Mtazamo wangu kuhusu kuweka smelter kwa ajili ya mchanga wa dhahabu

Oct 12, 2014
78
48
Tumezuia usafirishaji wa mchanga wa dhahabu na other un-beneficiated ore, Je kuna research yoyote ambayo tunaifanya kujua ni gharama kiasi gani ku Install hizo smelters for beneficiaton?

Report ya TMAA (2011) inaonesha kua ili kuweka smelter na kuendesha kwa faida, tunahitaji tani150,000 za concentrate kwa mwaka kutoka migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ambao hawana uwezo wa kuzalisha kiwango hicho kwa mwaka. Wao wana uwezo wa kuproduce tani 60,000 kwa mwaka.

Teknolojia iliyokuapo mwaka 2011 ni tofauti sana na teknolojia iliyopo mwaka 2017. Gharama zinazoongelewa kipindi kile ni tofauti sana na gharama za kipindi cha sasa hivi. Naamini kuna kampuni zimetengeneza au zinatengeneza smelters ambazo ni low operating cost na pia zinaweza kuaccommodate mchanga wetu wa tani 60,000 kwa mwaka.

Hiyo ni report ya 2011, Je kuna report nyingine ambazo zimeandikwa au kuna research yoyote iliyofanywa kuangalia status ya sasa ikoje? Status means operating cost za smelter, je kuna smelter zenye low operating cost ambazo zinaweza kuaccommodate kiwango chetu cha mchanga wa tani 60,000?

Note: Sijawapinga TMAA wala MEM kwa njia yoyote mana research yoyote inapingwa kwa research na sio kwa maneno ila nawashauri wawe wanafanya hizi research kila mwaka ili watuhabarishe kuhusiana na Smelter na mchanga wa dhahabu na mchanga mwingine wenye madini ndani yake kama Iron ore

My Beneficiation word is “If not today, then when are we going to beneficiate our minerals to increase revenue and level of employment”
 
Some researches (especially when funded by the beneficiaries) tend to seek for a certain answer and turn away answers that do not benefit them. We have to to clear of this. Lets have the research institutions do the research.
Lets give our embassies abroad to do researches on the matter and the outcome be compared. Thereafter we will have a long term answer to the problem, we will also have the options as to which smelter from which country will benefit us
 
Kama huo mchanga haufikii kiwango cha smelter kujiendesha kwa faida, wasubiri mpaka pale watakapoweza kuzalisha mchanga wa kutosha wa smelter kujiendesha kwa faida, tusiingiliane kwenye rasimali zetu, hatupangiwi
 
POINT.
Pia sijui watu wa research wanasemaje,
Kutumia Reasearch (kuna mambo siyaungi mkono mule japo nafuata ushauri kuwa bila resaeach tusipinge) ya Mwaka 2011 leo 2017 juu ya kitu ambacho ni technology based, tena Tunajua technolgy inabadilika kila sekunde sioni kama ni sawa kabisa.

Nakubaliana na hoja ya Kuwa na Serous research institute, Tena napendekeza hata vyuoni kama tunaogopa gharama ya miundombinu vyuo kama UDSM au Nelson Mandera vinaweza kufaa Juu ya Mambo Serious ya kitaifa yanayogusa hadi kizazi cha tatu na cha nne cha kijacho. Maswali kama haya tayari tungekuwa na majibu yake na uamuzi ungekuwa umeshafanyika na muwekezaji anayeshikiria ajira za watu zaidi ya 6000 akajua hatma yake mapema...
 
Nawaunga mkono kuhusiana na kuunda kwa Research Institute ambayo inaweza kufanya hizi Research na kutupa majibu sahihi wananchi wa Tanzania na hizi research Institute ziwe hazifungamani na upande wowote ili watuletee majibu ambayo ni sahihi
 
Muhimu sasa kiwanda cha kuchambua mchanga wa dhahabu kijengwe Tanzania. Ni maoni yangu tu baada ya ripoti iliyotolewa.
 
Thread kama hizi zinafaa kutupwa kapuni.

Mtu anafungua uzi akijua kuna kitu cha maana halafu unakuta maelezo ya line moja.
 
Nawaunga mkono kuhusiana na kuunda kwa Research Institute ambayo inaweza kufanya hizi Research na kutupa majibu sahihi wananchi wa Tanzania na hizi research Institute ziwe hazifungamani na upande wowote ili watuletee majibu ambayo ni sahihi
ii ni kazi ya universities zetu
 
Tatizo watu bright wa research kama Prof Mkumbo ndo wananyamazishwa kwa kupewa vitengo
 
Naamini Report ya Timu iliyoundwa na Raisi imeonesha kua kuna Smelter zinazoweza kuprocess mchanga unaokua produced hapa Tanzania na ndio nliichokishauri hapo juu kua Research ndio itatupa majibu sahihi.

Ni furaha sana unapoona ushauri wako umeleta mchango katika jamii au nchi
 
Back
Top Bottom