Mtego wa CCM Kujilipa Kupitia Dowans na Tafsiri ya Wapiga-Kura 'TALAKA TOKOMEA'!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtego wa CCM Kujilipa Kupitia Dowans na Tafsiri ya Wapiga-Kura 'TALAKA TOKOMEA'!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Chief Rumanyika, Dec 29, 2010.

 1. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #1
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haijalishi taasisi gani (ICC) imesema Wa-Tanzania wkupitia TANESCO tukamplipe Dowans Billioni 185, kama hatuwezi kujuzwa wamiliki wake wazi wazi, mkataba wenyewe ulivyokua, na nyaraka zote za kesi, basi sisi kama walipa kodi tunahaki ya kuyagomea malipo hayo.

  Lakini, kwa kuwa AG Werema kama msimamizi wa sheria zetu na utekelezaji wake ndio wakwanza kukimbilia kusema DOWANS KULIPWA NI LAZIMA na kwamba Jalada la Wananchi sisi kutaka majibu zaidi anadai kufunga mjadala bila sisi kuridhi, haifai hata kidogo.

  HOJA YANGU JUU YA HILI:

  Hoja yangu hapa sasa ni kwamba siku SERIKALI YA CCM ikichukua hatua ya kulipa mikataba ya Dowans ambayo hatujaridhika nayo, licha ya madai kwamba ni mali ya CCM kupitia EL na RA kwa ajili ya kuhongea uchaguzi, basi ieleweke kwamba siku hiyo ndiyo WATAKUA WAMEANDIKA RASMI TALAKA TOKOMEA kwetu sisi wapiga kura katika uhai wote wa chama hicho.

  Wananchi kutokusikilizwa ni dhambi kubwa, kupuuzwa ni uhaini, na kutokupewa majibu juu ya mambo yanayotuhusu ki-ulipaji kodi ni kutokomeza kabisa uhusiano. CCM angalieni vizuri mtego huu!!!
   
 2. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2010
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wapi Waria KInana na mgosi Makamba?
  Wapi Malaria Sugu?
  Wapi mwenyekiti wa watanzania New York aliejigamba kupewa $ 2000 na mheshimiwa Pinda na kudai CCM ni safi?
   
 3. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Changuo liko mkononi mwao CCM ama kujinyonge hili kamba la Dowans sasa hivi tu au vinginevyo. Tunashukuru sana mtego huu wameusuka wenyewe tu na wa kunasia mle ndani si mwingine.

  Wa-Tanzania wapiga kura sasa tuko pembeni baada ya Werema KUJITANGAZIA KUFUNGA mjadala wa walipa kodi kuvurumsha maswali kutaka kujua mambo mengi sana kabla ya malipo yoyote kwenda Dowans.
   
 4. S

  Sheka Senior Member

  #4
  Dec 29, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi sisi watanganyika hutuwe kujipanga tukawashitaki hawa akina RA, EL na Visenti kwa mashirika ya kimataifa pamoja na wafadhi wanao saidia bujeti yetu wakawekewa vizuizi vya kwenda ughaibuni ikiwa nipamoja kuzifilisiwa account zao zote za nje pamoja za hapa nchini? Tuamke watanganyika kumtetea huyu mama yetu.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,131
  Trophy Points: 280
 6. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #6
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sheka, hayo yote unayoyasema ni tano.

  Sita ya CCM kuondoka madarakani hivi sasa inaandaliwa rasmi na CCM yenyewe. Kaburi lilishachimbwa sasa hivi kupigwa tu plasta vizuri na kuendelea kumtizamia MAREHEMU HUYU MTARAJIWA analetwa lini tukamalize kabisa kazi bila lawama.

  Nadhani unanisoma hapo.
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Yaani unataka kusema tuwashitaki RA na EL na kumwacha mhusika mkuu ambaye uwezo wote wa kuwawajibisha uko mikononi mwake kikatiba, kiserikali na kichama. Mbona tunadanganyana hapa ?
   
 8. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #8
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr Dr Dr Jakaya Mrisho Kikwete mtoto CCM kumfia mkononi. Wakati wa kukabidhiwa mtoto huyu wala hakukuepo na malalamiko makubwa saana afya kuwa na migogoro.

  Lakini pale tu alipoanza kuacha mtoto CCM kupewa uji nyumba ya jirani kule Igunga na Monduli ndipo kuhara na kutapika kulikoanzia. Tangu wakati huo mtoto huyu CCM ugonjwa wake wa kukohoa sana damu hakujatulia wala kusikia dawa.

  Mhe Ole-Sendeka alijaribu kuleta dawa aina ya 'Sokonoi' kusaidia japo kidogo, almanusura mgonjwa akate roho. Mwakyembe akaleta maji ya alfajiri ya migomba michanga toka kule Tukuyu, ajabu almanusura walinzi wa mgonjwa wakambugize sumu ya panya. Mama Kilango kajaribu kuleta maji ya tangawizi ya kuzuia wizi aliyoyapata toka kule mlimani lakini wapi??

  Hamad Rashi alidaiwa kuleta karafuu kufukizia na Mama Maghimbi kuleta vijumba vya konokono baada ya kupiga mbizi yeye mwenyewe mpaka kina kirefu usawa wa viwanja vitatu vya mpira kwenda chini kwani maradhi yalitulia huko???

  Ama kweli sikio la kufa halisikii dawaaaaa!!!
   
 9. Sailor Boy

  Sailor Boy Senior Member

  #9
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 105
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh kweli wa tz siye wapumbavu:eek:
   
 10. P

  Percival Salama Senior Member

  #10
  Dec 29, 2010
  Joined: Feb 3, 2010
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Waliochimba shimo watatumbukia wenyewe!
   
 11. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #11
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa umenena, shimo hili si mwingine bali ni Mzee Ruksa mwenyewe na makundi ndani ya CCM, wanamtandao wakalipiga plasta saafi, na Makamba na busara zake nzito nzito akachanga sanda hapo, ukweli ndio huo.
   
 12. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #12
  Dec 29, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtanzania akituli na kukupa nafasi ukafanye purukshani zako zote weee wala mtu hakawii kumuchukulia MSUKULE kumbe jaama wee, hhheeeee!!!
   
 13. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #13
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani hapo hata mimi sijaelewa hata kidogo mantiki ya huyo mchangiaji.
   
 14. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #14
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Percival Salam, hebu fafanua kauli yako hiyo hapo juu kwani bado haujaeleweka.
   
 15. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #15
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DOWANS HATUWALIPI HATA SENTI MOJA MAANA MADAI YAO YANATOKANA NA MKATABA BATILI ULIOSAINIWA NA KAMPUNI HEWA YA RICHMOND DEVELOPMENT CORPERATION.

  Kwa kuwa uhusiano wa kikazi uliopo sasa hiv kati ya Kampuni moja iitwayo Dowans na Shirika letu la TANESCO linatokana na KURITHISHWA kwake MKATABA na RICHMOND DEVELOPMENT CORPORATION ambayo ilithibitishwa kuwa ni BATILI kwa kuwa MKATABA hauwezi ukasainiwa na Kampuni hewa, ukweli huu peke yake ni sababu tosha ya kutusaidia walipakodi Tanzania tusilipe hata thumni katka hiyo bilioni `185.

  Ikibidi, shitaka la kuabisha zaidi huenda likafunguliwa huko huko ICC. Katika kesi hiyo mshitakiwa wa kwanza huenda akawa ni Mwanasheria Mkuu, Waziri Ngeleja, na Bodi ya TANESCO ili ukweli wote ujulikane kweupe.


  MAONI YA MWANA-JF, 'MASANJA:

  Nimeisoma hukumu ya ICC/msuluhishi/arbitrator kati ya TANESCO na DOWANS lakini kwa mtu yeyote mwenye uelewa wa sheria, ni hakika facts zote hazikutolewa. Na nina mashaka kwamba kulikuwa na collusion kati ya mshtaki na mshtakiwa..(walikuwa kitu kimoja)..ilmradi hiyo pesa ilipwe na hela za walipa kodi. Maana ile decision ukiisoma unaona kwamba wahusika walifanya njama. Yaani ni yale yale ya Radar na ile hukumu ya juzi pale London (maana BAE walikubali kosa through plea bargaining na kulipa faini..ilmradi mahakama isiandike kwenye hukumu neno "corruption"..yet kwetu huku Tanzania tumeambiwa vingine kabisa!. Nitajitahidi kuzi-summarize niziweke hapa kwa lugha rahisi wananchi mzisome. Maana nadhani watu tumeshafanywa wajinga kabisa as if hatukwenda shule.

  From my judgement..huu mkataba (TANESCO na DOWANS) haukuwepo..PRECISELY BECAUSE THE CONTRACT WAS BUILT ON ILLIGALITY..WHICH NULLIFIED ITS ENFORCEABILITY FROM THE TIME IT WAS CONCLUDED. Na uwezo wangu mdogo lakini naelewa kabisa..kama mkataba umeafikiwa kwa hila au udanganyifu hauwezi kuwa mkataba halali.....Clearly, Mwakyembe alituandalia report. (ambayo ilimuondoa Lowassa).....na wengi tuliisoma..tunajua kabisa Richmond haikuwepo..ilikuwa ni kampuni hewa. Kwa hiyo isingeweza kurithisha mkataba kwa DOWANS kwa sababu tayari huo mkataba haukuwepo kisheria! Huhitaji PhD ya International Law kutoka Stanford au Cambridge kulijua hili. Nina imani hata WEREMA analitambua hili..ila anacheza na fikra zetu watanzania.

  Mwanzoni wengi tulikaa kimya kwa sababu tulijua ni mambo ya kisheria yatamalizwa kisheria. Lakini ukweli ni kwamba, its politics vs. politics. Yaani hapa..kesi ya TANESCO ilikuwa rahisi sana. Maana wale waliosign mkataba walidanganya from the biggining..kitu ambacho hata polisi ni kosa la jinai. Unfortunately nilichogundua it is highly likely huu mkataba ni " deal" la watu kwenye "system". Lakini kinachouma ni kwamba..wanaoumia ni sisi wananchi wa kawaida..ambao tunahangaika kila kukicha na haya maisha kwa sababu ya watu wachache sana. Mimi nadhani kwa kweli serikali yetu na wanasheria wetu hawajatutendea haki kabisa they should be ashamed of themselves. I have read the judgement na naona TANESCO wanted to loose from the beggining.

  Hivi kweli kama taifa ambalo kila siku tunashinda kuomba vyandarua vya malaria....kwa akina Ray Chambers....tumeamua kuukubali huu udhurumaji kirahisi rahisi hivi? Hivi ni kweli tumekubali kulipa Billion 185 (na kuendela mpaka deni litakapolipwa) kwa Kampuni hewa? Mimi naomba viongozi wetu especially Raisi wetu na wabunge waache mzaha...This is serious its not politics anymore..its about the survival of the nation and its people. Na huu umasikini unaotukabili ni dhihaka ya hali ya juu kuambiwa tulipe hizo billions wakati hata sasa umeme hatukupata na wala mpaka leo hatuna! Jamani hivi viongozi wetu kwa nini wanakuwa wagumu kuelewa au wanafanya maksudi? Please Kikwete stop this! It pains. To all men and women in this poor country called TANZANIA.

  Kwanza kabisa hii Kampuni hatujui mmiliki wake..kila mtu hata RAIS wetu wako kimya kuhusu nani mmiliki halali wa hii kampuni, sasa hiyo hela tunamlipa nani? Au viongozi wetu wamekula njama ya kutudhulumu sisi raia? Wanachokifanya ni kutwambia mjadala umefungwa? Jamani hizo pesa ni kodi zetu tuna kila haki ya kuhoji matumizi yake. Na hii siyo kutafutana ugomvi. Ni haki yetu ya kiraia kabisa. Sisi kama raia wa Tanzania TUNAHUKUMIWA kwa sababu eti tulivunja mkataba wa kufua umeme. Lakini tuliuvunja na nani? huyo mwenye kampuni kwa nini asijitokeze hadharani? Sisi wananchi ambao tunalala gizani tukamuuliza maswali? Maana viongozi wetu wana majenereta hawajui dhahma na kero ya huu umeme wa Tanzania. Cha kusikitisha zaidi huo umeme hatukupata hata wa kuwasha balbu moja ya jikoni! Leo tunaambiwa tulipe hayo mabilioni kwa taifa ambalo halina nyuma wala mbele.

  Jamani mimi nadhani Watanzania sasa tuache ushabiki wa kisiasa tujipange kuuliza maswali magumu kwa hawa watawala wetu ambao wanaiendesha nchi yetu kama kampuni binafsi ya Mohamed Enterprises. Its tragic kweli kabisa sisi kama taifa kusimama na kusema kwamba tuna uhuru wakati hatuwezi hata kuamua au kutambua kipi kinatufaa kipi hakitufai.Inauma Kuona kwamba wale tunaowaamini ndo wanatuzunguka na kutufanya sisi ni wajinga. Nimemsikiliza Werema Jaji Mkuu..nimesikitika sana...kuona mwanasheria mkuu kama yeye anaweza toa kauli kama zile as if haijui sheria. Watu tunaweza kuwa na imani tofauti ya kisiasa. Lakini kuna mambo ambayo lazima tufike mahali tuyapiganie kwa maslahi ya hili taifa letu.

  As we move forward nategemea Rais wetu atakuja na kutoa kauli thabiti dhidi ya huu udhurumaji wa mchana kweupe...Please Mr. President..stand up and be counted....tunalalamika kila siku mikataba mibovu..but ultimately the buck stops at your table..maana wewe ndo kiranja mkuu na baba mkuu mwenye nyumba.

  Kama vipi..mimi nitajitolea BURE kuandika LEGAL OPINION kwenye hii HUKUMU YA ICC kati ya DOWANS na TANESCO kumshauri Rais wetu afanye nini baada ya hapa.... Kama aliyepewa hilo Jukumu haliwezi. I am ready to do it..for the sake of my country and its people. Tunasoma tuwezi kulisaidia taifa letu. Sasa kama hatuwezi hata kutetea maslahi ya taifa at its hour of need, ni usaliti.

  I challenge my fellow compatriots. Lets stand up and say no to this day time robbery of our hard earned shilling.
   
 16. C

  Chief JF-Expert Member

  #16
  Dec 30, 2010
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,490
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160


  The thing is, hatakusikiliza. Hakuna njia ambayo kama individual unaweza kuchukua legal action against hii judgement, badala tu ya kuishia kutoa "legal opinion"? Nipo radhi kuchangia move ya namna hii.
   
 17. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #17
  Dec 30, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mkuuu nami hapo ndipo nilitaka kujua CCM wapo ki CCM zaidi au Kiserikali zaidi wanapo taka madaraka huwa wanapiga Domo sana lakini kwa hili la matatizo wako wapi Je wanafurahii hili la TANESCO kuongeza bei ya umeme?? Je wanafurahi Serikali inaongozwa na CCM kulipa pesa yote hiyo ya walipa Kodi ukizingatia wana CCM nao inawahusu mbona hili Makamba wa Kinana kuliijia juu na kuikanya serikali walio ipa Uongozi kwa kupitia NEC kuwa hili sio jamani???

  Na kwanini Hao wanao tajwa kuhusu DOWANA RA,EL,RAU_MASHA,MKONO wasijitokeze kuwa wao sio wamiliki maana wanachafuliwa majina na wanakaaa kimya kwanini???
   
 18. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #18
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika 'Chief', taifa letu kwa kukosa uongozi bora, busara, na uwezo wa kujizuia nafsi tamaa za kidunia za kupata kingi na zaidi. Hebu fikiria kwa juhudi zote chafu hii ndio tena habari nyeti kati duru za ndani ya serikali zinasema kuna mpango wa siri mno Raisi sasa kutoroka nchi kupiti kwa Prof Bingu wa Mutharika.

  Ndani tu ya mwezi mmoja keshachanja mbuga mara mbili huko. Na unafikiri hela zinazoendelea kutoroshwa nchi hadi dakika hii zitakua ni shilingi ngapi? Kwa kweli mwakani huko na kwa kuendelea sipati picha maisha yatakua magumu kiasi gani hasa vijijini.
   
 19. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #19
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jethro, mambo ni mawili hapa kwamba kwa ukimya huu unaoziba masikio kwa upande wa CCM kama chama kuzungumzia hii hasara ya mwaka kwa taifa la bilioni 185 kwa taifa masikini kama yetu, ina maana chama hiki kipo madarakani kimaslahi binafsi zaidi na wala si kwa manufaa ya wananchi wa taifa hili.

  Pili, kwa lugha ya mwili wa ukiya wanaoonyesha waheshimiwa hawa wanaodaiwa kumiliki Dowansi moja kwa moja ni kwamba wamekiri bila ya kutumia maneno ya kwamba wezi wetu si wengine tofauti bali ni wao tu hapa.
   
 20. C

  Chief Rumanyika Senior Member

  #20
  Dec 30, 2010
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sheka, najua unazungumzia tu uchungu ulionayo juu ya nchi yetu inavyoporwa. Leo hii hata ukisema ukawashitaki hawa waheshimiwa ndiyo hivyo kila siku kwa Chenge, hata apatwe na kesi hatari kama nini, kesho yake tu unasiki CHENGE APATA HUKUMU YA FURAHA. Unaona hilo???
   
Loading...