Ulimsikia Sumaye? Unajua kala ngapi kwenye mradi ule wa maji?Naamini kati ya watoto au wanafamilia wako kuna waliosoma shule za kata, au kufaidi mradi wa maji ya kutoka mto nile. Tusiwe wepesi kupingana na uwezo wa utendaji wa Mh. Lowasa.
Ile Party ya tarehe 1 zilitumika shilingi ngapi? Zilitoka wapi? Kwa malengo gani? Eleza kwa kina utajiri wa Lowasa unatokana na nini. Usitudanganye kwa ving'ombe vya familia na Mungu kumshushia yeye utajiri.Utajiri wa Lowasa ni wa muda tokea kwenye familia, hatakuwa na muda wa kutafuta biashara za familia kama wengine bali kuwakomboa wananchi, ata akina Sumaye, Sitta na Kina Membe ni matajiri wakubwa sana ila hawana uthubutu wa kiutendaji, wangewezaje kuona taifa linadidimia bila kumshauri rais? Lowasa aliweza kushauri na kutoa maamuzi, alafu ndugu yangu swala la utajiri Mungu ndiye anayepanga, usi mjudge mtu kwa alichonacho bali uwezo wake kiutendaji.
Jibu pekee la haya yote ni Mh. Lowasa kuwa Rais wa tanzania.
Hata uoni wake ni hafifu sana na anatembea wima kabisa kama....Hivi ni kweli anatetemeka mikono na hawezi kuandika...
Napenda kuwatakia watanzania kheri ya mwaka mpya wa 2014. Kwa utafiti mchache ila wa kina juu ya waziri mkuu mstaafu Mh. Edward Lowasa nimegundua kuwa, ndiye mtu pekee anayeweza kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na kisiasa hapa nchini. Nchi imekuwa ikiyumba kwa mambo hayo matatu, si kwa uzembe wa Rais Kikwete ila kwa uzembe wa wasaidizi na washauri wa Kikwete. Kwa muda aliokuwa waziri mkuu tuliona mengi aliyofanya na ni hakika kama angebaki adi leo kama waziri mkuu tungekuwa tumeshafuta maadui wa kuu wa taifa hili yaani ujinga, maradhi na umaskini.
Ndugu zangu watanzania, tusisikilize maneno ya watu wasiopenda maendeleo ila tumwombee mh. Lowasa aweze kuja kutuongoza mwaka 2015 Mungu akipenda. Taifa linadidimia, vijana hawana ajira, wengi wamekwama kwenda vyuo vikuu kwa kukosa ada. Jibu pekee la haya yote ni Mh. Lowasa kuwa Rais wa tanzania.