujifunza kutoka kwenye ishu ya epa wanarudia makosa akili zao fupi kama maisha ya funza na wanaona waliposimama tu wakidhani wananchi wote ni vipofu. Nadhani wanataka kama yale YaTunisia. Wanadhani wao ndo mpango mzima, kumbe wanaizika nchi kidogo kidogo yaani kiungo kimoja baada ya kingine.
 
Kweli Kama Watanzania Tutakaa Kimya na kuacha Dowans walipwe ni kupigwa risasi vichwani sote. Hivi haya yote tunayachukua na kwenda kulala...mimi binafsi nataka hatua ichukuliwe na wananchi tunao uwezo...wapi na nini tufanye....
 
Naona kama tamko la UVCCM si kipindi kirefu sana litageuka petroli ya kukichoma kabisa chama chao na kutoweka kwenye ramani nchi yetu.

Walidhani wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini ni wajinga kiasi hicho kiasi cha kudanganyika na ghiliba za watoto wasiokua na maamuzi serikalini na ambao siku zote walikua kimya kama maji ya mtungi wakati CCM ikukwapua fedha za mikopo kwenda kuchakachulia uchaguzi wetu 2010?

Ujanja wa KIKWETE KURUDISHA HOJA YA DOWANS BUNGENI ili kuwakomoa wabunge wa CCM Uadilifu tulishaufahamu siku nyingi na wala nafasi hiyo kamwe hawapati.

Na matusi waliomfurumshia Dr Slaa kwa Umma wa Tanzania basi ndio kaburi la chama hicho. Uamuzi mgumu uliobaki ni kujiuzulu kwa Kikwete na serikali yake basi!!
 
kwa kuwa wote tuikubai kuvaa T-Shirts na Kofia,vyakula vya bure na ngonjera na nyimbo za wanamuziki kama MALLO haina namna inabidi fedha hizo zilipwe ili kuipatia CCM ahueni maana iko hoi bin taabani kifedha.
 
Mkuuu nami hapo ndipo nilitaka kujua CCM wapo ki CCM zaidi au Kiserikali zaidi wanapo taka madaraka huwa wanapiga Domo sana lakini kwa hili la matatizo wako wapi Je wanafurahii hili la TANESCO kuongeza bei ya umeme?? Je wanafurahi Serikali inaongozwa na CCM kulipa pesa yote hiyo ya walipa Kodi ukizingatia wana CCM nao inawahusu mbona hili Makamba wa Kinana kuliijia juu na kuikanya serikali walio ipa Uongozi kwa kupitia NEC kuwa hili sio jamani???

Na kwanini Hao wanao tajwa kuhusu DOWANA RA,EL,RAU_MASHA,MKONO wasijitokeze kuwa wao sio wamiliki maana wanachafuliwa majina na wanakaaa kimya kwanini???


Uso umeumbwa na haya ndugu yangu!!!!
 
Mbona CCM yenyewe inajifahamu kuwa hadi sasa waliokuwa wanachama wake wamepoteza imani kabisa?
 
Ni habari endelevu. Walivyo wehu na wenda wazimu CCM na Serikali wanaweza kuwalipa Dowans kinyume cha ukweli, haki, matwawa ya wenye nchi.

Jeuri kama hiyo ndio itawafanya watu wengine kuona kwa urahisi zaidi CCM na hatma yao na vizazi vijavyo. Je wana matumaini yoyote ya kuishi katika nchi huru yenye kumjali, kumsikiliza na kumwendeleza mwananchi wake? Aau ni kundi la wajanja & wahuni ambao wameshawahi seat na gari ndio limeondoka.

Kifupi, ishara zote zaonyesha Kikwete anataka na amedhamiria kuilipa/kujilipa kupitia Dowans....lakini ingalipo siku ya leo let's us join arm and proceed with fighting for Tz.
 
kwa kuwa wote tuikubai kuvaa T-Shirts na Kofia,vyakula vya bure na ngonjera na nyimbo za wanamuziki kama MALLO haina namna inabidi fedha hizo zilipwe ili kuipatia CCM ahueni maana iko hoi bin taabani kifedha.
Umesahau kidogo jambo moja; na kuwekewa KIPINDI MAALUM CHA VICHEKESHO (akina masanja) huku wajanja wakipakua rasilmali ya taifa kwa tani yao kuingia mifuko binafsi na kuhifadhiwa salama zaidi USWISI.
 


Katiba ni SHERIA MAMA ambapo sheria zote za nchi hupatikana na kufanyiwa kazi.

Wakati sheria za kawaida hutungwa na wawakilishi wa wananchi kwa maana ya Wabunge kule bungeni Dodoma, Katiba ni sheria mama yenye UPEKEE KATIKA JAMII HUSIKA ambapo utungaji wake ni JUKUMU LA RAIA WOTE katika nchi.

Sasa Ugomvi mkubwa kati ya vyama vya upinzani na Wanaharakati, kwa upande mmoja, dhidi ya CCM ni katika kusema kwamba NI HAKI YA KILA MTANZANIA KUSHIRIKI MOJA KWA MOJA katika kutekeleza wajibu wao kutunga Katiba Mpya.

Lakini wao CCM wakiongozwa na Mafisadi wao wanasema Rais ANATOSHA KUTUTUNGIA TU KATIBA KWA KUSHIRIKIANA NA LOWASA, CHENGE na akina ROSTAM AZIZI kututungia tu katiba hiyo kupitia KIKUNDI CHA MADALALI WAO KWA JINA LA WATAALAM WALIOBOBEA KWENYE SHERIA.

Sasa swali hapa ni kwamba; tangu lini Watanzania tukasikia KIKUNDI CHA Mi-FISI wakatunga sheria murua ya kulinda maslahi ya SWALA jangwani???

UWEZO TUNAO, haki hapewi mtu bali ni kwamba haki hufuatwa na kuchukuliwa. Kazi inaendelea kila kona ya nchi kwa watu tunaojali maslahi ya taifa letu. Hakuna kulala!!!
 
Back
Top Bottom