Mtazamo wangu kuhusu demokrasia (customized democracy)

Rwaz

JF-Expert Member
May 3, 2013
1,969
3,320
Salaam! Nitangulie kusema tu hili ndo jukwaa pekee la kutandaza mawazo na hisia zetu wengine tuliopoteza tayar wazee wa kuanzia kutuchuja fikra na wasomi kuwa busy au mbali au kutokuwepo. Hivyo nieleweke tu binafs mtazamo wangu umeanzia hapa hapa. Na elim yang ya siasa na uongoz au utawala iko kwenye kijivu. Kuna namna nyingi za watu kuongozana/kutawalana. Demokrasia ni mojawapo tu. Leo nitembelee mtazamo wa Churchill (‘Many forms of Government have been tried, and will be tried in this world of sin and woe. No one pretends that democracy is perfect or all-wise. Indeed it has been said that democracy is the worst form of Government except for all those other forms that have been tried from time to time.…’). Naona ni kama kinachofanya maendeleo ya wananchi si mfumo wa kiutawala bali nafsi ya mtawala mwenyewe. Kama ni mzalendo hata akiwa mfalme mtaendelea tu. Kama ni mbinafs na mlafi hata mkitunga sheria
zipi atapata namna ya kuzisigina na kutuibia na kutudhoofisha tu. Bas nataman kama ilivyo kwamba bunge hutunga sheria kwa niaba yetu na KURA WAPIGE WENYE SIFA ZA KUJITAMBUA. Nafikiria tafsir ya Bi Hillary Clinton kushinda kura za raia lakin kuukosa urais! Kwa vile kwa dunia ya leo si rahis kuihama demokrasia hii nashaur wataalam wa siasa WAUNDE CUSTOMIZED DEMOCRACY! Inayoendana na jamii yetu ya kiafrica na kitanzania. 'Customised' namaanisha kama lilivyo gari aina flan unavyoweza kuliongezea vitu vinavyokidhi mahitaj yako iwe kimuundo au muonekano au accessories. Nataman kukutana na kitabu kinachoelezea jins demokrasia inayotufaa kama Tanzania inavyoweza kuwa tofaut na ya nchi nyingine. Hapa bila shaka mtaalam ataongelea namna ya kudhibit udikteta ndan ya mfumo wa kidemokrasia na namna ya kumlea mtawala mzuri aendelee kuendeleza.
 
Makes sense to some point ...
Lakini nadhani nchin kwetu tu nafuatia mfumo huo wa customized democracy ambayo ni nchi ya chama kimoja kinachoamua nani awe rais na mwenyekit wake alaf yeye anaongoza nchi na chama anavotaka kwa shadow ya katiba then bunge linakuwa rubber stamp ya maamuzi yake.... nchi I naenda siku zinaenda. ...
Masikini wale wale matajiri wale wale wengine wanageuka mashetani haya....
All is well here....
 
Una wazo zuri ,tatizo kubwa ni kwa baadhi ya watawala kutokuheshimu katiba.Tunahitaji katiba mpya itayoondoa madaraka yanayomfanya Rais kuwa juu hata ya katiba pia.Tukipata katiba bora yenye taasis na mifumo imara mengine yatasonga.
 
Back
Top Bottom