Mtifuano mkali baina ya viongozi wa CCM na Serikali kuhusu mipaka ya kazi na uwajibikaji wa Viongozi hao unaleta ukakasi

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Mtifuano mkali katikati ya majira tete ya chaguzi za 2024 na 2025 baina ya viongozi waandamizi wa CCM na serikali yake kuhusu mipaka ya kazi na uwajibikaji wa viongozi hao unaleta ukakasi na tafsiri ngumu ya hali hiyo isiyo adhimu tangu Februari 5, 1977.

Tambo, jazba, kujiapiza, kupiga ngumi vifua, vidole juu, kukunja ndita, kugonga meza kwa ngumi, istilahi na misamiati mikali isiyohaririwa vimetumiwa katika majibizano kwenye hadhira zinayotarajiwa ziombwe kura 2024 na 2025.

Hayo yanafanyika wakati Kamati ya Maadili ya CCM inayoogopwa kuliko Mahakama ya Rufaa, Kamati ambayo ina nguvu za turufu, ikiangalia tamthilia hii bila kutia neno wala kujuwa namna ya kutabiri mwisho wake.

Chama kinathibitisha kuwa na misuli juu ya serikali na serikali nayo kupitia walioingia kwenye mtanange huu inathibitisha kuwa na misuli juu ya chama.

Hali hii ni abracadabra inayofanya wanachama na wapiga kura washindwe kutofautisha Punda na Pundamilia kwenye tabia na hulka zao (achilia rangi zao), wengine wakitabiri kwamba unaweza pia hata kumfuga Pundamilia nyumbani na Punda naye akaishi porini.

Nijuavyo mwelekeo wa siasa za JMT, naona kabisa SSH 2026 anaenda kubadilika na kuwa Magufuli 100% kwamba tujiandae kisaikolojia.

Miaka hii 4 amesoma watu na kuwaelewa vizuri, amekulia urais kwa miaka 9 sasa, na ikizingatiwa kwamba 2026 itakuwa ndiyo anaanza awamu yake ya mwisho kwa mujibu wa Katiba zote.

Mahesabu ya upatikanaji wa PCM (Paul Christian Makonda) ni makali na yametumia mbinu za QQT (Quantitative and Qualitative Technics) kuliko mahesabu ya kumpata Nchimbi ambayo yamezingatia tu uanamtandao.

Ukimbeza na kumkataa Punda leo kwa kumtaka Pundamilia, ujuwe kwamba tunaweza kununua Gold Star tukampaka Punda rangi za milia ili umpende lakini 2026 tukamfutia milia ili kumrudishia rangi yake ya asili ya Punda alafu ukajikuta unatafuta ukimbizi nje ya nchi.

Ninashuhudiwa kabisa kuwa katika mchakato wa mama kujibadilisha kuwa Complete-Metamorphosis-Magufuli 100% 2026 kubali ukatae anahitaji Waziri Mkuu toka Usukumani na among PM materials hawa hawakosekani:-

1. Paul Christian Makonda PCM.

2. Luhaga Mpina (kwenye siasa hakuna uadui wa kudumu bali maslahi ya kudumu)

3. Dotto Biteko (Sundries)

Bila 1 na 2 au mwingine toka Usukumani ambaye pia ni fire-brand, mabadiliko ya mama kuwa Complete-Metamorphosis-Magufuli 100% 2026 yata-abort na ndipo hali ya kisiasa ya nchi na uchumi wake vitakuwa kama Ugiriki. ‭Mk‬.3:25‬ ‭na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama.

Niwashauri warasimu wa serikalini wasiojuwa kutofautisha Punda na Pundamilia wajisahihishe mapema hata kwa kumuendea inbox PCM badala ya kuendelea kung'ang'ania kuhoji MUNGU aliwaza nini na kumaanisha nini kuumba kitu kile kile mara 2 (Punda na Pundamilia).

Rt. Hon. Raila aliunda Deep State ambayo ndiyo ilikuwa ikiongoza serikali yeye akiwa kinara wa upinzani. Akajihakikishia na dunia pia 100% kuwa safari hii ya 7 anashinda uchaguzi na kuwa rais na amiri jeshi mkuu wa Jamhuri ya Kenya.

Yule Makonda (Ruto) aliyetengwa na Uhuru na Raila kwenye Deep State akilipwa mshahara wa Makamu Rais kwa kusoma tu magazeti na kurudi kulala nyumbani kwa miaka 4 bila kuhudhuria hata kikao kimoja cha baraza la mawaziri wala bila kufanya ziara hata 1 ya kiserikali akaja kuwa huyo aliyekuwa leo.

Asomaye na afahamu, asikiaye na aelewe, mwenye kiburi na azidishe kiburi chake.
 
Mtifuano mkali katikati ya majira tete ya chaguzi za 2024 na 2025 baina ya viongozi waandamizi wa CCM na serikali yake kuhusu mipaka ya kazi na uwajibikaji wa viongozi hao unaleta ukakasi na tafsiri ngumu ya hali hiyo isiyo adhimu tangu Februari 5, 1977.

Tambo, jazba, kujiapisha, kupiga ngumi vifua, vidole juu, kukunja ndita, kugonga meza kwa ngumi, istilahi na misamiati mikali isiyohaririwa vimetumiwa katika majibizano kwenye hadhira zinayotarajiwa ziombwe kura 2024 na 2025.

Hayo yanafanyika wakati Kamati ya Maadili ya CCM inayoogopwa kuliko Mahakama ya Rufaa, Kamati ambayo ina nguvu za turufu, ikiangalia tamthilia hii bila kutia neno wala kujuwa namna ya kutabiri mwisho wake.

Chama kinathibitisha kuwa na misuli juu ya serikali na serikali nayo kupitia walioingia kwenye sintojuwa hii inathibitisha kuwa na misuli juu ya chama.

Hali hii ni abracadabra inayofanya wanachama na wapiga kura washindwe kutofautisha Punda na Pundamilia kwenye tabia na hulka zao (achilia rangi zao), wengine wakitabiri kwamba unaweza pia hata kumfuga Pundamilia nyumbani na Punda naye akaishi porini.

Nijuavyo mwelekeo wa siasa za JMT, naona kabisa SSH 2026 anaenda kubadilika na kuwa Magufuli 100% kwamba tujiandae kisaikolojia.

Miaka hii 4 amesoma watu na kuwaelewa vizuri, amekulia urais kwa miaka 9 sasa, na ikizingatiwa kwamba 2026 itakuwa ndiyo anaanza awamu yake ya mwisho kwa mujibu wa Katiba zote.

Mahesabu ya upatikanaji wa PCM (Paul Christian Makonda) ni makali na yametumia mbinu za QQT (Quantitative and Qualitative Technics) kuliko mahesabu ya kumpata Nchimbi ambayo yamezingatia tu uanamtandao.

Ukimbeza na kumkataa Punda leo kwa kumtaka Pundamilia, ujuwe kwamba tunaweza kununua Gold Star tukampaka Punda rangi za milia ili umpende lakini 2026 tukamfutia milia ili kumrudishia rangi yake ya asili ya Punda alafu ukajikuta unatafuta ukimbizi nje ya nchi.

Ninashuhudiwa kabisa kuwa katika mchakato wa mama kujibadilisha kuwa Complete-Metamorphosis-Magufuli 100% 2026 kubali ukatae anahitaji Waziri Mkuu toka Usukumani na among PM materials hawa hawakosekani:-

1. Paul Christian Makonda PCM.

2. Luhaga Mpina (kwenye siasa hakuna adui wa kudumu bali maslahi ya kudumu)

3. Dotto Biteko (Sundries)

Bila 1 na 2 au mwingine toka Usukumani ambaye pia ni fire-brand, mabadiliko ya mama kuwa Complete-Metamorphosis-Magufuli 100% 2026 yata-abort na ndipo hali ya kisiasa ya nchi na uchumi wake vitakuwa kama Ugiriki. ‭Mk‬.3:25‬ ‭na nyumba ikifitinika juu ya nafsi yake, nyumba hiyo haiwezi kusimama.

Niwashauri warasimu wa serikali wasiojuwa kutofautisha Punda na Pundamilia wajisahihishe mapema hata kwa kumuendea inbox PCM badala ya kuendelea kung'ang'ania kuhoji MUNGU aliwaza nini na kumaanisha nini kuumba kitu kile kile mara 2 (Punda na Pundamilia).

Raila aliunda Deep State ambayo ndiyo ilikuwa ikiongoza serikali yeye akiwa kinara wa upinzani. Akajihakikishia na dunia pia 100% kuwa safari hii ya 6 anashinda uchaguzi.

Yule Makonda (Ruto) aliyetengwa na Uhuru na Raila kwenye Deep State akilipwa mshahara wa Makamu Rais kwa kusoma tu magazeti na kurudi kulala nyumbani kwa miaka 4 bila kuhudhuria hata kikao kimoja cha baraza la mawaziri wala bila kufanya ziara hata 1 ya kiserikali akaja kuwa huyo aliyekuwa leo.

Asomaye na afahamu, asikiaye na aelewe, mwenye kiburi na azidishe kiburi chake.
Ndio uhai wa Chama,sio kama kile chama Cha nyumbu upande ule
 
Back
Top Bottom