Mtazamo wangu:Siku mia moja za JPM

aminiusiamini

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,577
2,221
Kwanza Shukrani kwa Jamiiforums kwa kutuletea hii platform ya pekee kabisa,kujadili masuala mengi kwa mapana kuhusu jamii zetu,nchi yetu kipenzi,siasa nk.Hawa jamaa wanastahili pongezi kwa kudumisha demokrasia nchini na pia kufumbua watu mambo mengi,ambayo hayakuwa yanajulikana kwa muda mrefu.

Napenda kuzungumzia kuhusu siku 100 za Magufuli kwa ufupi sana.Kuna mengine nitasema bila maelezo ya kina,lakni,sitaki tuchoshane kwa mistari mirefu ambayo najua watu wengi hawapendi kusoma.
Naweza kusema,tulianza vyema mwaka katika siasa zetu hasa kwa upande wa bara kwa Amani pamoja na kuwepo kwa mambo mengi,hasa kuhusu uchaguzi,mabishano ya hapa na pale kuhusu uchaguzi mkuu.
Tanzania kwa muda mrefu ililkuwa inahitaji kiongozi kama MAGUFULI mwenye msimamo,na kuweza kufanya kazi kwa haraka.Mimi pamoja ni mshabiki wa lowassa,lakni nimeona ni bora MAGUFULI alivyopitshwa kuliko au kama angepita Lowassa katika kinyan'ganyiro hicho.

Magufuli,ni mtanzania anayependa nchi yake na nia nzuri anayo kwa nchi yake,sema mkuu huyu hana vision kabisa,wala hajui nini afanye;namfananisha na mchezaji wa mpira anayeranda randa uwanjani hajui acheze vipi,mbele au nyuma,au awe golikipa.Nasema hivyo sio kumkashifu ila kwa kujadili ni namna gani anaweza kubadili mchezo kwa kusikilza maoni ya watanzania na sekta binafsi na waataalamu wengi kuliko kuendelea kuwasikiliza wale wazee waliotufikisha hapa kama Kikwete,Mkapa na wengineo.

Magufuli bado anawaza kuwa,anaweza kushinda mchezo huu kwa technicalities hizi hiz tulizonazo,formation hihi tuliyonayo na watu wale wale katika kuleta maendeleo Tanzania yetu hilo unajidanganya.Magufuli alianza vizuri kwa kumchagua waziri mkuu MAJALIWA.Baada ya sokoine,hakuna waziri ambaye amewajibika kwa kiwango cha kuridhisha sana na huyu ni mtu pekee ambaye raisi magufuli anatakiwa kumwamini.

Raisi,asitegeeme CCM ndio itampa maarifa au ushauri katika mambo ya msingi na yanayohitaji kutatuliwa kwa haraka sana.Suala la rushwa liko kwenye mizizi ya chama.Raisi,ameamua kuwashughulikia watu wadogo sana kwenye hiii vita ya rushwa na kuwaacha wakubwa kwa kuona aibu au kwasababu wapo kwenye chama.Vta dhidi ya rushwa,bado naona inahitaji uwanja mpana bila kuangaliana uso wala majina.Kwa hapa naona raisi bado hajakamata watuhumiwa wote ambao ni wakubwa na tunawajua.Hapo juzi change aliteuliwa kuwa kiongozi wa bunge,nilijiuliza sana kwa usafi gani alio nao?na je,ndio hawa watu magufuli anataka kufanya nao kazi? watu kama MWAKYMBE,MUHONGO nk hawa watu hawafai hata kidogo ni wachafu.

Lazima kwenye ukweli tutasema.Mfano,uzwaji wa nyumba za serikali ni suala ambalo raisi magufuli anatakiwa kulivalia njuga kama alivyowanyanyasa watu wa jangwani basi na wale wa masaki na oysterbay kiama chao kije kwa knunua nyumba za serikali kwa mazingira ya rushwa na yasio ya haki kwa watanzania wote.Pia nimkumbushe raisi magufuli kuwa,aache unafiki,nayeye arudishe zile nyumba zake nne pale masaki kwa serikali,ili serikali ijue itfanya nini nazo na kama kuuza,ziuzwe kwa bei halali na sio milioni 20.

Nachotaka kusema kwa msisitizo kuwa,raisi magufuli asiwe kama mkapa kwa kula na watu ndani ya circle yake bali awe muwazi na mkweli na kufanya mambo ya misingi ya haki bila kujali tikadi za chama au mtu mmmoja moja,maana aliapa kwa Mungu na watanzania.
Magufuli asitegeme kufaulu kwenye system mbovu tuliyonayo hii.Katiba ni kiungo muhimu sana katika kuleta na kubadilisha mtazamo na dira ya nchi.Suala la kubadili mfumo,katiba ni misingi ya kwanza kabisa Magufuli atakiwa kuanzia kuliko kufufua air Tanzania,kutaka viwanda vijengwe overnight au kufunga kila mtu mwenye ubathirifu.Lazima tuanze na ugonjwa ulipo na kutibu.
 
Umeandika vizuri; ni maoni yako na mimi nakubaliana na wewe kwa asilimia 85 hivi. Hata hivyo tarajia madongo toka kwa wachangiaji wavivu wa kusoma makala.
 
Mie niseme Rais ameanza vyema,angekuwa hana vission sidhan kama mabilion aliyoyarejesha angejua yalikofichwa,asingerejesha moyo wa kulipa kodi,asingerejesha moyo wa uwajibikaji,sasa hivi wafanyakazi wa umma wanapatikana ofisin muda wote wa kazi.BInafsi niseme hayo uliyoyasema ni mhimu kati ya mhimu zaidi aliyoanza nayo,mchakato wa katiba ni hela sasa utauanzisha fedha zipo kwa mafisadi?,mambo ya hizo nyumba ni suala ama jipu lililowazi lakini kuna.majipu ambayo yalikuwa pabaya zaidi huwezi tumbua yote mara moja.siku mia moja za JPM mwendo wake mzuri
 
Kwanza Shukrani kwa Jamiiforums kwa kutuletea hii platform ya pekee kabisa,kujadili masuala mengi kwa mapana kuhusu jamii zetu,nchi yetu kipenzi,siasa nk.Hawa jamaa wanastahili pongezi kwa kudumisha demokrasia nchini na pia kufumbua watu mambo mengi,ambayo hayakuwa yanajulikana kwa muda mrefu.

Napenda kuzungumzia kuhusu siku 100 za Magufuli kwa ufupi sana.Kuna mengine nitasema bila maelezo ya kina,lakni,sitaki tuchoshane kwa mistari mirefu ambayo najua watu wengi hawapendi kusoma.
Naweza kusema,tulianza vyema mwaka katika siasa zetu hasa kwa upande wa bara kwa Amani pamoja na kuwepo kwa mambo mengi,hasa kuhusu uchaguzi,mabishano ya hapa na pale kuhusu uchaguzi mkuu.
Tanzania kwa muda mrefu ililkuwa inahitaji kiongozi kama MAGUFULI mwenye msimamo,na kuweza kufanya kazi kwa haraka.Mimi pamoja ni mshabiki wa lowassa,lakni nimeona ni bora MAGUFULI alivyopitshwa kuliko au kama angepita Lowassa katika kinyan'ganyiro hicho.

Magufuli,ni mtanzania anayependa nchi yake na nia nzuri anayo kwa nchi yake,sema mkuu huyu hana vision kabisa,wala hajui nini afanye;namfananisha na mchezaji wa mpira anayeranda randa uwanjani hajui acheze vipi,mbele au nyuma,au awe golikipa.Nasema hivyo sio kumkashifu ila kwa kujadili ni namna gani anaweza kubadili mchezo kwa kusikilza maoni ya watanzania na sekta binafsi na waataalamu wengi kuliko kuendelea kuwasikiliza wale wazee waliotufikisha hapa kama Kikwete,Mkapa na wengineo.

Magufuli bado anawaza kuwa,anaweza kushinda mchezo huu kwa technicalities hizi hiz tulizonazo,formation hihi tuliyonayo na watu wale wale katika kuleta maendeleo Tanzania yetu hilo unajidanganya.Magufuli alianza vizuri kwa kumchagua waziri mkuu MAJALIWA.Baada ya sokoine,hakuna waziri ambaye amewajibika kwa kiwango cha kuridhisha sana na huyu ni mtu pekee ambaye raisi magufuli anatakiwa kumwamini.

Raisi,asitegeeme CCM ndio itampa maarifa au ushauri katika mambo ya msingi na yanayohitaji kutatuliwa kwa haraka sana.Suala la rushwa liko kwenye mizizi ya chama.Raisi,ameamua kuwashughulikia watu wadogo sana kwenye hiii vita ya rushwa na kuwaacha wakubwa kwa kuona aibu au kwasababu wapo kwenye chama.Vta dhidi ya rushwa,bado naona inahitaji uwanja mpana bila kuangaliana uso wala majina.Kwa hapa naona raisi bado hajakamata watuhumiwa wote ambao ni wakubwa na tunawajua.Hapo juzi change aliteuliwa kuwa kiongozi wa bunge,nilijiuliza sana kwa usafi gani alio nao?na je,ndio hawa watu magufuli anataka kufanya nao kazi? watu kama MWAKYMBE,MUHONGO nk hawa watu hawafai hata kidogo ni wachafu.

Lazima kwenye ukweli tutasema.Mfano,uzwaji wa nyumba za serikali ni suala ambalo raisi magufuli anatakiwa kulivalia njuga kama alivyowanyanyasa watu wa jangwani basi na wale wa masaki na oysterbay kiama chao kije kwa knunua nyumba za serikali kwa mazingira ya rushwa na yasio ya haki kwa watanzania wote.Pia nimkumbushe raisi magufuli kuwa,aache unafiki,nayeye arudishe zile nyumba zake nne pale masaki kwa serikali,ili serikali ijue itfanya nini nazo na kama kuuza,ziuzwe kwa bei halali na sio milioni 20.

Nachotaka kusema kwa msisitizo kuwa,raisi magufuli asiwe kama mkapa kwa kula na watu ndani ya circle yake bali awe muwazi na mkweli na kufanya mambo ya misingi ya haki bila kujali tikadi za chama au mtu mmmoja moja,maana aliapa kwa Mungu na watanzania.
Magufuli asitegeme kufaulu kwenye system mbovu tuliyonayo hii.Katiba ni kiungo muhimu sana katika kuleta na kubadilisha mtazamo na dira ya nchi.Suala la kubadili mfumo,katiba ni misingi ya kwanza kabisa Magufuli atakiwa kuanzia kuliko kufufua air Tanzania,kutaka viwanda vijengwe overnight au kufunga kila mtu mwenye ubathirifu.Lazima tuanze na ugonjwa ulipo na kutibu.

Kwa haya maelezo wakija watu wa Lumumba sidhani kama watakuelewa maana wangependa usifie kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Anyway kwa sisi watumishi wa umma tunampongeza kwa kuiweka tarehe ya mshahara fixed! ndani ya hizi siku 100 kila ikifika tarehe 22 unakuta white house tayari tofauti na kipindi cha nyuma.

Kuhusu maisha kwa ujumla ndani ya hizi siku 100 kusema ukweli hakuna unafuu wowote (huenda ni mapema sana kuyaona mabadiliko) na hatuna jinsi, tutaendelea tu kusubiri na kuvumilia. Labda baada ya bajeti ya mwaka huu 2016 kupita tutapata cha kuongea. Ila kwa sasa tunapiga tu kazi.
 
Back
Top Bottom