Waziri Kombo apokea kombe la ushindi kutoka kwa timu ya wizara ya mambo ya nje-nje sports club

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
1,327
850
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Balozi Mahamoud Thabit Kombo, tarehe 14 Januari 2025, amepokea kombe la ushindi kutoka kwa timu ya Wizara yake, Nje Sports Club, baada ya timu hiyo kushinda katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2025 yaliyofanyika Mkoa wa Unguja Kusini, Zanzibar.
mini_magick20250115-25003-x81cqo.jpg
Hafla fupi ya kupokea kombe hilo ilifanyika katika Ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa Wizara pamoja na Menejimenti.

Akizungumza baada ya kupokea Kombe hilo, Mhe. Balozi Kombo alishukuru Nje Sports Club kwa kuleta ushindi huo, kwani umeiletea heshima Wizara na kupanua wigo wa kuitangaza kupitia michezo.

"Mmefanya vizuri, nimefurahi na nimepokea pongezi nyingi kupitia ushindi mlioupata kwenye mashindano haya. Kwenye michezo, jambo kubwa ni ushabiki, kwani unaongeza nguvu na kuinua morali ya wachezaji kuendelea na michezo kuelekea ushindi," alisema Mhe. Balozi Kombo.
mini_magick20250115-25003-dst9fb.jpg
Aidha, Waziri Balozi Kombo ameupongeza uongozi wa Wizara, akiwashukuru Naibu Katibu Mkuu, Mhe. Balozi Said Shaib Mussa, pamoja na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bi. Chiku Kiguhe, kwa usimamizi mzuri wa wanamichezo wa Wizara ambao umewawezesha kushiriki mashindano wakiwa na afya nzuri na nguvu ya kukabiliana na changamoto, na hivyo kupata ushindi.
mini_magick20250115-25003-osd8ux.jpg
Katika michuano ya Fainali ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2024, timu ya mpira wa miguu ya Nje Sports Club ilitoka sare ya mabao 2-2 na timu ya Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, hatua ambayo ilisababisha timu hizo mbili kushindana katika mikwaju ya penati ili kutafuta mshindi. Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar ilishinda kwa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya Nje Sports Club.
mini_magick20250115-25003-5obdof.jpg
Magoli yao matatu katika fainali yameiwezesha Nje Sports Club kumaliza kama mshindi wa pili katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar 2024, na hivyo kutwaa kombe la ushindi kwa furaha kubwa.

Katika hatua ya nusu fainali, Nje Sports Club ilifanikiwa kuishinda timu ya Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar kwa ushindi wa magoli 3-1, na hivyo kuweza kuingia katika mashinano ya Fainali.
mini_magick20250115-25003-wm1176.jpg
 
Kumbe kuna michezo mingine ilikuwepo.
 
Back
Top Bottom