Mtazamo wangu kuhusu mustakabali wa Zanzibar

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
1,494
1,874
Yanapokuja masuala ya mitazamo au mitizamo (attitudes) kila mtu yuko sahihi kwa upande wake. Kwahiyo hakuna aliye sahihi zaidi kuliko mwingine, wala anayekosea maana ni mtazamo wake.

Wale wanaoona Maalim Seif kakosea tusiwabeze, wana hoja zilizo sahihi kwa mtazamo wao. Na wale wanaoona kapatia wana hoja sahihi kwa upande wao pia. Suala linalobaki kuwa gumu ni je, kugawana vyeo kwa wanasiasa wa juu ndiko kunaleta umoja wa kitaifa kwa Wazanzibari?

Ubaguzi wa kusema huyu chotara, huyu mwarabu, huyu Mpemba, huyu wa Unguja, huyu wa Bara, nk; unaisha? Na ilikuwaje mashehe waliwekwa ndani wakati wa serikali ya umoja wa kitaifa? Ilisaidiaje na itasaidiaje walioteswa kipindi hiki? Kupindua matokeo hadi kufuta uchaguzi kulikujaje chini ya SUK!? Ilikuwaje aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif hadi akaishia kutopeana mkono na aliyekuwa Rais Dkt Ali Shein, tena msibani?

Umoja wa kitaifa usiwe wa kugawana vyeo kwa wanasiasa wachache, bali uwe wa kuwaunganisha watu, kuondoa dhuluma, ufisadi, ubaguzi na kujaliana Wazanzibar wote. Usiwe wa kuwajali au kuwashabikia wasaka tonge na umaarufu wao pamoja na vyama vyao. Chama pekee cha kukijali na kukijenga iwe ni Zanzibar pekee, basi!
 
Tatizo la Zanzibar ni Wazanzibari walio katika madaraka. Wapo tayari kufanya ubaguzi wa kila namna ili mradi waendelee kusalia Madarakani. Hata hivyo kizazi cha Mapinduzi kinaondoka na kikiisha ndipo kizazi kipya kinaweza kuutafuta mustakabali wa Zanzibar.
 
Siku zote 'SUK' zinazoundwa kwenye nchi za Africa huja baada ya uchaguzi kuvurugwa,hivyo wanasiasa wa upande mmoja hutafuta namna ya kuwaridhisha wa upande wa pili kama njia ya kuwatuliza wafuasi wa wapinzani wao.

Hivyo wanasiasa wa ngazi za juu hugawana vyeo huku wafuasi wao wakibaki na mgawanyiko miongoni mwao.

Ifike sehemu raia tukatae kutumika na wanasiasa kama ngazi ya wao kufikia kwenye mafanikio yao, ni hatari mno kujitolea maisha yako na kuishia kujeruhiwa, kukamatwa na kujenga uhasama na mwenzako kisa mwanasiasa ambaye muda wowote anaweza kupewa mkate/keki na hasimu wake na akakusahau wewe.
 
1456109.jpg
457901234.jpg
 
Kwa hakika panahitajika kizazi kipya, si hiki cha wasaka tonge na madaraka
Tatizo la Zanzibar ni Wazanzibara walio katika madaraka. Wapo tayari kufanya ubaguzi wa kila namna ili mradi waendelee kusalia Madarakani. Hata hivyo kizazi cha Mapinduzi kinaondoka na kikiisha ndipo kizazi kipya kinaweza kuutafuta mustakabali wa Zanzibar.
 
Back
Top Bottom