Anselm
JF-Expert Member
- Nov 16, 2010
- 1,710
- 291
Wafalme wa Kandanda Tanzania Bara na wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya Club bingwa Africa jana walitolewa katika hatua ya nusu fainali baada ya kufungwa na Mahasimu wao Simba kwa penalt 4-2.
Ninajua kwa watu wasiokuwa wa mpira wa Yanga kipigo hicho kitakuwa kimewanyong'onyesha sana,kama ambavyo mambumbu wa Simba walivyoshangilia jana kama vile kwa kuingia fainali ya mashindano yale watakwenda kutwaa kikombe hicho na kuliwakilisha bara la Africa kwenye mashindano ya Club ya mabara.
Binafsi nitatofautiana na wengi kwani ninaona kuna faida nyingi Yanga itazipata kwa kutolewa kwenye hatua ile,hapa ninakuwekea faida 3 tu kati ya nyingi:-
1.Kombe lenyewe ni la Mbuzi,halina faida yeyote zaidi ya kuchukuliwa kama sehemu ya mazoezi,ni kwa team zile tu ambazo hazina mtiriko mzuri wa kutwaa vikombe vya maana na vyenye kuboresha CV/Club profile ndo watapambana karibia ya kufa uwanjani.
2.Kutoka ktk hatua ya nusu fainali kutaipa nafasi team ya Yanga kwenda kupumzika kidogo na kuanza mazoezi tena huku wakifanyia kazi mapungufu yote yaliyojitokeza wkt wakishiriki mashindano hayo na hivyo kuongeza kasi ya kutetea ubingwa wao wa Tz Bara na kufanya vizuri pia kwenye mashindano ya kimataifa wanayotarajiwa kuyaanza February.
3.Kuendelea kushiriki kwenye mabonanza ya aina ya Kombe la Mapinduzi kunaweza kuwa'expose wachezaji kwenye majeruhi kiasi cha kuathiri ushiriki wao kwenye mashindano ya maana,ikumbuke ni bonanza hili lilitusababishia Striker wetu Donald Ngoma aitajike kuwa nje kwa muda fulani.
Kwahiyo Wazee wa mabonanza endeleeni kupigania ubingwa wa Mapinduzi mpk jasho la damu liwatoke mkimaliza mtatukuta Bara tumalizie battle yetu ya ubingwa.