Mtazamo pinzani ( critical thinking) juu ya uchaguzi, Tanzania

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Nimejaribu sana kutafuta neno la kiswahili juu ya critical thinking. Ziko maana kadhaa ambazo hata zenyewe kuzisema ni msamiati mgumu kwa wengi.

Nieleze tu kwamba ninachotaka kuonyesha katika andiko langu ni mawazo mbadala ambayo yanatokana na mie kuyaona mambo katika jicho jingine, siyo la kupinga, Bali kusema upande mwingine wa jambo ambao unaweza kuwa haujaonwa na wahusika au wanaogopa kuusemea. Kumbuka Kila wakati kwamba sarafu huwa na pande mbili, andiko hili ni upande wa pili wa sarafu, tuuone pia.

Nishukuru serikali na hasa Rais wetu, kwa utashi siyo tu wa kisiasa, Bali namuona kama kiongozi ambaye ana picha kubwa (big picture) jinsi ya kuongoza nchi inayotaka kuwa na maendeleo ya kweli kwa maana ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na hata kistaarabu.

Jambo ambalo mpaka Sasa Sina hakika nalo ni kama kweli Kuna watu na hasa hawa watengeneza sera ( policy makers), wakiwemo na watu wa chama chake kama hakika Wana muono( vision) kama wake.

Kumbuka siyo tu viongozi ndo hutengeneza watu (kama mpendwa Rais wetu anavyofanya), bali watu nao Kuna wakati huwategeneza viongozi ( kama ninavyoona upepo wa watu nje yake wanavyotaka kujaribu kumtoa kwenye maono yake).
It isn't only the leaders who shape the society, the society can also shape it's Leaders.

Tusubiri tuone wakati nyakati zinaenda kama kweli kiongozi( Rais) atawa shape CCM au CCM watam shape yeye !

Nikija kwenye kiini Cha andiko langu, nikubaliane na wengine kwamba tunahitaji mabadiliko, yawe ya Katiba , kisheria, ya tume ya uchaguzi nk.

Wengi wanaongea juu ya tume ya uchaguzi kuundwa upya na kuwa na kinachoitwa tume huru. Inasikika vizuri kuwa na tume huru, lakini swali ambalo hatujajiuliza ni je tume ni Kila kitu katika uchaguzi?

Kwangu Mimi na hasa kwa uzoefu wa chaguzi za kiafrica, ninasema hapana. "Kuna jambo ambalo nadhani tunapoongea juu ya haki na kuwa na uchaguzi huru lazima lisemwe au liwe addressed."

Na jambo lenyewe ni vyombo vya Dola au majeshi ukitaka. Nionavyo Mimi ( critically thinking) ni mpaka tu majeshi au vyombo vya Dola, vitakapoamua kuwa neutral kwa maana ya kutopendelea upande wowote ndo tutakapokuwa na uchaguzi ulio huru na wa haki

Ebu nambie, kama una vyombo vya Dola ambavyo vitakuwa vinaegemea mlengo Fulani, utakuwa na hakika ya uchaguzi huru na haki?

Kama unajua mienendo ya nchi wakati wa chaguzi popote duniani, wakati huu nguvu zote za utekelezaji katika nchi huwa ziko kwa kiwango kikubwa juu ya vyombo vya Dola.

Wanaotafuta kuingia madarakani huzitegemea na wanaotafuta kubaki madarakani huzitegemea pia.

Wanaotafuta kuingia madarakani, hutegemea nguvu hii Ili kuwasaidia kuingia madarakani bila mzunguko na bughudha endapo watakuwa wameshinda kura . Na kwa upande mwingine walioko madarakani walioshindwa kwa mfano, hutafuta support yao Ili kubaki kwa kutaka kutumia vyombo vya Dola.

Wakati walioko madarakani wameshinda kihalali, hapo si pa kujadili manake mambo huwa as business as usual. " Hakuna shida"

Uchaguzi uliofanyika karibuni nchini Gabon, baada ya Rais aliyekuwa madarakani kuona anaelekea kushindwa, aliagiza tume ya uchaguzi imtangaze yeye kuwa mshindi, ilihali kura bado zilikuwa zinahesabiwa.

Nambie katika mazingira hayo kama vyombo vya Dola vingekuwa upande wake, ndo ilikuwa imetoka hiyo. Matokeo Yale yalikataliwa na Jeshi, bahati nyingine mbaya tu ni kwamba, badala ya kutaka uchaguzi urudiwe au hata kusimamia umaliziaji wa kuhesabu kura Ili mshindi apatikane kidemokrasia, wao Wakachukua madaraka ya nchi. ( Narudia hii ni bahati mbaya sana).

Hivi hatuoni nguvu ya vyombo vya Dola katika chaguzi zetu? Kwa mfano mtu anayeweza kupewa amri ya kuhamisha sanduku la kura au kusimamia uhamishaji wa Hilo sanduku kwenda kusiko, unaachaje kumjadili huyu, Ili aelewe majukumu yake kikatiba na asimamie haki za watu?

Kabla sijahitimisha andiko langu, nimetambua kwa hakika kabisa kwamba, wakati vyombo vya Dola vinapokuwa havina mrengo katika kusimamia michakato yote ya uchaguzi, ni lazima uchaguzi huo utakuwa huru.

Wanasiasa, watawala, na hata wazee wa kuiba kura, wakati huu huwa Hawana nguvu Wala ujanja. Utafanyaje ujanja mbele ya vyombo vya Dola?

Nguvu za Hawa huja tu wakati Kuna consent ya vyombo hivi.

Nionavyo mie, pamoja na harakati zote za elimu ya Katiba, uchaguzi, nk, uchaguzi huru na haki utapatikana wakati majeshi yetu yanajua na yanapokuwa huru ( neutral) kulinda Katiba na haki za watu wote.

Tunapojadili juu ya mambo mengine yote, tukumbuke factor ya majeshi au niseme kidiplomasia, vyombo vya Dola. wakati havijawa neutral, vikawa consumed na haki za watu, na vikatetea na kulinda Katiba ambayo basically inalinda watu na haki zao, chaguzi zitaendelea kuwa mahali pa vilio

Mungu ibariki Africa, Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom