Mtazamo wangu juu ya washabiki wa kisiasa!!!

Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,416
12,604
Washabiki (namaanisha wapenzi wa kweli) wengi wa siasa, ukiacha wanasiasa wenyewe ni watu ambao wana uelewa mdogo wa mambo, na ni watu ambao wakishampenda mtu basi huwaambii kingine chochote juu ya mtu huyo, huwa reasoning yao ni ndogo sana. Wao ndoto zao ni kwamba ni wanasiasa ndio watakaowatoa kwenye hili lindi la umaskini, na wanakaa wanasubiri kama vile hao wanasiasa watawaletea hela mifukoni mwao.

Mara nyingi nimekuwa kwenye vijiwe vya draft, kwenye daladala unashangaa watu wanabishana juu ya huu mzozo wa CDM na kila upande una point zake ambazo ni nje ya zile zinazotangazwa na wahusika, sasa unajiuliza siku zote hizi, zaidi ya wiki sasa lakini bado watu hawajui sababu ni nini, wanabishana tu, hata kujua habari za waraka hawana, sasa ukichagua upande wa Zitto ukawaeleza mabovu ya CDM Mbowe na Dr Slaa kwa kutumia point za Buku & utashangaa wanaanza kukubali bila hata kufikiria, au ukiamua kuwa timu Mbowe ukawambia Zitto ni mroho wa madaraka, wanakubali pia. Unaweza kuona jinsi taarifa zinavyochelewa kufika kwa wapiga kura, na wa kwanza kuwafikia ndiye mshindi, maana wakishasikia hili hawana muda wa kusikia lingine kabisa.

Wanasiasa katika kulijua hili, wanaangalia nani anaweza kuwa mbishi mbishi, wanampa kitengo cha uhamasishaji, wanamlipa, anafanya kazi hata kama sera hazikubali, ili mradi alipwe, ataenda kuzungumza vitu ambavyo kimoyomoyo anajua ninahadaa watu.

Mfano kwenye huu mzozo wa Zitto nina uhakika kuna watu wako upande wake bila hata kuwa na uhakika kama ana malengo mazuri ama mabaya, ili mradi tu wanampenda, kwa sababu wanazozijua wao, kuna wengine ni za kidini, za kikabila, za kiutendaji, kimaslahi nk, hivyo hawatakaa wakusikie ukizungumza unafiki wa Zitto popote pale.

Pia kwa wale Team Mbowe/Dr Slaa pia kuna watu wana mapenzi nao kwa sababu zile zile za kidini, kikabila, kiutendaji, kimaslahi nk, hawa hawataki uwaambie kwamba Mbowe (Mkwe wa muasisi wa chama) anaitumia CDM kufanikisha biashara zake, wala kusikia kwamba Dr na Mke wake wanaitumia CDM vibaya, sijui uzungumzie hela za chama no! Wameshapenda wameshapenda.

Halafu utashangaa wale wote wanaoelewa vizuri, hasa hasa watu wenye information, hawaendi kupiga kura, aslimia 70 ya wanaoelewa watasema wako bize siku ya kura, hivyo kura zinapigwa na wale ambao sio waelewa wa ukweli, wao hata sumu wanameza tu. Na ni style hii ambayo imekuwa ikiwaweka CCM madarakani, eti Kinana akibeba tofali moj begani kwenye kujenga, akapigwa picha inatosha kuonyesha CCM inajali, na walioona wataipigia kura.

CDM kama chama kinachahitaji madaraka kina kazi kubwa ya kuelimisha watu nini maana ya kuchanganua sera, lakini kikae tayari pia kwamba watu wakielewa watakiuliza kuhusu yale ambayo yanaenda tofauti na matarajio, majibu ya usaliti, uhaini, umetumwa na mengineyo ya kushushana confidence siku yakiisha, tutachukua hii nchi.

Chonde chonde great thinkers wa JF, ni wakati mwafaka sasa wa kwenda kufanya kampeni hata kama ni kwenye vile vijiwe tunavyoshinda, kwenye jumuia zetu, kwenye vikao vyetu vya bar etc, kuwasimulia nini tunajua juu ya hizi siasa hasa kwa msaada huu wa JF, kila mmoja awe mwelewa na kuweza kupambanua nani mbaya nani mwongo.

Na declare interest kwamba sijafurahishwa na maamuzi ya CDM, lakini pia naiona kama ni njia pekee nzuri ya kuachana na maisha ya wasiwasi juu ya watu tusiowaamini ndani ya nyumba, unalala ukiwa una wasi wasi, unaogopa hata kufumba macho usije ukachomwa kisu. Baada ya haya maamuzi, pia na sisi tukubali kubadilika, kwa kutumia mabovu yaliyotajwa kwenye ule waraka, tujirekebishe; ninaamini hata sisi tunajua kwamba kuna mengi ya ukweli kwenye ule waraka, so tukiufanyia kazi tutashinda. Tusipoufanyia kazi kuna kina MM wengine watakaokuja, labda wao watajiita NN, lakini watakuja na point hizi hizi. Nasema hivi kwa sababu hii sio mara ya kwanza watu kuvuliwa uongozi kwa malalamiko kama haya.
 
Back
Top Bottom